DUA KUMAYL
  • Kichwa: DUA KUMAYL
  • mwandishi:
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 18:17:18 1-9-1403

DUA KUMAYL
بسم الله الرحمن الرحيم
Kwa jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
أَللّهُمَّ إِنِّي أَسأَلُكَ بِرحَمتِكَ الَّتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Hakika mimi nakuomba kwa rehema
Zako ambazo zimeenea kila kitu.
وَبِقُوَّتِكَ الَّتِي قَهرْتَ بِها كُلَّ شَيءٍ
Na kwa nguvu Zako ambazo zimetiisha kila kitu,
وَخضَعَ لَها كُلُّ شَيْءٍ ، وَذَلَّ لَها كُلُّ شَيْءٍٍ
na kunyenyekewa ni kila kitu na kudhalilikiwa ni kila kitu.
وَبِجَبَرُوتِكَ الَّتِي غَلَبْتَ بِها كُلَّ شَيْءٍ
na kwa ushindi Wako ambao haulingani na chochote,
وَبعَزَّتِكَ الَّتِي لا يَقُومُ لَها شَيْءٌ
Na kwa uwenyeezi Wako ambao umeshinda kila kitu
وَبِعَظَمَتِكَ الَّتِي مَلاَتْ كُلَّ شَيْءٍ
na kwa ukuu Wako ambao umejaa juu ya kila kitu,
وَبِسُلْطانِكَ الَّذِي عَلا كُلَّ شَيْءٍ
na kwa utawala Wako uliyojuu ya kila kitu.
وَبِوَجْهِكَ الباقِي بَعْدَ فَناءِ كُلِّ شَيْءٍ
Na kwa dhati Yako yenye kudumu baada ya kutoweka kila kitu,
وَبِأَسْمائِكَ الَّتِي ملاَ َتْ أَرْكانَ كُلِّ شَيْءٍ
na kwa majina Yako ambayo yamekusanya misingi ya kila kitu,
وَبِعِلْمِكَ الَّذِي أَحاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ
na kwa ujuzi Wako ambao umedhibiti kila kitu,
وَبِنُورِ وَجْهِكَ الَّذِي أَضأَ لَهُ كُلُّ شَيءٍْ
na kwa nuru ya dhati Yako amabyo kwayo kimeangazia kila kitu.
يا نوُرُ ياقُدُّوسُ
Ewe Nuru! Ewe Mtakatifu!
ياأَوَّلَ الاوَّلِينَ ، وَيا آخِرَ الآخِرينَ
Ewe Mwanzo wa wamwanzo, Ewe Mwisho wa wamwisho.
اللّهُمَّ اغْفِرْ لِيَ الذُّنُوبَ الَّتِي تَهْتِكُ العِصَمَ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Nighofurie dhambi zinazovunja kinga
اللّهُمَّ اغْفِرْ لِيَ الذُّنُوبَ الَّتِي تُنْزِلُ النِّقَمَ
Ewe Mwenyezi Mungu! Nighofurie dhamb izinazo teremkisha mateso.
اللّهُمَّ اغْفِرْ لِيَ الذُّنُوبَ الَّتِي تُغَيِّرُ النِّعَمَ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Nighofurie dhambi zinazo haribu neema.
اللّهُمَّ اغْفِرْ لِيَ الذُّنُوبَ الَّتِي تَحْبِسُ الدُّعأَ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Nighofurie dhambi zinazo zuia dua
اللّهُمَّ اغْفِرْ لِيَ الذُّنُوبَ الَّتِي تّقّّْطع الرَّجّاّءّ
Ewe Mwenyeezi Muu! Nighofurie dhambi zinazo kata matumaini.
اللّهُمَّ اغْفِرْ لِيَ الّذنُوبَ الّتي تُنْزِلُ البَلاَ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Nighofurie dhambi zinazo teremkisha balaa.
اللّهُمَّ اغْفِرْ لِيَ كُلَّ ذَنْبٍ أذْنَبْتُهُ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Nighofurie kila dhambi niliyoitenda
وَكُلَّ خَطِيئَةٍ أَخْطَأْتُها
na kila kosa nililokosea.
اللّهُمَّ إِنِّي أَتَقَرَّبُ إِلَيْكَ بِذِكْرِكَ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Hakika mimi najikurubisha Kwako kwa utajo Wako,
وَاسْتَشفِعُ بِكَ إِلى نَفْسِكَ
na nakuomba shufaa Yako nikielekea Kwako.
