SALA NDANI YA QUR_ANI
  • Kichwa: SALA NDANI YA QUR_ANI
  • mwandishi: MAHMUUD JUBEYR
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 16:55:24 3-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

SALA NDANI YA QUR_ANI

Aya hizi zinazofuata zinahusiana na sala gani?

[1] 1: وَإِذَا ضَرَبْتُمْ فِى الاَرْضِ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ اَن تَقْصُرُواْ مِنَ الصَّلاَةِ إِنْ خِفْتُمْ اَن يَفْتِنَكُمُ الَّذِينَ كَفَرُواْ إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُواْ لَكُمْ عَدُوّاً مُّبِينا

Na mnaposafiri katika ardhi, si vibaya kwenu kama mkifupisha Sala; iwapo mnaogopa ya kwamba wale waliokufuru watakutaabisheni. Bila shaka makafiri ni maadui zenu dhahiri.

 2  وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَي اَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَاماً مَّحْمُودا ً[2]:

Na katika usiku jiondoshee usingizi (kidogo) kwa (kusoma) hivyo (Qur-ani ndani ya sala). Hiyo ni (ibada) zaidi kwako. Huwenda Mola wako akakuinua cheo kinachosifika.

 3: يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِى لِلصَّلاَةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَي ذِكْرِ اللهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ[3]

Enyi mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kumtaja Mwenyeezi Mungu na acheni biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua (hivi basi fanyeni).

4: وَاَقِيمُواْ الصَّلاَةَ وَآتُواْ الزَّكَاةَ وَارْكَعُواْ مَعَ الرَّاكِعِينَ[4]

Na simamisheni Sala (Enyi Mayahudi) na toeni Zaka na inameni (yaani rukuuni) pamoja na wanaoinama (yaani kuweni Waislamu).

VIPENGELE VYA SALA NDANI YA QUR_ANI

Aya hizi zifuatazo zinahusiana na sehemu (vipengele) gani ndani ya Qur-ani?

 1 : يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِذَا قُمْتُمْ إِلَي الصَّلاةِ فاغْسِلُواْ وُجُوهَكُمْ وَاَيْدِيَكُمْ إِلَي الْمَرَافِقِ وَامْسَحُواْ بِرُؤُوسِكُمْ وَاَرْجُلَكُمْ إِلَي الْكَعْبَينِ وَإِن كُنتُمْ جُنُباً فَاطَّهَّرُواْ وَإِن كُنتُم مَّرْضَي اَوْ عَلـٰي سَفَرٍ اَوْ جَاء اَحَدٌ مَّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ اَوْ لاَمَسْتُمُ النِّسَاء فَلَمْ تَجِدُواْ مَاء فَتَيَمَّمُواْ صَعِيداً طَيِّباً فَامْسَحُواْ بِوُجُوهِكُمْ وَاَيْدِيكُم مِّنْهُ مَا يُرِيدُ اللّهُ لِيَجْعَلَ عَلَيْكُم مِّنْ حَرَجٍ وَلَـكِن يُرِيدُ لِيُطَهَّرَكُمْ وَلِيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ[5]

Enyi mlioamini! Mnaposimama ili mkasali, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na (mpake) miguu yenu. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmeingiliana na wanawake, na hamkupata maji, basi kusudieni (tayamamuni) udongo (mchanga) ulio safi na kuupaka nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyeezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema Yake juu yenu ili mpate kushukuru.

2:َ[6]  قَدْ نَرَي تَقَلُّبَ وَجْهِكَ فِى السَّمَاء فَلَنُوَلِّيَنَّكَ قِبْلَةً تَرْضَاهَا فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَحَيْثُ مَا كُنتُمْ فَوَلُّواْ وُجُوِهَكُمْ شَطْرَهُ وَإِنَّ الَّذِينَ اُوْتُواْ الْكِتَابَ لَيَعْلَمُونَ اَنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ وَمَا اللّهُ بِغَافِلٍ عَمَّا يَعْمَلُون

Kwa yakini tukiona unavyogeuzageuza uso wako mbinguni. Basi tutakugeuza kwenye Kibla ukipendacho. Basi geuza uso wako upande wa Msikiti Mtakatifu (Al-Kaaba); na popote mnapokuwa zielekezeni nyuso zenu uliko (msikiti huo); na hakika wale waliopewa Kitabu wanajua kwamba hiyo ni haki itokayo kwa Mola wao; na Mwenyeezi Mungu si Mwenye kughafilika na yale wanayoyatenda.    

3: وَرَبَّكَ فَكَبِّر[7]

Na Mola wako umtukuze.

4: يا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ[8]

Enyi mlioamini! (Salini) rukuuni na kusujudu na Mwabuduni Mola wenu na fanyeni mema, ili mpate kufaulu (kufuzu).

5 :وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِى اَسْتَجِبْ لَكُمْ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِى سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ[9]   

Na Mola wenu anasema: “ Niombeni nitakujibuni. Kwa hakika wale wajivunao kufanya ibada yangu, bila shaka wataingia jahanamu wadhalilike.”

 6  إِنَّ اللهَ وَمَلاَئِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلـٰي النَّبِيِّ يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيماً[10]          

Hakika Mwenyeezi Mungu anamteremshia rehema Mtume; na Malaika Wake (wanamuombea dua dua kwa vile vitendo vizuri alivyovifanya). Basi; enyi Waislamu (mliopata neema hii ya kufundishwa haya na Mtume) msalieni (Mtume, muombeni rehema) na muombeeni amani.

 7 : فَسُبْحَانَ اللهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ[11]

Basi mtukuzeni Mwenyeezi Mungu mnapoingia katika nyakati za usiku (kwa kusali Magharibi na Isha) na mnapoingia katika asubuhi (kwa kusali sala ya Alfajiri).

[1]Suratun- Nisaa 101

[2] Asraa 79

[3] Jumua 9

[4]Baqara 43

[5] Maida 6

[6] Baqara144

[7] Mudathir3

[8] Hajj 77

[9] Ghafir 60

[10] Ahzab 56

[11] Ruum 17

MWISHO