NYENZO ZA ELIMU YA MWENYEEZI MUNGU
  • Kichwa: NYENZO ZA ELIMU YA MWENYEEZI MUNGU
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 22:10:18 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

NYENZO ZA ELIMU YA MWENYEEZI MUNGU

Kuwepo kwa Mwenyeezi Mungu ni uhakika usiopingika, Mwenyeezi Mungu Mtukufu ametakasika na kila kitu, Yeye hana jinsia yoyote yaani (si mwanamke wala si mwanamme), lakini ili wanaadamu waweze kuelewa na kufahamu nyenzo tofauti zinazohusiana na elimu ya Mwenyeezi Mungu wanatakiwa waifahamu Qur-ani kwa vizuri, Qur-ani tukufu imetumia lafdhi (maneno) yanayomaanisha hisia, kwa mfano, kusikia , kuona… katika kumsifu na kumtakasa Mwenyeezi Mungu,Kwa mfano, ilipoelezewa kuhusiana na elimu ya Mwenyeezi Mungu ya kwamba Yeye anajua na anasikia kila kitu limetumiwa neno (سمیع) yaani anasikia, kama pale hadharati Zakariyya (a.s) alipokuwa akimuomba na kumtakasa Mola wake, kwa kusema:-

هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ قَالَ رَبِّ هَبْ لِى مِن لَّدُنْكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاء[1]

Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi.

Maelezo kuhusiana na Aya

Nabii Zakariyya kuona karama zile aliona naye aombe afanyiwe muujiza wa kuzaa, hali ya kuwa keshapindukia siku za kuzaa, na mkewe pia kapindukia. Akamzaa Nabii Yahya (a.s). Na kwa ajili ya kuelezea kuwa Mwenyeezi Mungu ana elimu na anajua matendo yote yanayofanywa na wanaadamu ikiwa watayafanya kidhahiri au kwa kujificha limetumiwa neno (بصیر) yaani ni mwenye kuona, kama pale aliposema:-

لَن تَنفَعَكُمْ اَرْحَامُكُمْ وَلاَ اَوْلاَدُكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَفْصِلُ بَيْنَكُمْ وَاللهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ[2]

Hawatakufaeni jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.

هُوَ الَّذِى خَلَقَكُمْ فَمِنكُمْ كَافِرٌ وَمِنكُم مُّؤْمِنٌ وَاللهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ[3]

Yeye ndiye aliye kuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.

Na pale alipoelezea kuhusu elimu ya Mwenyeezi Mungu ya kuwa Yeye anajua yote ya ylimwenguni ambayo wanaadamu hawawezi kuyaona ametumia neno (لطیف خبیر)  kama pale Luqmani aliposema kuwaambia mtoto wake:-

يَا بُنَيَّ إِنَّهَا إِن تَكُ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ فَتَكُن فِى صَخْرَةٍ اَوْ فِى السَّمَاوَاتِ اَوْ فِى الاَرْضِ يَاْتِ بِهَا اللهُ إِنَّ اللهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ[4]

Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyo fichika, Mwenye khabari za yote.

Udogo wa khardali ni kama mawele.

Maelezo kwa ufupi kuhusiana na somo lililopita.

-Elimu ya Mwenyeezi Mungu, dhati ya Mwenyeezi Mungu yote hayo yanathibitisha na kuhakikisha nidhamu ya ulimwengu aliyoumba Mwenyeezi Mungu.

- Mwenyeezi Mungu ndiye muumbaji wa vitu vyote ulimwenguni, na kuwepo hesabu ya malipo kutokana na yale ambayo wanaadaamu wameyatenda inathibitisha utukufu wa elimu ya Mwenyeezi Mungu.

- elimu ya Mwenyeezi Mungu iko katika matabaka mbali mbali, elimu ambayo imekusnya elimu ya dhati ya Mwenyeezi Mungu, ufalme wake, na matendo yote anayoyafanya mwanaadamu.

Masuala

 1-Neno elimu lina maana gani?,

2- Elezea tofauti baina ya elimu ya Mwenyeezi mungu na elimu ya viumbe vyote duniani.

3- Kwa kuzingatia Aya tukufu zilizotajwa hapo nyuma elezea mpaka na kiwango cha elimu ya Mwenyeezi Mungu.

4- Kwa kuzingatia hesabu ya malipo siku ya Kiama vipi unaweza ukatoa dalili na kuthibitisha elimu ya Mwenyeezi Mungu?

5- Maneno haya yana maana gani ? (ام الکتاب) و(لوح محو و اثبات)

6- Elezea tabaka za elimu ya Mwenyeezi Mungu.

7- Kwa nini katika Qur-ani kumetumiwa sifa (maneno) kama:-

Anasikia, au anaona katika kumsifu na kumtakasa Mwenyeezi Mungu?

Maelezo ya matini (Rejea kitabu cha tafsiri almiyzani, juzuu ya 11 Aya ya 39 ya Surat Araad).

[1] Surat al-Imrani aya ya 38

[2] Surat Mumtahina aya ya 3

[3] Surat Taghabun Aya ya 2

[4] Surat Luqman aya ya 16

MWISHO