وَأَسْأَلُكَ بِجوُدِكَ
Na nakuomba kwa ukarimu Wako
أَنْ تُدْنِيَنِي مِنْ قُرْبِكَ
unisogeze karibu Nawe,
وَأَنْ تُوزِعَنِي شُكْرَكَ،
Unizindue ni kushukuru,
، وأَنْ تُلْهِمَنِي ذِكْرَكَ
Unitie ilhamu ya ukumbusho Wako.
اللّهُمَّ إِنِّي أَسأَلُكَ سُؤالَ خاضِعٍ مُتَذَلِّلٍ خاشِعٍ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Hakika mimi nakuomba ombi la mnyenyekevu, mnyonge, mchaji,
أَنْ تُسامِحَنِي وَتَرْحَمَنِي
nikikusihi Unisamehe na Unihurumie,
وَتَجْعَلَنِي بِقِسَمِكَ راضِياً قانِعاً
Unipe gawio maridhia la kutosheleza
وَفِي جَمِيعِ الاحْوالِ مُتَواضِعاً
na katika hali zote Unipe utulivu.
اللّهُمَّ وَأَسأَلُكَ سُؤالَ مَنِ إِشْتَدَّتْ فاقَتُهُ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Na nakuomba ombi la aliye zongwa ni matakwa yake,
فاقَتُهُ وَأَنْزَلَ بِكَ عِنْدَ الشَّدائِدِ حاجَتَهُ
na haja yake pindi inapo mdhiki akaileta Kwako,
وَعَظُمَ فِيما عِنْدَكَ رَغْبَتُهُ
yakizidi mapenzi yake kwa yaliyo Kwako.
اللّهُمَّ عَظُمَ سُلْطانُكَ وَعَلا مَكانُكَ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Umetukuka utawala Wako, cheo Chako kijuu,
وَخَفِيَ مَكْرُكَ ، وَظَهَرَ أَمْرُك
mipango Yako imefichamana, amri Yako iko wazi,
أَمْرُك وَغَلَبَ قَهْرُكَ ، وَجَرَتْ قُدْرَتُكَ
nguvu Zako zimeshinda, uwezo Wako umetanda,
وَلايُمْكِنُ الفِرارُ مِنْ حُكُومَتِك
na kamwe! Haikimbiliki hukumu Yako.
اللّهُمَّ لا أَجِدُ لِذُنُوبِي غافِراً
Ewe Mwenyeezi Mungu! Simpati wakunighofiria dhambi zangu,
وَلا لِقَبائِحِي ساتِراً
wala wakuyasitiri maovu yangu,
وَلا لِشَيٍْ مِنْ عَمَلِيَ القَبِيحِ بِالحَسَنِ مُبَدِّلاً غَيْرَكَ
wala hakuna wakunibadilishia tendo lolote langu ovu kwa lema, isipokuwa Wewe
لا إِلهَ إِلا أَنْتَ ، سُبْحانَكَ وَبِحَمْدِكَ
Hapana mungu ila Wewe Uliyetakasika Mwenye kusifika,
ظَلَمْتُ نَفْسِي ، وَتَجَرَّأْتُ بِجَهْلِي
nimeidhulumu nafsi yangu, nikijasiri kwa ujahili wangu,
وَسَكَنْتُ إِلى قَدِيمِ ذِكْرِكَ لِي ، وَمَنِّكَ عَلَيَّ
nikijituza kwa kunitangulia kunikumbuka Kwako na kwa wema Wako Unaonifanyia.
اللّهُمَّ مَوْلايَ
Ewe Mwenyeezi Mungu, Mola wangu!
كَمْ مِنْ قَبيحٍ سَتَرْتَهُ
maovu mangapi, Umeyasitiri,
وَكَمْ مِنْ فادِحٍ مِنَ البَلاِ أَقَلْتَهُ
na mazito mangapi, ya balaa Umeyapunguza,
وَكَمْ مِنْ عِثارٍ وَقَيْتَهُ
na mangapi, ya kuangamiza Umeyakinga,
وَكَمْ مِنْ مَكْروُهٍ دَفَعْتَهُ
na mangapi, ya maudhi Umeyazuia,
وَكَمْ مِنْ ثَنأٍ جَمِيلٍ لَسْتُ أَهْلاً لَهُ نَشَرْتَهُ
na sifa ngapi, nzuri sikuwanazo Umezizagaza.
