MUUJIZA WA QUR_ANI
  • Kichwa: MUUJIZA WA QUR_ANI
  • mwandishi: DOCTOR SAYYID RIDHA MUADAB
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 10:43:53 4-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

MUUJIZA WA QUR_ANI

UTANGULIZI

Miongoni mwa mambo muhimu yaliyoelezewa ndani ya Qur-ani ni muujiza wa Qur-ani unaoshuhudiwa katika Kitabu hicho kitukufu, katika zama zilizopita hadi zama zetu za sasa hivi kuna Maulamaa, na Wafasiri wengi wa Qur-ani wanaofanya jitihada ili wauwelewe kwa unadni zaidi ule muujiza wa Qur-ani uliomo ndani ya Kitabu hiki Kitukufu.

Katika maandishi haya yafuatayo kwanza kabisa tutaelezea kuhusiana na muujiza wa Qur-ani, na ili kufafanua zaidi kuhusiana na maudhui hayo basi kwanza kabisa tutafafanua (definition), maana ya muujiza, na zaidi tutaelemea kwa kufafanua kwa ufupi yale yanayohusiana na muujiza kwa kuelezea nadhari za Maimamu (a.s), na Maulamaa wa dini ya kiislamu.

Na kwa kuendelea tutaelezea njia tofauti zinazothibitisha muujiza wa Qur-ani, ijapokuwa hakuna shaka kwamba njia moja ya kuthibitisha muujiza wa Qur-ani inaweza ikamkanaisha mtu yoyote yule, hata kwa wale wataalamu wa kilugha na wale waliokuwa sio wafuasi wa waislamu wala sio wafuasi wa dini ya Kiislamu, lakini ili kuthibitisha zaidi tutazielezea njia hizo kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea muujiza wa Qur-ani uonekane kwa uwazi zaidi.

Kitabu hicho ambacho sasa hivi kiko mikononi mwenu ni kitabu ambacho kinaelezea kuhusu muujiza wa Qur-ani, na ndiyo kwanza kimesahihishwa tena kwa mara ya pili ili kitolewe chapa kwa mara ya pili na kitengo kinachopanga program za kuandika matini za masomo kwa wanafunzi wanaojifunza elimu ya kiislamu chini ya kitengo kikuu cha elimu ya kiislamu, tunategemea kwamba yale yaliyomo katika kitabu hicho ambayo yanahusiana na (muujiza wa Qur-ani) yatawasaidia na kuwafaidisha wanafunzi ambao wanajishughulisha na masomo katika kitengo hicho, au hata kwa wanafunzi ambao wanajifunza elimu ya kiislamu katika vitengo vyengine mbali mbali duniani.

Na mwisho kabisa nawashukuru wafanyakazi wote waliojitahidi kwa kushirikiana ili kufanikisha lengo lao la kutaka kutaka kuwaelezea watu kuhusiana na muujiza wa Qur-ani.

Miongoni mwa wafanyakazi hao ni:-

Mheshimiwa ustadh Hujatul-islamu walmuslimina doctor Azu diyni Ridha Nizad (yeye ni mkuu wa kupanga program na kuandika matini za masomo kwa wanafunzi). Vile vile nawashukuru viongozi wote walioshughulika katika kukichapisha kitabu hiki chini ya kitengo kikuu cha kiislamu. Na tunamuomba Mwenyeezi Mungu awape tawfiq watu hao kuendelea na kazi yao hiyo ya kusambaza mafunzo ya elimu ya kiislamu.

Na mwisho kabisa nawaomba walimu ambao watawafundisha wanafunzi yale yaliyoelezewa katika kitabu hiki pindi watakapoona kunahitajia masahihisho au kutowa nadharia zao basi wasisite kuwa pamoja na sisi na sisi tutafaidika kwa kuona nadharia hizo.

 Sayyid Ridha Muadab 1386.

