UUMBWAJI WA MBINGU NA ARDHI
  • Kichwa: UUMBWAJI WA MBINGU NA ARDHI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 22:28:55 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
UUMBWAJI WA MBINGU NA ARDHI
Mwenyeezi Mungu Mtukufu katika suratun Nisaa aya ya 131- 134 anasema:-
وَللّهِ مَا فِى السَّمَاوَاتِ وَمَا فِى الاَرْضِ وَلَقَدْ وَصَّيْنَا الَّذِينَ اُوتُواْ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَإِيَّاكُمْ اَنِ اتَّقُواْ اللّهَ وَإِن تَكْفُرُواْ فَإِنَّ لِلّهِ مَا فِى السَّمَاوَاتِ وَمَا فِى الاَرْضِ وَكَانَ اللّهُ غَنِيّاً حَمِيدا وَلِلّهِ مَا فِى السَّمَاوَاتِ وَمَا فِى الاَرْضِ وَكَفَي بِاللهِ وَكِيلاً . إِن يَشَاْ يُذْهِبْكُمْ اَيُّهَا النَّاسُ وَيَاْتِ بِآخَرِينَ وَكَانَ اللّهُ عَلـٰي ذٰلِكَ قَدِيرا. مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ الدُّنْيَا فَعِندَ اللهِ ثَوَابُ الدُّنْيَا وَالآخِرَةِوَكَانَ اللّهُ سَمِيعاً بَصِيرا

Maana ya Aya hizo tukufu ni:-
Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote viliomo katik mbingu na viliomo katika dunia. Na kwa hakika tuliwausia walio pewa Kitabu kabla yenu,na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu. Na mkikataa, basi ni vya Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha, na Msifiwa. Na ni vya Mwenyezi Mungu viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mlinzi. Akitaka atakuondoeni, enyi watu! Na awalete wengineo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa hayo.
Anaye taka malipo ya dunia, basi kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.

Maaelezo kuhusiana na Aya 131 – 134 surat Nisaa.
Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini.
Ndani ya Qur-ani kuna Aya zilizo kaririwa. Hapa  tutazungumzia kukaririka kwenye Aya hasa hii , kwa sababu ni Aya iliyotajwa na kurudiwa zaidi katika Qur'an . Kisha tutadokeza kukaririka kwa namna maalum ambayo imetajwa kwa kunakiliwa mara mbili katika Aya moja na kurudiwa mara ya tatu katika Aya inayoifuatia moja kwa moja bila ya kuweko kati kitu kingine.
Ama sababu za kukaririka kwake kwa ujumla ni kwamba maudhui yake ni ulimwengu ambao pamoja na vilivyomo ndani yake unatolea dalili kuwapo Mwenyezi Mungu na sifa zake; kama elimu, uweza, matakwa na hekima. Ni dalili inayokusanya aina za dalili zote na vyenye kutolewa dalili. Kwa hiyo kukumbuka Aya hii ni kukumbuka kuwapo Mwenyezi Mungu na utukufu wake.
Ama kutajwa kwake hapa mara tatu, ni ishara ya faida tatu:
Kwanza: Mwenyezi Mungu katika Aya iliyotangulia amesema: "… Atamtosheleza kila mmoja kwa wasaa wake" Kwa hiyo dalili hii imenasibiana na wasaa huu kuwa ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini.
Pili: Amesema: Kama mkikufuru basi ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini.
Yaani yeye hamhitaji mwenye kukufuru kwa sababu vilivyomo mbinguni na ardhini ni vyake.
Tatu: Amesema Mwenyezi Mungu: Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, na Mwenyezi Mungu atosha kuwa mlinzi. Akitaka atawaondelea mbali, enyi watu na alete wengine.
Makusudio ni kwamba Yeye ni muweza wa kuwamaliza waasi na kuwaleta watiifu; kwa sababu ni vyake vilivyomo mbinguni na ardhini.
Kwa hiyo kila moja katika mara hizo tatu ina sababu yake na kukutanishwa na faida mpya.
Anayetaka malipo ya duniani, basi yako kwa Mwenyezi Mungu malipo ya duniani na akhera.
Yaani malipo ya duniani na akhera yanawezekana kupatikana pamoja na imani na takua. Mwenye kudhani kuwa malipo ya duniani hayawi pamoja na takua, basi huyo amekosea. Kwa sababu hakuna kitu chochote kinachotengeneza vizuri maisha ya hapa duniani ila kitakuwa kinakubaliwa na dini bali kinaamrishwa na kuhimizwa na hiyo dini, lakini kwa sharti moja tu; kuwa kufanikiwa kwake kusiwe ni uovu kwa mwingine na utukufu wake usiwe ni utwevu wa mwingine.
Kwa hivyo malipo ya duniani na akhera hayagongani; isipokuwa kugongana kunatokea baina ya dhulma na malipo ya akhera -baina ya ghushi, hadaa na unyang'anyi na vilevile radhi za Mwenyezi Mungu, neema zake na pepo yake.
 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاء لِلّهِ وَلَوْ عَلَى أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالأَقْرَبِينَ إِن يَكُنْ غَنِيًّا أَوْ فَقَيرًا فَاللّهُ أَوْلَى بِهِمَا فَلاَ تَتَّبِعُواْ الْهَوَى أَن تَعْدِلُواْ وَإِن تَلْوُواْ أَوْ تُعْرِضُواْ فَإِنَّ اللّهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا[1]
Enyi mlioamini! Kuweni imara na uadilifu mtoao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ijapokuwa ni juu ya nafsi zenu au wazazi wawili na jamaa wa karibu. Akiwa ni tajiri au fukara basi Mwenyezi Mungu anawastahiki zaidi. Basi msifuate hawaa ili mfanye uadilifu.
Na mkiupotoa au mkaachana nao basi Mwenyezi Mungu ana habari ya myatendayo.
 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ آمِنُواْ بِاللّهِ وَرَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي نَزَّلَ عَلَى رَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِيَ أَنزَلَ مِن قَبْلُ وَمَن يَكْفُرْ بِاللّهِ وَمَلاَئِكَتِهِ وَكُتُبِهِ وَرُسُلِهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلاَلاً بَعِيدًا[2]
Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Akhera, basi huyo amekwisha potelea mbali.

Maelezo kuhusiana na Aya Na hii ni moja katika aya nyingi zinazowakataza waislamu kuwaitakidi wanaojidai Utume baada nabii Muhammad (s.a.w.w),Hao ni makafiri, na wanaoitakidi ni makafiri vile vile, waiislamu wote juu yao kufuata Qur-ani na hadithi za Mtume.

Na zote zimekwisha kusema kuwa itikadi hiyo ni ukafiri, na kafiri ni wa motoni milele. Juu yetu sisi katika kuwajibu wapotezi hao wakituonyesha ya uwongo wao, tuwaonyeshe Aya hizi za Qur-ani, hatutaacha maneno ua Qur-ani kwa ajili ya maneno ya fulani, kwa kusema kwao Shekh fulani kasema….” Ni uwongo tu huo, Hakuwashindi watu hao kuwasingizia mashekhe kuwa shekhe kasema hivi na hali ya kuwa ni uwongo kabisa, ni uzushi tu wanaowazulia, Qur-ani yote inasema “ min qablika” waliopewa Utume kabla ya Nabii Muhammad (s.a.w.w) ndio Mitume wa haki sio wanaojisingizia baada ya kuja  Nabii Muhammad.

[1] Surat Nisaa Aya ya 135

[2] Surat Nisaa aya ya 136


MWISHO