اللّهُمَّ عَظُمَ بَلائِي
Ewe Mwenyeezi Mungu! Balaa zangu zimekuwa kubwa,
وَأَفْرَطَ بِي سُؤُ حالِي
na hali yangu ya uovu imepita mipaka,
وَقَصُرَتْ بِي أَعْمالِي
na mema yangu ni machache.
وَقَعَدَتْ بِي أَغْلالِي
Minyororo yangu imeniweka kitako,
وَحَبَسَنِي عَنْ نَفْعِي بُعْدُ أَمَلِي
na yamenizuia kujinufaisha matamanio yangu yalobaidika.
وَخَدَعَتْنِي الدُّنْيا بِغُرُورِها
Dunia imenihadaa kwa udanganyifu wake,
وَنَفْسِي بِجِنايَتِها وَمِطالِي
na nafsi yangu kwa khiyana zake na utepetevu wangu.
ياسَيِّدِي فَأَسْأَلُكَ بِعِزَّتِكَ أَنْ لايَحْجُبَ عَنْكَ دُعائِي سُؤُ عَمَلِي وَفِعالي
Ewe Bwana wangu! Nakuomba kwa utukufu Wako, lisikataliwe ombi langu kwa ubaya wa amali zangu na vitendo vyangu,
وَلاتَفْضَحَنِي بِخَفِيِّ مااطَّلَعْتَ عَلَيْهِ مِنْ سِرِّي
wala Usinifedheheshe kwa kuyafichuwa yangu yaliyositirika ya siri.
وَلاتُعاجِلْنِي بِالعُقُوبَةِ عَلى ما عَمِلْتُهُ فِي خَلَواتِي
Na wala Usinipatilizie mateso kwa niliyoyatenda faraghani mwangu,
خَلَواتِي مِنْ سُؤِ فِعْلِي وَإِسأَتِي ، وَدَوامِ تَفْرِيطِي وَجَهالَتِي
kutokana na vitendo vyangu viovu na mabaya yangu, na kudumu kwangu kukiuka mipaka na ujinga wangu,
وَكَثْرَةِ شَهَواتِي وَغَفْلَتِي
na wingi wa matamanio yangu na kughafilika kwangu.
وَكُنِ اللّهُمَّ بِعِزَّتِكَ لِي فِي كُلِّ الاحْوالِ رَؤُوفاً ، وَعَلَيَّ فِي جَمِيعِ الامُورِ عَطُوفاً
Ewe Mwenyeezi Mungu! Kwa utukufu Wako, Kuwa mpole kwangu katika hali zote na Mwenye huruma mno juu yangu kwa yangu yote.
إِلهِي وَرَبِّي مَنْ لِي غَيْرُكَ أَسأَلُهُ كَشْفَ ضُرِّي وَالنَّظَرَ فِي أَمْرِي
Mungu wangu! Mlezi wangu! Nimtake nani asiyekuwa Wewe, anitatulie matatizo yangu na kunitizamia mambo yangu?
إِلهِي وَمَوْلايَ أَجْرَيْتَ عَلَيَّ حُكْماً اتَّبَعْتُ فِيهِ هَوى نَفْسِي وَلَمْ أَحْتَرِسْ فِيهِ مِنْ تَزْيينِ عَدُوِّي
Mungu wangu! Mola wangu! Ulinipangia kanuni, nikaandama humo mapenzi ya nafsi yangu, nisijilinde na vishawishi vya adui wangu.
فَغَرَّنِي بِما أَهْوى وَأَسْعَدَهُ عَلى ذلِكَ القَضاءُ
Basi akanihadaa kwa niliyokuwa nikiyapenda, ikimsaidia kulitekeleza hilo kadari,
فَتَجاوَزْتُ بِما جَرى عَلَيَّ مِنْ ذلِكَ بَعْضَ حُدُودِكَ
nikavuka baadhi ya mipaka uliyoniwekea,
وَخالَفْتُ بَعْضَ أَوامِرِكَ
na nikakhalifu baadhi ya amri Zako.
فَلَكَ الحَمْدُ عَلَيَّ فِي جَمِيعِ ذلِكَ
Kwa yote hayo shukurani ni Zako,
وَلاحُجَّةَ لِي فِيما جَرى عَلَيَّ فِيهِ قَضاؤُكَ وَأَلْزَمَنِي حُكْمُكَ وَبَلاؤُكَ
wala mimi sina utetezi kwa uamuzi Wako, ikinipasa hukumu Yako na adhabu Yako.
