KUDHUHURU KWA IMAM MAHDI (A.S).
BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
IMEANDIKWA NA NDUGU ZETU WA KIISLAMU.
KUDHUHURU KWA IMAM MAHDI (A.S).
SABABU NA ALAMA ZA KUDHUHURU IMAM MAHDI (A.S).
Kudhihiri kwa Imam kuna sababu na alama maalum na sababu hizo pamoja na alama zinaeleweka kuwa ndio matayarisho ya kuja kwake, tofauti ya vitu hivi
viwili (alama na matayarisho) ni kwamba matayarisho yana athari muhimu katika kudhihiri kwa Imam kiasi ya kwamba yakikamilika matayarisho hayo basi
kudhihiri kwa Imam ni lazima kutokee, na kukosekana kwake kudhihiri kwa Imam hakutotokea, lakini alama za kudhihiri haziathiri kitu chochote katika kudhihiri kwake, bali alama hizo zinasaidia kuelewa umbali na ukaribu wa kudhihiri kwake. Kwa kutokana na tofauti tulizozielezea itakuwa ni rahisi kuelewa ya kwamba matayarisho pamoja na masharti yana umuhimu zaidi kuliko alama za kudhihiri, kwa hiyo basi kabla ya kuzifukuzia alama na kuzifuatilia ni bora zaidi tufuatilie matayarisho na kila mmoja ajitahidi kwa kadri ya uwezo wake katika kuyatekeleza matayarisho hayo, ndio maana mwanzo kabisa tulizielezea shuruti pamoja na matayarisho, na sasa tutazitaja baadhi ya shuruti na matayarisho hayo.
MATAYARISHO YA KUMFANYA ADHUHURU
Kila tokeo katika ulimwengu hutokea kwa kutokana na kauwepo shuruti maalum, na bila ya kupatikana shuruti hizo haliwezi kutokea tokeo hilo kila ardhi haiwezekani kupanda kitu ukitakacho na kila hali ya hewa hainasibiani na kumea kila mmea, mkulima huwa na matarajio ya kupata mavuno mazuri kutokana na ardhi ambayo ina masharti maalumu ambayo ameyataarisha mkulima huyo. Kwa msingi huu basi kila mapinduzi na kila tokeo la kijamii huwa lina fungamano maalumu baina ya tokeo hilo na masharti ya tokeo hilo, kama vile tokeo la mapinduzi ya kiislamu ya Irani ambalo limetokea chini ya vitangulizi maalumu vilivyotangulia kabla yake, ambavyo vimesababisha kupatikana ushindi. Mapinduzi ya Imam Mahdi ya kilimwengu ambayo ni badiliko kubwa katika ulimwengu,nalo linafuata misingi hiyo hiyo, na bila ya kupatikana kwa masharti na matayarisho tokeo hio haliwezi kutokea.
Makusudio ya maelezo haya ni kwamba kusije akatokea mtu akafahamu kuwa Mapinduzi ya Imam Mahdi (a.s) yatatokea kimiujiza na bila sababu na matayarisho maalumu. Lakini tukitupia macho mafunzo ya Qur-ani ka kauli za Maimamu (a.s) zinasema hivi:-
"Matakwa ya Mwenyeezi Mungu hutendeka kwa kupitia sababu za kikawaida na sio kimiujiza.
Imam Sadiq (a.s) anasema: "Mwenye enzi Mungu hataki kutenda kitu bila ya kukamilika sababu zake[1]"
Imenukuliwa kutoka kwa Imam Baaqir (a.s) kua mtu mmoja alimwambia Imam (a.s) "watu wanasema kua atapodhihiri Imam Mahdi (a.s) mambo yato yatakwenda kama yeye atakavyo, Imam akamjibu, "katu haiwezekani kua hivyo, naapa kwa Mola wangu kua ingelikuwa Mwnyeezi Mungu ameyapanga mambo yaende hivyo, basi Mtume (s.a.w) angelikua ndiye mtu wa mwanzo wa kuyaendesha mambo kama vile atakavyo.
Lakini mazungumzo hayo yaliyopita hayamaanishi kuwa msaada wa Mwenyeezi Mungu hautakuwepo katika zama za uongozi wa Imam mahdi, lakini yana maana hii ya kwamba kuwepo kwa msaada wa Mwenyeezi Mungu kunahitajia kuwepo kwa shuruti na matayarisho. Kwa hiyo basi mwanzo kabisa tunatakiwa tuyafahamu matayarisho na vitangulizi vya kuja kwake kisha tujitahidi ili kukamilisha matayarisho hayo. Matayarisho yaliyo muhimu katika Mapinduzi ya Imam Mahdi ni mambo manne, na kila moja kati ya hayo inabidi tulifanyie utafiti peke yake.
