MAYAHUDI HAWAMSADIKI MTUME
  • Kichwa: MAYAHUDI HAWAMSADIKI MTUME
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 22:37:1 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

MAYAHUDI HAWAMSADIKI MTUME (S.A.W.W)

MAYAHUDI HAWAISADIKI QUR_ANI TAKATIFU WALA HAWAMSADIKI MTUME (S.A.W.W).

Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:-

وَلَمَّا جَاءهُمْ كِتَابٌ مِّنْ عِندِ اللهِ مُصَدِّقٌ لِّمَا مَعَهُمْ وَكَانُواْ مِن قَبْلُ يَسْتَفْتِحُونَ عَلـٰي الَّذِينَ كَفَرُواْ فَلَمَّا جَاءهُم مَّا عَرَفُواْ كَفَرُواْ بِهِ فَلَعْنَةُ الله عَلـٰي الْكَافِرِينَ[1]

Na kilipo wajia Kitabu kitokacho kwa Mwenyezi Mungu kinacho thibitisha waliyo nayo - na wao walikuwa wakitafutia ushindi kuwashinda makafiri - yalipo wajia yale waliyo kuwa wakiyajua waliyakanusha. Basi laana ya Mwenyezi Mungu juu ya wakanushao!.

 Maelezo kuhusiana na Aya

Kabla ya kuja Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Mayahudi walikuwa wakiwapa khabari Waarabu kuwa karibuni atadhihiria Mtume[2].

Ama kusema kuwa hao Mayahudi walikuwa wakiomba kwa jaha ya Mtume, na wakishinda maadui zao kuwa ndio muradi wa Aya hii – maneno haya hawaakuyasema wale wafasiri wa mwanzo kabisa (salaf) wenye kutegemewa, kama Imam Ibn Jarir[3] Wala hawakuitaja vile vile wale wafasiri wanaotegemea hadithi sahihi za Mtume.

Imekuja katika qur-ani na hadithi sahihi kuombwa Mwenyeezi Mungu kwa majina yake, basi tufupizike na alivyotuambia Mwenyeezi mungu na Mtume wake. Wallahi hatutakuwa watovu kwa kufupizika juu ya haya.

Mwenyeezi anasema kuwaambia Mayahudi:-

لْ مَن كَانَ عَدُوّاً لِّجِبْرِيلَ فَإِنَّهُ نَزَّلَهُ عَلـٰي قَلْبِكَ بِإِذْنِ اللهِ مُصَدِّقاً لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَهُدًى وَبُشْرَي لِلْمُؤْمِنِينَ[4]

Sema: “ Anayemfanyia ushinde jibril (kwa kuwa ndiye aliyemletea Utume Nabii Muhammad (s.a.w.w) asiwapelekee Mayahudi, (ni bure hana kosa jibril), hakika yeye ameiteremsha qur-ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyeezi Mungu, (sio kufanya kwa kupendelea kwake); (Qur-ani), inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake, na ni uwongozi wa habari njema kwa wanaoamini.

Mayahudi katika hila zao za kumkataa Mtume Muhammad walimuuliza:-

“Malaika gani anayekuletea wahyi? Mtume akasema:-

“Jibriyl”. Wakasema: “Lo! Huyu adui yetu, hatumtaki. Lau kama angelikuwa Malaika mwengine ndiye anayekuletea wahyi tungelikufuata.” Basi Mwenyeezi mungu anawajibu hivi:-

[1] Suratul-Baqarah Aya ya 89

[2] Tazama marejezo 18: 15-19, na yohana 1:25

[3] Tazama juzuu 2 iliyoshereheshwa na Shakir, ukurasa wa 332-335 hutaiona tafsiri hiyo.

[4]Suratul baqara aya ya 97

MWISHO