MABAINISHO YALIYOBAINISHWA KWA NJIA NYEPESI
  • Kichwa: MABAINISHO YALIYOBAINISHWA KWA NJIA NYEPESI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 13:34:15 3-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

VIPENGELE VYA MIUJIZA YA QUR-ANI -1- (B)

Katika makala ya mwanzo tulielezea nyanja ya mwanzo ya miujiza. Katika makala hii tutaendelea na nyanja nyengine zifuztazo:-

B. MABAINISHO YALIYOBAINISHWA KWA NJIA NYEPESI.

Nyanja ya pili miongoni mwa sehemu ya miujiza ya mabainisho ni:-

Mabainisho yaliyobainishwa katika Qur-ani yamewapelekea kuwajalibisha na kuwavutia watu wa jamii ya kiarabu, njia zilizotumika katika kuibainisha Qur-ani hazijafanana wala kukaribiana na zile njia zilizozoweleka ambazo zinatumiwa na watu wa jamii ya Kiarabu.

Ni jambo la kustaajabisha kuona Qur-ani imetumia maneno yaliyoepukana na kila kasoro na ubainishwaji huo mwepesi umepelekea kukubaliwa na wasikilizaji wa Qur-ani, na umewafanya watu wa jamii ya kiarabu (Waarabu) watoke nje na zile njia zao zilizo maarufu, la kuvutia zaidi ni kwamba Qur-ani imetumia maneno na njia zote nzuri za ubainishaji, na imeepukana na zile njia za aibu, au mbaya (yaani zilizo na kasoro).

Aina (njia) za maneno – ambazo zimezoeleka na watu wa jamii ya Kiarabu ni hizi zifuatazo:-

Mashairi, ni maneno ambayo yana mezani na vibwagizo, Nathri , (nathri ni maneno yaliyoparaganyika yasiyokuwa na nidhamu hayana mezani wala vibwagizo), na Saj-i (Saj-i ni sentensi fupi zilizo na vibwagizo lakini hazina  nidhamu wala mezani maalumu).

Kila njia moja katika njia tatu hizo zina uzuri wake na ubaya wake, ama ubainishaji mwepesi wa Qur-ani ni wenye kujalibisha na kuvutia na umekusanya njia tatu zote hizo, yaani shairi, nathri na saj-i.

C. NIDHAMU NA MPANGILIO KATIKA SAUTI ZA QUR-ANI

 Wakati tunapotega sikio kusikiliza sauti ya Qur-ani kitu cha mwanzo kinachotuvutia na kutujalibisha ni sauti tunayoisikia pindi inaposomwa Qur-ani hiyo, katika nidhamu hiyo kwa kuzingatia harka (fat-ha, kisra, dhamma) zilizotumika katika ibara hizo za Qur-ani sauti huingia masikioni, sauti ambayo huifanya nafsi ya mwanaadamu kuwa na shauku ya kuisikiliza, na huingiwa na furaha nyoyoni mwake, hiyo ni nidhamu ya sauti ya Qur-ani ambayo humfanya mwanaadamu aihisi katika nafsi yake. Kwa kutowa mfano na tuangalie na kuisoma Surat Najmi kuanzia Aya ya 1-18. Allah (s.w) anasema:-

وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَي .مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَي . وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَي . إِنْ هُوَ إِلاَّ وَحْيٌ يُوحَي . عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَي . ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَي . وَهُوَ بِالاُفُقِ الاَعْلَي . ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّي .فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ اَوْ اَدْنَي .  فَاَوْحَي إِلَي عَبْدِهِ مَا اَوْحَي . مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَاَي اَفَتُمَارُونَهُ عَلـٰي مَا يَرَي . وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً اُخْرَي . عِندَ سِدْرَةِ الْمُنْتَهَي . عِندَهَا جَنَّةُ الْمَاْوَي إِذْ يَغْشَي السِّدْرَةَ مَا يَغْشَي . مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَي .لَقَدْ رَاَي مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَي[1]   

