ADABU ZA KUSOMA QUR_ANI
  • Kichwa: ADABU ZA KUSOMA QUR_ANI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 21:57:13 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

ADABU ZA KUSOMA QUR_ANI.

- Kuihifadhi (kuiweka safi) Qur-ani ni sunna.- Kuwa tohara au (kuwa na udhu), kujitia mafuta mazuri, kuelekea kibla wakati wa kusoma Qur-ani ni sunna.

- Kusoma Qur-ani katika sehemu tukufu, kwa mfano msikitini,au sehemu nyengine tukufu ni suna, na kusoma Qur-ani katika sehemu zisizokuwa nzuri kwa mfano chooni, n.k ni karaha (kunakirihisha).

- Kusoma Qur-ani kwa sauti ya juu ni sunna.

- Kumsalia Mtume Muhammad (s.a.w.w) kabla ya kusoma Qur-ani ni sunna.

- Kusoma Audhu bilahi mina Shayttani rajiymi kabla ya kusoma Qur-ani ni sunna.

- Kusoma Qur-ani kwa lahni ya lugha ya kiarabu na sauti nzuri ni sunna.

- Kusoma Qur-ani kwa usahihi katika herufi zake ni sunna.

- Kusoma Qur-ani kwakutafakari, uangalifu, na kufahamu maana ya aya zake ni sunna.

- Kucheka wakati wa kusoma Qur-ani ni karaha na kunakirihisha.

- Ni sunna wakati inaposomwa Qur-ani wasikilizaji wanyamaze kimya.

- Kukata kusoma Qur-ani, au kuzungumza wakati unaposoma Qur-ani kunakirihisha.

Hivi unaelewa kwamba herufi za lugha ya kiarabu ni herufi ishirini na nane, na herufi zote hizo zimejikusanyaka katika aya mbili za Qur-ani,aya hizo ni hizi zifuatazo:-

1- Aya ya mwisho ya suratul- fat-ha.

2- Baina ya aya ya 145 hadi 155ya Suratul-al-imrani.

Suala : tafuta aya mbili hizi na baadae uziandike.

HUKUMU ZA KISHERIA ZA KUIHIFADHI NA KUITUKUZA QUR_ANI

MAULAMAA WOTE WAMEWAFIKIANA KATIKA MAMBO MATANO KATIKA KUITUKUZA QUR_ANI.

1- Kumeharamishwa kutia najisi katika kurasa (waraka) au hati za Qur-ani, ambapo Qur-ani itaingia najisi ni lazima itoharishwe kwa kutiliwa maji.

2- Kumeharamishwa kuweka Qur-ani katika najisi, hata itakapokuwa najisi hiyo imeshakauka. Mfano wa najisi hizo ni:-

Damu, mkojo, maiti, manii, kiwiliwili cha mtu kafiri, kinyesi, mbwa, nguruwe, ulevi n.k. najisi hizo zinajulikana kwa jina la najisi za dhati.

3-Kumeharamishwa kuandika Qur-ani (hata kama ni herufi moja) kwa wino ulio na najisi, basi pindi itakapokuwa mtu ataandika Qur-ani kwa wino ulio na najisi ni lazima aitoharishe Qur-ani hiyo kwa kutumia maji au kwa kitu chochote kile kinachoweza kuitoharisha.

4- Pindi itakapokuwa kurasa (karatasi) ya Qur-ani au karatasi ambayo ndani yake mna jina la Mwenyeezi Mungu (s.w), Mtume (s.a.w.w),au jina la Imam (a.s) imeanguka chooni basi ni lazima kuitoa karatasi hiyo hata kama kutakuwa na mashaka makubwa, na baadae kuitoharisha kwa maji, ama itakapokuwa hakuna uwezekano wa wa kwenda ….kuitoa basi ni lazima upatikane uhakika na yakini kuwa karatasi hiyo imegeuka na kuwa udongo.

5- Ni jambo lililo la lazima kwa waislamu kutompa mtu kafiri Qur-ani, na kama tukiona kama Qur-ani iko mikonono mwa mtu kafiri ni lazima tufanye jitihada za kuichukuwa Qur-ani hiyo.

6- Kumeharamishwa kwa mtu asie na udhu kugusa maandishi ya Qur-ani, majina ya Mitume au majina ya Maimamu, kugusa huko inawezekana ikawa kwa mkono au kiungo chochote kile cha mwanaadamu.

7- Kusoma Qur-ani kwa makosa na kwa makusudi katika mwezi wa ramadhani kunabatilisha funga na mwenye kufanya hivyo inamuwajibikia yeye kutoa kafara.

8- Kumeharamishwa kwa mtu asie na udhu kugusa jina la Mwenyeezi Mungu lililoandikwa kwa hati za aina zozote, au kwa lugha yoyote.

9- Kumeharamishwa kwa mtu asie na udhu, au mwenye hadathi (najisi) kugusa Qur-ani au jina la Mwenyeezi Mungu lililoandikwa kwa hati za aina zozote zile.

10- Kumeharamishwa kwa mtu mwenye janaba, au mwenye hedhi kusoma sura tukufu hata kama itakuwa aya moja,  -sura tukufu ni sura ambazo mtu anaposoma au anaposikiliza zinaposomwa ni lazima aende sujudu- .

Ni sura nne ambazo zinaposomwa ni lazima mtu aende sijda, kila sura moja miongoni mwa sura nne hizo kuna aya moja ya sijda, basi pindi mtu atakaposoma au kusikiliza sura hizo baada ya kumaliza kuisoma aya ambayo ina sijda ndani yake ni lazima asujudu, ama pindi itakapokuwa mtu huyo amesahau wakati wowote atakapokumbuka ni lazima aikidhi sijda hiyo na kusujudu.

Sura hizo nne zinazojulikana kuwa ni sura tukufu ni hizi zifuatazo:-

1- Sura ya 32, surat sajda aya ya 15.

2- Sura ya 41, surat fusillat aya ya 37.

3- Sura ya 53, surat najm aya ya mwisho.

4- Sura ya 96, surat Alaq aya ya mwisho.

MWISHO