SIFA TUKUFU ZA MWENYEEZI MUNGU
  • Kichwa: SIFA TUKUFU ZA MWENYEEZI MUNGU
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 21:34:25 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

SIFA TUKUFU ZA MWENYEEZI MUNGU.

Qur-ani kariym amemsifu na kumuelezea Mwenyeezi Mungu kwa sifa zilizo bora na kamili kabisa, na imejiepusha na kumuelezea kwa sifa mbaya. Katika Suratul-Hashri Aya ya 22-24 tunasoma:-

هُوَ اللهُ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ هُوَ الرَّحْمَنُ الرَّحِيمُ[1]

Yeye ndiye Mwenyeezi Mungu ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye tu. Anayejuwa yaliyofichikana na yaliyo dhahiri. Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.

 هُوَ اللهُ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلاَمُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ الْمُتَكَبِّرُ سُبْحَانَ اللهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ[2]

Yeye ndiye Mwenyeezi Mungu ambaye hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa Yeye tu; Mfalme, Mtakatifu, Mwenye salama, Mtoaji wa amani, Mwenye kuyaendesha Mwenyewe mambo yake, Mwenye shani, Anayefanya analolitaka, Mkubwa. Mwenyeezi Mungu Yu mbali na hao wanaomshirikisha naye.

هُوَ اللهُ الْخَالِقُ الْبَارِئُ الْمُصَوِّرُ لَهُ الاَسْمَاء الْحُسْنَي يُسَبِّحُ لَهُ مَا فِى السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضِ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ

Yeye ndiye Mwenyeezi Mungu, Muumbaji, Mtengenezaji, Mfanyaji wa sura (za namna namna za viumbe); Mwenye majina (sifa) mazuri. Kinamtukuza kila kilichomo mbinguni na ardhini. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

 Sifa hizo njema na nzuri za Mwenyeezi Mungu zimetajwa na kuelezewa katika Qur-ani, ama katika vitabu vyengine zimeelezewa vyengine kabisa kiasi ya kwamba uelezewaji huo ulioelezewa katika vitabu vyengine haufanani na sifa za Mwenyeezi Mungu.

Katika Kitabu cha Taurati cha sasa hivi ambacho kimeharifiwa, Mwenyeezi Mungu amesifiwa kwa sifa mbaya zisizokubalika kuwa ni sifa za Mwenyeezi Mungu, katika kutunga stori ya mji wa Babil Mwenyeezi Mungu alikuwa ana hofu ya kuwa pindi wanaadamu wakikusanyika atakutwa na hatari ya wanaadamu hao kufahamu siri ya Uungu wake, kwa hiyo alimuamrisha Jibril kuwakusanya watu hao.[3]

 Historia au stori za paukwa pakawa zaYunan za zamani zilimchora Mwenyeezi Mungu na kuuwakilisha mchoro huo duniani, ambapo kulikuwa kuna aina mbali mbali za waungu wadogo wadogo na wakubwa wakubwa.

[1] Suratul-Hashri Aya ya 22-24

[2] Suratul-Hashri Aya ya 22-24

[3] (rejea safari Peydoyesh, mlango wa 11, namba 22-24).

MWISHO