A) UPANGAJI WA MIPANGO
Ni jambo la wazi kabisa kwamba mageuzi ya aina yeyote ile yanayohusiana na matengenezo yanahitajia mipango ya aina mbili:-
1. Mpango wa kupambana na matatizo yasiyo ya kawaida kwa kupitia uongozi bora wenye nguvu.
2. Kanuni zilizo kamili na zenye kunasibiana na mahitajio yote ya jamii, kanuni hizo zinatakiwa ndani yake ziwe zimekusanya haki za mtu mmoja mmoja pamoja na haki za kijamii kwa ujumla, ndani ya nidhamu moja ya Serikali iliyo adilifu na iwe imeichorea jamii yake mistari inayoweza kuikomaza jamii hiyo, na kuikuza katika maendeleo yake.
Mafunzo ya Qur-ani pamoja na hadithi ambavyo vitu viwili hivi ndio uislamu halisi na ndio kanuni iliyo bora na yenye mipango mizuri zaidi, vitu viwili hivi ndio nyenzo kuu zitakazokuwa ndani ya mikono ya Imam, na Imam kwa kupitia vitu viwili hivyo ataendesha Serikali yake, Qur-ani ni kitabu ambacho aya zake kwa ujumla zimetoka kwa Mwenyeezi Mungu. Mola ambaye anaelewa matakwa yote ya mwanaadamu katika maisha yake, yakiwemo matakwa ya kimwili na ya kiroho, kwa hiyo basi Mapinduzi ya kilimwengu ya Imam katika upande wa mipango na kanuni za Serikali itakuwa imepangika vizuri bila ya kifani, na mapinduzi haya huwezi ukafananisha na aina nyengine yeyote ile ya mapinduzi. Dalili ya madai haya ni kwamba ulimwengu wa kileo baada ya kupita majaribio tofauti ya kanuni za wanaadamu umeeleweka wazi udhaifu wa kanuni hizo, na siku baada ya siku watu wanasubiri kanuni kutoka kwa Mwenyeezi Mungu ili ziweze kuendesha ulimwengu huu.
AlwinTaflo ambaye ni mshauri wa wanasiasa wa Kimarekani amefanya juhudi kubwa katika kutaka kutatua matatizo na misokotano iliyoko katika uongozi waleo, na ametoa mtizamo wa Kitecnologia akitarajia kwamba wimbi kubwa la kiteknologia amablo limeingia hivi sasa huwenenda likatatua matatizo yaliyokuweko,ambapo kabla ya wimbi hili ulimwengu ulipitiwa na mawimbi mawili makubwa nayo
1. Wimbi la wakulima (kilimo).
2. Wimbi la viwanda (uzalishaji wa viwandani).
Lakini bado wamagharibi wenyewe wamekubali kuwa wimbi hili la kiteknologia lina matatizo tofauti, na bado halijaweza kutatua matatizo ya ulimwengu.
Aliwin Taflo anasema hivi:-
"Matatizo yaliyomo ndani ya jamii yetu ya kimagharibi bado yanaendelea na kwa kujitokeza mvurugiko wa siku baada ya siku katika jumuia tofauti zenye kushughulikia utamaduni wa viwanda, na zikiwemo katika hali ya mizozano, huku harufu ya kuvurugika kwa tabia ikisikika, natija yake ni kutokea wimbi la kutokuwa na furaha, wakifazaika katika kutafuta mabadiliko, katika kutafuta utatuzi wa mafazaiko haya kumepanmgwa mipango tofauti huku kila mpango ukidaiwa kwamba uataleta mabadiliko, na kuwa mpango huo ndio msingi halisi lakini kila mara mipango na kanuni mpya zilizopangwa ili kutatua matatizo yetu zimeonekana kuwa zinazidisha matatizo yetu, na inasababisha kukata tamaa na kujihisi kuwa tumeshindwa, ambalo jambo hili halitusaidii chochote sisi, hisia hizi katika kila nidhamu ya kidemokrasia ni hatari na kila siku zikienda mbele ile methali ya watu inayoashiria kua kuna mtu anayehitajiwa na jamii atakuja akiwa amepanda farasi mweupe, watu wanakaribiana nayo zaidi (yaani wanahisi kua wanamhitajia mtu huyo). (rejea kitabu kuelekea katika utamaduni mpya).
[1] tazama Mizanil hikma juzu ya tano ukurasa 8166.
MWISHO