UMUHIMU WA MUUJIZA WA QUR_ANI

Umuhimu na madhumuni ya muujiza wa Qur-ani, ni kuwa na imani, yakini, na kusidikisha yale ambayo Mitume mitukufu ya Mwenyezi Mungu waliyokuja nayo, inawezekana baadhi ya watu wakawa hawana ulazima wa kuletewa muujiza, kwani watu kama hao hukubali ujumbe waliyokuja nayo Mitume, na huikubali na kuisadikisha Mitume ya Mwenyeezi Mungu kwa yale waliyokuja nayo, kwani watu hao wamezisafisha nyoyo zao kwa kuyakubali yale ambayo Mola wao na Mitume yao imewaamrisha, watu kama hao huwa na kauli za kweli nyoyoni mwao (dhahiri na batini), na kutokana na ukweli, amana na kusidikisha yele madai ambayo Mitume wamekuja nayo basi watu hao hawana ulazima wa kuletewa miujiza, kwani watu hao wametii na kuamini yale waliyokuja nayo Mitume yao. watu hao huamini kwa kuwa wazi au bila ya kuwepo wazi, kujuwa au kutojuwa hekima ya kuamini kwao huko, nyoyo za watu hao zimesafika kwa sababu wana yakini na yale ambayo Mola wao amewaamrisha.

Kwa upande mwengine watu wote duniani wanahitilafiana, baadhi yao hawawezi kukubali maoni ya mtu kwa urahisi, hadi pale ambapo wanapopata dalili zitakazowakinaisha, na kuwawekea kwa uwazi yale yanayowatatiza, watu kama hao pindi ambapo watakuwa hawajapata yakini na kusidikisha kwamba Mitume imekuja kwa amri ya Mwenyeezi Mungu basi haitowawajibikia wao kutii amri walizokujanazo Mitume hiyo, na kutokana na sababu hizo basi yule mtu anyekuja na akadai kuwa yeye ni Mtume ni lazima aje na miujiza ili kujenga uhusiano na watu pamoja na dunia ili kuwapa yakini, kuwathibitishia na kuwawekea wazi wale watu ambao ni vigumu kwao kuamini kwa wepesi, kwa hiyo pindi Mitume itakapokuja na miujiza kutasidikisha ya kwamba wameteuliwa na Mwenyeezi Mungu na wamekuja kwa amri ya Mola wao.

Kusidikisha yale waliyokujanayo Mitume kwa watu kama hawa ni jambo muhimu na lazima, na zaidi kwa wale ambao wanafanya uadui juu ya dini ya kiilamu na wanahalifu amri ya Mwenyeezi Mungu na yale waliyokujanayo Mitume yake na hawako tayari kuwaamini, kwa hiyo kila Mtume ili kukamilisha hoja zake ni lazima aje na muujiza, na tunathibitisha hayo kwa kauli ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu pale aliposema:-

قَالَ اَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَيْءٍ مُّبِينٍ[1]

pale Nabii Mussa (a.s) alipomuelekea firauni, Akasema:-

 “Je! Ijapokuwa nitakuletea kitu kilicho wazi, (hoja zilizo wazi za kuonyesha ukweli wa Utume wangu)?” hivi kweli hutoamini?.

Firauni akasema kumwambia Mussa (a.s) “ikiwa unasema kweli basi lete huo muujiza wako”, wakati huo basi Mussa (a.s) akatupa fimbo yake chini na mara ikageuka na kuwa nyoka. (nyoka huyo akawameza nyoka wa wataalamu wa kichawi waliofanya uchawi wao ili kukabiliana na Nabii Mussa (a.s)) . Na mara akatia mkono wake kwapani na baadae kuutowa na watizamaji waliushuhudia mkono huo kuwa ni mweupe.

Katika kipindi chote cha tarehe Mitume ilikuja na miujiza ili kuthibitisha ujumbe waliokujanao kutoka kwa Mwenyeezi Mungu, kwa sababu kama wasingelikuja na miujiza watu wasingeliamini rehema za Mwenyeezi Mungu na yale waliyokuja nayo.

Ulamaa maarufu Seikh Alama Tabatabai kuhusiana na miujiza anasema:-

“Mitume imekuja na miujiza ili kuthibitisha na kusidikisha ujumbe waliokuja nao Mitume hiyo, na wala sio kwa ajili ya kuthibitisha maarifa na rehema zake   Mwenyeezi Mungu[2].

Hajj Nasiru dini Tuwsiy na yeye anasema:-

" طريق معرفة صدقه, ظهور المعجزة علي يده"[3].

Njia waliokuja nazo Mitume ili kusidikisha madai yao ni miujiza.

[1] Shuaraa 30

[2] Almiyzani fiy tafsiril-qur-ani, juzuu ya 1, ukurasa wa 6-82

[3] Kashfu-l-muradi fiy sharhi tajriyd al-iitikadi, ukurasa wa 275.