HEKIMA ZA MWENYEEZI MUNGU
  • Kichwa: HEKIMA ZA MWENYEEZI MUNGU
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 9:42:54 13-8-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

* Vipi sifa tukufu za Mwenyeenzi Mungu zinaonesha utukufu wake?.
* Kuzielewa hekima za Mwenyeezi Mungu kuna athari gani katika kukuza na kuimarisha imani za wanaadamu?.
HEKIMA ZA MWENYEENZI MUNGU
Kwa kuangalia uumbaji na utukufu wa Mwenyeenzi Mungu tunashuhudia tofauti ya viumbe wengi duniani, miongoni mwa tofauti hizo ni kama hizi zifuatazo:-
Nguvu, udhaifu, mwanamme, mwanamke, ubora, na kutokuwa bora, maudhi, kheri, shari, faida, hasara n.k.

Ni jambo lililowazi kabisa kwamba pindi mwanaadamu anaposhuhudia tofauti hizo hujiwa na masuala mengi tofauti, na kujiuliza hivi kweli tofauti zote hizo ni alama inayowastaajabisha wanaadamu  kwa kuona nidhamu ya viumbe alivyoviumba Mwenyeenzi Mungu? Na hivi kweli tofauti hizo zinaonesha utukufu wa milki ya Allah (s.w)?
Masuala hayo hujiuliza wanaadamu na viumbe vyote vyenye akili (majini, na malaika) duniani, hii ni kwa sababu kila mwanaadamu anatafuta anataka kujua uhakika wa mambo, natija ya masuala kama haya imesababisha baadhi ya viumbe – yaani kundi la mwanzo tulilolitaja hapo juu yaani (majini).
– kumkufuru Mwenyeenzi Mungu na kupinga uhakika waliouona, - na kundi la pili walimuamini Mola wao na kumtii– (malaika).
Kundi la mwanzo ambalo miongoni mwao na iblisi ambaye alijadiliana na Mwenyeenzi Mungu kuhusiana na uumbaji wa mwanaadamu alidhihirisha kufuru yake, kama vile Qur-ani inaavyosema:-
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلاَئِكَةِ اسْجُدُواْ لآدَمَ فَسَجَدُواْ إِلاَّ إِبْلِيسَ اَبَي وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ[1]
Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri.
Na mfano wa kundi la pili ni Malaika ambao baada ya kuuliza masuala yao kuhusiana na kuumbwa kwa Nabii Adam (a.s) Mwenyeezi Mungu aliwajibu, na wao waliridhika na jawabu ya Mola wao basi waliamini na wakazidi kuimarisha imani yao, walimtii Mola wao na kufuata maamrisho yake, na ndipo wakasema:-
قَالُواْ سُبْحَانَكَ لاَ عِلْمَ لَنَا إِلاَّ مَا عَلَّمْتَنَا إِنَّكَ اَنتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ[2]
Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima.
Basi kitu ambacho kinamsaidia mwanaadamu kupata majibu ya masuala ambayo yanamjia akilini kuhusiana na uumbaji wa dunia ni kujua na kuzifahamu hekima zake Allah (s.w). kwa hiyo katika somo hili tutaelezea baadhi ya hekima za Mwenyeenzi Mungu.
Maana ya neno (hekima).
Maana ya nono hekima ni “ kuelewa uhakika wa mambo bila ya kuwa na ujahili au shaka kuhusiana na uhakika wa mambo hayo”
Asili ya neno (حکمت) ni (حکم) yaani kuzuia kitu kwa sababu ya suluhu, au kuzuia kitu kutokana na dhulma.


(حکیم) Hakim huitwa mtu ambaye anayajua mambo kwa uhakika na ukamilifu, na hufanya mambo kwa ukamilifu na kwa mipango iliyopangwa kwa program maalum.

[1] Suratul-Baqara aya ya 34

[2] Suratul-Baqara Aya ya 32


MWISHO