BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
KUDHIHIRIKA KWA QUDURA YA MOLA
Mwenyeezi Mungu Mtukufu Mwenye uwezo na qudra ameiumba dunia kutokana na nidhamu maalumu. Na kwa sababu hiyo basi anawapa jawabu kaumu ya Mayahudi kwa kusema:-
وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللهِ مَغْلُولَةٌ غُلَّتْ اَيْدِيهِمْ وَلُعِنُواْ بِمَا قَالُواْ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيراً مِّنْهُم مَّا اُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَاناً وَكُفْراً وَاَلْقَيْنَا بَيْنَهُمُ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاء إِلَي يَوْمِ الْقِيَامَةِ كُلَّمَا اَوْقَدُواْ نَاراً لِّلْحَرْبِ اَطْفَاَهَا اللّهُ وَيَسْعَوْنَ فِى الاَرْضِ فَسَاداً وَاللّهُ لاَ يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ[1]
Na Mayahudi walisema: Mkono wa Mwenyezi Mungu umefumba. Mikono yao ndiyo iliyo fumba, na wamelaaniwa kwa sababu ya waliyo yasema. Bali mikono yake iwazi. Hutoa apendavyo. Kwa yakini yaliyo teremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi yatawazidisha wengi katika wao uasi na kufuru. Na Sisi tumewatilia uadui na chuki baina yao mpaka Siku ya Kiyama. Kila mara wanapo washa moto wa vita, Mwenyezi Mungu anauzima. Na wanajitahidi kuleta uharibifu katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu hawapendi waharibifu.
Njia inayodhihirisha qudra Ya Mwenyeezi Mungu katika nidhamu nzuri na iliyo bora imegawika katika njia mbili, nazo ni:-
1- تدریجی (kuumba kidogo kidogo). – dunia ya uumbaji-.
دفعی-2 (kuumba mara moja). – dunia ya maamrisho-.
Mwenyeezi Mungu akielezea uumbaji wa kidogo kidogo anasema:-
إِنَّ رَبَّكُمُ اللّهُ الَّذِى خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالاَرْضَ فِى سِتَّةِ اَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَي عَلـٰي الْعَرْشِ يُدَبِّرُ الاَمْرَ مَا مِن شَفِيعٍ إِلاَّ مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ذٰلِكُمُ اللّهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ اَفَلاَ تَذَكَّرُونَ[2]
Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake,anaendesha mambo yote. Hapana mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?
Na alipoelezea kuhusu uumbaji wa mara moja wa Nabii Issa (a.s) anasema:-
قَالَتْ رَبِّ اَنَّي يَكُونُ لِى وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِى بَشَرٌ قَالَ كَذٰلِكِ اللّهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ إِذَا قَضَي اَمْراً فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ[3]
Maryamu akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanaadamu? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo,Mwenyezi Mungu huumba apendacho. Anapo hukumu jambo, huliambia: Kuwa! Likawa.
Kudhihirika kwa qudra isiyo mpaka ya Mwenyeezi Mungu kwa njia ya mara moja ni alama inayowajalibisha wanaadamu kinadharia na kupata uhakika wa rehema kutoka kwake Allah (s.w).
Kama vile anavyosema Mwenyeezi Mungu kuhusiana na uumbaji wa nabii Issa (a.s).
قَالَ كَذٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا وَكَانَ اَمْراً مَّقْضِيّاً[4]
(Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.
Vile vile Kudhihirika kwa qudra isiyo mpaka ya Mwenyeezi Mungu kwa njia ya mara moja, imewafanya madhalimu na watu wenye kibri kuogopa na kuhisi kuwa hawako katika amani, kama vile anavyosema Allah (s.w).
وَمَا اَمْرُنَا إِلاَّ وَاحِدَةٌ كَلَمْحٍ بِالْبَصَرِ . وَلَقَدْ اَهْلَكْنَا اَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ[5]
Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho. Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka?.
[1] Surat Maidah aya ya 64
[2] Surat Yunus Aya ya 3
[3] Surat Al-imrani Aya ya 47
[4] Surat maryam aya ya 21
[5] Surat Al-Qamar Aya ya 50-51
MWISHO