KUITUKUZA QUR_ANI
  • Kichwa: KUITUKUZA QUR_ANI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 20:43:46 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

KUITUKUZA QUR_ANI

Walidi bin Mughera alikuwa ni mmoja katika maadui wa kiislamu na Mtume Muhammad (s.a.w.w), Siku moja wakati alipokuwa akisikiliza Qur-ani alisema:-

“ Qur-ani ni kitabu kizuri kutokana na yaliyomo ndani yake, na ni kitabu chenye kuleta jazba kwa mwanaadamu. Qur-ani ni kitabu bora na hakuna kitabu bora chengine zaidi ya Qur-ani,

Maelezo hayo yalimfikia Abu Jahli, na Abu Jahli alikwenda kwa Walidi bin Mughera na kumwambia:-

“Kaumu yako imekusanya mali na kukuletea wewe ili uwache kuisifu Qur-ani, mughera alimjibu abu jahli kwa kusema:-

“Mimi nina mali zaidi ya kaumu yangu, na ninajuwa njia za uzungumzaji, kwa hakika maneno anayozungumza Muhammad (s.a.w.w.) ambayo yamo katika Qur-ani sio mashairi.

Abu jahli akasema:

“Ni lazima utafute njia ili kuiridhisha na kuifurahisha kaumu yako”.

Walidi bin Mughera aliomba fursa kwa Abu Jahli ili alifikirie jambo hilo, baada ya kulifikiria jambo hilo alisema:

“Huu ni uchawi- yaani Qur-ani ni uchawi, na maelezo yaliyomo humo yametungwa na mwanaadamu. Walidi bin Mughera aliyasema maneno hayo kutokana na kinyongo alichokuwa nacho moyoni mwake nay eye mwenyewe alielewa wazi kwamba maneno hayo hayana ukweli wowote, kwani Qur-ani muujiza utokao kwa Mwenyeezi Mungu (s.w).

 MUUJIZA WA QUR_ANI

Moja miongoni mwa miujiza ya Qur-ani ni kwamba Qur-ani imekuja na mtume ambaye umi.

Umi ni mtu gani? , katika kipengele hiki hapana budi kuelezea maana ya neno umi ili liweze kueleweka maana yake.

Umi ni mtu ambaye hajuwi kusoma wala kuandika, Mwenyeezi Mungu mtukufu anasema:-

وَمَا كُنتَ تَتْلُو مِن قَبْلِهِ مِن كِتَابٍ وَلاَ تَخُطُّهُ بِيَمِينِكَ إِذاً لاَّرْتَابَ الْمُبْطِلُونَ

Na hakuwa mwenye kusoma kitabu chochote kabla ya hiki, wala hakukiandika kwa mkono wako wa kuume (kulia), ingekuwa hivyo wangefanya shaka wale wanaotaka kubadilisha (haki).

Muujiza mwengine miongoni mwa miujiza ya Qur-ani ni:-

Ustadh Amiyn Rayhani masiyhi katika barua aliyomuandikia Alameh Sheykh Huseyni Kashif Alghataa anasema:-

Nyinyi mnasema kwamba Qur-ani ni muujiza nah ii ni kauli ya kweli nay a haki, mimi katika kipindi nilichokuwa nikiiishi London na Amerika wakati mwingi nilikuwa nikiisoma Qur-ani kwa lugha hiyo hiyo ya kiarabu, ambapo jambo hilo liliwafanya majirani zangu waingiwe na jazba pindi niisomapo qur-ani, na waliingiwa na mshawasha akilini mwao kutaka kuijuwa Qur-ani.

Carbon anasema:-

“ Kama kusingelikuwa na miraji, kama Muhammad (s.a.w.w.) hakuwa na tabia nzuri na tukufu, na kama Qur-ani haikuwa ikimuongoza mwanaadamu na kumuongowa hakuna shaka kwamba aya zilizomo ndani ya Qur-ani zingelitosheleza kusidikisha Utume wa hadharati Muhammad (s.a.w.w).”

و بشر عبادی الذین یستمعون القول فیتبعون احسنه

Na wapeni malipo na ujira wale waja wangu ambao huyasikiliza maneno yangu na hufuata njia bora.

1. Miujiza yote ya Mitume iliyopita ilikuwa ni ya muda na sehemu maalumu, lakini Qur-ani haina muda maalumu, na imeenea katika sehemu na pande zote nne za dunia, na itabakia hadi milele.

2. Qur-ani iko hai na itabakia hai kwa kumuongoza mwanaadamu katika njia iliyonyooka.

3. Qur-ani inazungumza ukweli na haki, na wala haizungumzi kwa kupendelea upande fulani au nasaba fulani.

 

MWISHO