BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
TAWHIDI NI KIINI CHA ELIMU
TAWHIYD NI KIINI CHA ELIMU NA MAFUNZO YOTE YA UISLAMU.
Sisi tuna itakidi ya kuwa; mambo muhimu yanayohusiana na elimu na taaluma bora ya Mwenyeezi Mungu ni Tawhiyd, na kuwa na imani ya kuwepo Mola mmoja aliyetakasika, kwa hakika Tawhiyd sio msingi miongoni mwa misingi ya dini tu, bali, mbali ya kuwa Tawhiyd ni msingi wa dini vile vile ni kiini cha itikadi zote za Kiislamu, na tunaweza kusema kuwa; Misingi na matawi ya Kiislamu yamejikusanya katika misingi ya Tawhiydi, kila kipengele miongoni mwa vipengele vya Islamu kumezungumzwa masuala ya Tawhid, na kuwa na imani na Mola mmoja, tawhiydi katika sifa na matendo ya Mwenyeezi Mungu, Tawhiyd katika malengo mamoja walikuja nayo Mitume walipokuwa wakilingania nyumati zao, Tawhiyd katika dini moja miongoni mwa dini za Mwenyeezi Mungu, Tawhiydi katika kibla na vitabu vya mwenyeezi Mungu, Tawhitdi katika hukumu na sheria za Mwenyeezi Mungu kwa wanaadamu wote, na hatimae Tawhiyd kwa Waislamu wote na tawhiyd kwa siku ya Kiama, na kwa sababu hiyo basi, Qur-ani takatifu inabainisha kuwa upotoshaji wowote ule utakaofanywa katika tawhiyd ya Mwenyezi Mungu ni uovu usiosamehewa na ni shirki kubwa.
إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ اَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ وَمَن يُشْرِكْ بِاللهِ فَقَدِ افْتَرَي إِثْماً عَظِيماً[1]
Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa.
وَلَقَدْ اُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَي الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكَ لَئِنْ اَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ[2]
Na kwa yakini yamefunuliwa kwao, na kwa wale waliokuwa kabla yako (maneno haya):- kama ukimshirikisha (Mwenyeezi Mungu) bila ya shaka amali zako zitaruka patupu, (hutazipata thawabu japo ni amali njema), na lazima utakuwa miongoni mwa wenye hasara.
MATAWI YA TAWHIYD.
Sisi tuna itikadi ya kuwa tawhiyd ina matawi mbali mbali, na kuna manne muhimu miongoni mwa hayo, nayo ni haya yafuatayo:-
A: TAWHIYD KATIKA DHATI YAKE ALLAH (S.W).
Yaani dhati ya Allah (s.w) ni moja, naye ni mmoja tu, asiyefanana na kitu chochote ulimwenguni.
B: TAWHIYD KATIKA SIFA ZAKE ALLAH (S.W).
Tawhiyd katika sifa za Mwenyeezi Mungu, yaani sifa zote za Mwenyeezi Mungu, mfano elimu, Qudra na uwezo, ubakiaji wa milele wa Allah (s.w), na sifa nyengine nyingi zote ziko katika dhati yake Allah (s.w), sio kama sifa za viumbe, kwani sifa za viumbe haziko ndani ya udhati wa viumbe bali ziko nje ya viumbe, ama ni lazima tuzingatie kuwa; dhati hiyo ya sifa za Mwenyeezi Mungu inahitajia tafakuri na mazingatio ya kifikra.
[1] Suratun Nisaa Aya ya 48.
[2] Surat Az-Zumar Aya ya 65.
MWISHO