BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
DALILI ZINAZOTHIBITISHA KWAMBA MOLA NI MMOJA 2
MATAMANIO YA NAFSI (STIMULUS NATURAL)
Viumbe wote tangu wanapozaliwa wanakuwa na matamanio ya nafsi, na matamanio hayo yanawapelekea wanaadamu kupata jawabu ya mahitajio yao ya kidunia na akhera, lakini mbali ya kuwa mwanaadamu ana matamanio ya nafsi vile vile ana matamanio mengine ambayo ni ya juu zaidi, matamanio hayo yamo katika moyo wa mwanaadamu, na hayawezi yakampotosha na kumuweka katika njia mbaya ,kwa sababu Mwenyeenzi Mungu ndiye aliyemjaalia na kumtunukia mwanaadamu neema hiyo. Kwa mfano: -
(Mwanaadamu yoyote anapendelea mazuri na anachukia mabaya), mwanaadamu yoyote anajua kwamba kumdhulumu mtu sio jambo zuri, hata kama hajasoma lakini nafsi yake inahukumu ya kwamba dhulma ni dhambi, na vile vile nafsi yake inahukumu kuwa kufanya jambo jema ni vizuri. Matamanio hayo yaliyomo ndani ya nafsi ya mwanaadamu yanaitwa (matamanio ya nafsi). Na matamanio hayo yanamuongoza mwanaadamu katika njia njema.
Katika sehemu hii na tuzingatie mifano hii ya aya inayothibitisha maudhui hayo.
MWANAADAMU NI MWENYE KUKUBALI (UKWELI) HAKI
Mwenyeenzi Mungu amemuumba mwanaadamu na kumpa uwezo mwanaadamu huyo wa kupambanua jema na baya, qur-ani kariym inaelezea uhakika huo kwa kusema:-
فَاَلْهَمَهَا فُجُورَهَا وَتَقْوَاهَا[1]
Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake.
Aya hiyo inathibitisha kuwa mwanaadamu ni mwenye uwezo wa kupambanua kheri na shari, na matamanio ya kheri humuongoza mwanaadamu katika njia ya haki na kumuonyesha ukweli wa mambo, aya ya Qur-ani inathibitisha tokeo lililotokea kwa wachawi wa firauna kwa kusema:-
فَاَلْقَي مُوسَي عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا يَاْفِكُونَ فَاُلْقِيَ السَّحَرَةُ سَاجِدِينَ قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ الْعَالَمِينَ[2]
Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua.Hapo wachawi walipinduka wakasujudu.Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Mfano mwengine unaoelezea uhakika huo ni kuhusu firauna, firauni ambaye hakuwa na imani yoyote juu ya kuwepo kwa Mwenyeenzi Mungu mmoja, firauni alistahiki kuadhibiwa kutokana na kibri na (ghururi) alichokuwa nacho, njia zote za tawba zilikuwa tayari zimeshafungwa, na pale Mwenyeenzi Mungu alipomteremshia adhabu ya kumzamisha baharini alisalimu amri na kudai kwamba anamuamini Mola mmoja. Alidai ya kuwa yeye hana nguvu zozote, na alifahamu kuwa uwezo na nguvu zote ziko kwake yeye Allah (s.w), basi alimuamini Mola mmoja lakini Mwenyeenzi Mungu hakumkubalia tawba yake hiyo, qur-ani imeyathibitisha hayo kwa kusema:-
وَجَاوَزْنَا بِبَنِى إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَاَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ وَجُنُودُهُ بَغْياً وَعَدْواً حَتَّي إِذَا اَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ اَنَّهُ لا إِلِـهَ إِلاَّ الَّذِى آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَاَنَاْ مِنَ الْمُسْلِمِينَ[3]
Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa hapana mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa walio nyenyekea! (waislamu).
Maelezo kuhusiana na aya
Mwenyeenzi Mungu amebainisha dhahiri- hasa katika aya ya 18 ya Suratun- Nisaa kuwa toba haikubaliwi wakati mauti yamekwishafika. Na mauti mtu hajui yatamshambulia lini:
وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّي إِذَا حَضَرَ اَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّى تُبْتُ الآنَ وَلاَ الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ اُوْلَـئِكَ اَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَاباً اَلِيماً[4]
Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia. Wala wale wanao kufa na hali wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu.
Basi sio vibaya na kujikumbusha na shairi hili lifuatalo:-
Mauti sidhani Yana muhala
Milele ziumbe hufa ghafula
Muamini hamba Chenda kulala
Sipamabaukiwi Nili mzima.
Basi tujitahidi kuchuma mazuri upesi na kuepuka kila mabaya.
Nawe siliwaye ukaikuwa.
Ni haki mauti Yafaridhiwa
Numanuma taa Ukikutiwa
Ufiye dinini Mwake hashima.
[1] Surat shams aya ya 8
[2] Surat Shuaraa aya 45-47
[3] Surat Yunus aya ya 90
[4] Suratun-Nisaa aya ya 18
MWISHO