Naapa kwa nyota zinapoanguka (zinapokuchwa). Kwamba mtu wenu (huyu Nabii Muhammad) hakupotea (kwa ujinga) wala hakukosa (na hali ya kua anajua); Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya (anayosema) ila ni wahyi (ufunuo), uliofunuliwa (kwake). Amemfundisha (Malaika) Mwenye nguvu sana,Mwenye uweza. Na yeye (huyu Jibrili) akalingana sawa sawa.Na yeye yu katika upeo wa kuona, (Horizon) (katika mbingu kwa) juu kabisa. Kisha akakaribia (kwa Mtume) na akateremka. Ukawa (ukaribu wao) ni kama baina ya upinde na upinde au karibu zaidi. Na akamfunulia huyo Mtumwa wake (Mwenyeezi Mungu) Aliyoyafunua.Moyo haukusema uwongo uliyoyaona. (Moyo wake ulisadiksha yale yaliyotokea).Je! Mnabishana naye juu ya yale anayoyaona (daima)? Na (Mtume) akamuona (Jibrili) mara nyengine (kwa sura ile yake ya Kimalaika katika usiku wa Miiraji). Penye Mkunazi wa kumalizikia (Mambo yote). Karibu yake ndiyo kuna hiyo Bustani, (pepo) itayokaliwa (maisha na hao watu wema). Kilipoufunika Mkunazi huo kilichoufunika (katika mambo ya kiajabu ya kimbinguni). Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka (uliowekewa).Kwa yakini aliona (Nabii Muhammad) mambo makubwa kabisa katika alama, (Qudra) za Mola wake.

Maelezo kuhusiana na Suratun Najm

Hapa inatajwa habari ya Miiraji ya Mtume (s.a.w.w) - kwenda mbinguni.-

Ndani ya Sura hii Mola wetu anakula kiapo kwa nyota kwa ajili ya kuwahakikishia waja wake utukufu, daraja pamoja na sifa alizonazo Mjumbe Wake Muhammad (s.a.w.w). Angalia basi ni nani mwenye kutoa sifa hizo na ni nani anayesifiwa katika Aya za Sura hii? Mwenye kutoa sifa hapa za kumsifu Mtume (s.a.w.w) ni Mola Mtukufu, hebu uangalia mtiririko wa sifa hizo ulivyopangika katika Aya hizo za Suratun-Najmu. Mola katika Aya hizo Anasema:

وما ینطق عن الهوی.  إن هو إلا وحی یوحی. علمه شدید القوی.  ذو مرة فاستوی.  وهو بالافق الاعلی. ثم دنا فتدلی  فکان قاب قوسین أو أدنی.

Maana yake ni kwamba: “Naye hazungumzi kitu kwa kupitia matamanio yake, bali hayo (asemayo) hayakuwa ni kitu chengine bali ni Wahyi ulioshushwa kwake, Wahyi ambao amefunzwa na Jibraail mwenye uwezo aliye madhubuti ambaye alisimama sawasawa katika kazi yake ya ufikishaji wa Wahyi wa Mola wake hali akiwa yeye ni mwenye upeo wa hali ya juu wa uoni na utambuzi, kisha Mtume akamkaribia na kumkaribia zaidi Mola wake, hadi masafa yaliopo baina Yake na Mola wake yakawa ni kiasi cha kutoka ncha moja upinde hadi ncha ya pili (kiasi cha dhiraa mbili) au karibu zaidi…”. Mola aliendelea kumsifu Mjumbe wake (s.a.w.w)  katika Aya  hizi hadi akasema:

Ustadi Dirozi anasema herufi hizo zilizotumika katika sura hiyo, wakati zinaposomwa ni kama mtu anayesoma kasida yenye kuvutia na inayobembeleza kwa kuzingatia yale yaliyomo.

Wakati tunapozisoma Aya za Surat Dhuha tunakabiliana na vibwagizo na maneno ambayo yamefanana na mashairi ijapokuwa sio mashairi hiyo ni nidhamu na mpangilio wa sauti ambao ndiyo siri ya muujiza wa Qur-ani.

[1] Surat Najmi kuanzia Aya ya 1-18

MWISHO