وَقَدْ أَتَيْتُكَ ياإِلهِي بَعْدَ تَقْصِيرِي وَإِسْرافِي عَلى نَفْسِي
Hakika, nimekujia Ewe Mola wangu! baada ya uzembe wangu na kuzidi kuikosea nafsi yangu,
مُعْتَذِراً نادِماً مُنْكَسِراً مُسْتَقِيلاً
hali yakuwa ni mwenye kujitolea udhuru na mwenye kujuta, na kwa hali ya tahayuri na unyonge,
مُسْتَغْفِراً مُنِيباً مُقِرّاً مُذْعِنا مُعْتَرِفاً لا أَجِدُ مَفَرّاً مِمّا كانَ مِنِّي
nikiwa ni mwenye kuomba msamaha na ni mwenye kutubia, ni kiwa mwenye kuungama na kunyenyekea, nikijitambua kuwa sina pakukimbilia kwa hali niliyonayo,
وَلا مَفْزَعاً أَتَوَجَّهُ إِلَيْهِ فِي أَمْرِي، غَيْرَ قَبُوُلِكَ عُذْرِي
wala sina muhifadhi wa kumwelekea kwa niliyoyatenda isipokuwa Wewe kunikubalia udhuru wangu,
وَإِدْخالِكَ إِيّايَ فِي سَعَةِ رَحْمَتِكَ
na ukaniegesha mimi eneoni mwa rehema Zako.
اللّهُمَّ فَاقْبَلْ عُذْرِي ، وَارْحَمْ شِدَّةَ ضُرِّي وَفُكَّنِي مِنْ شَدِّ وَثاقِي
Ewe Mwenyeezi Mungu! basi nikubalie udhuru wangu na unihurumie kwa dhiki zangu, na unifungue na kifungo changu kizito.
يارَبِّ ارْحَمْ ضَعْفَ بَدَنِي ، وَرِقَّةَ جِلْدِي ، وَدِقَّةَ عَظْمِي
Ewe Mlezi wangu! Uhurumie, udhaifu wa mwili wangu, ulaini wa ngozi yangu na wepesi wa mifupa yangu kuvunjika.
يامَنْ بَدَأَ خَلْقِي وَذِكْرِي وَتَرْبِيَتِي وَبِرِّي وَتَغْذِيَتِي
Ewe uliyetanguliza kuniumba, kunitambulisha, kunilea, kunitendea wema na kunilisha,
هَبْنِي لابْتِدأِ كَرَمِكَ وَسالِفِ بِرِّكَ بِي
endelea kunipa kwa ukarimu Wako na wema Wako ulionitangulizia.
ياإِلهِي وَسَيِّدِي وَرَبِّي
Ewe Mungu wangu! Bwana wangu! Mlezi wangu!
أَتُراكَ مُعَذِّبِي بِنارِكَ بَعْدَ تَوْحِيدِك
Ndivyo basi! Niadhibiwe kwa moto Wako baada ya kukupwekesha?
وَبَعْدَما انْطَوى عَلَيْهِ قَلْبِي مِنْ مَعْرِفَتِكَ
Na baada ya welekevu wa moyo wangu kukufahamu
وَلَهِجَ بِهِ لِسانِي مِنْ ذِكْرِكَ وَاعْتَقَدَهُ ضَمِيرِي مِنْ حُبِّكَ
na uzoefu wa ulimi wangu kukutaja, na kukupenda kwa dhati ya moyo wangu!
وَبَعْدَ صِدْقِ إِعْتِرافِي وَدُعائِي خاضِعاً لِرُبُوبِيَّتِكَ
Na baada ya kukiri kwangu ukweli, na maombi yangu nikinyenyekea Ulezi Wako?!
هَيْهاتَ ! أَنْتَ أَكْرَمُ مِنْ أَنْ تُضَيِّعَ مَنْ رَبَّيْتَهُ
Lipishe mbali hilo! Wewe Umkarimu mno hata Uje Umtupe uliyemlea!
أَوْ تُبَعِّدَ مَنْ أَدْنَيْتَهُ أَوْ تُشَرِّدَ مَنْ آوَيْتَهُ ، أَوْ تُسَلِّمَ إِلى البَلاءِ مَنْ كَفَيْتَهُ وَرَحِمْتَهُ
Au Uje kumtenga Uliyemkaribisha! Au Uje kumtelekeza Uliyemuhifadhi! Au Uje kumtumbukiza balaani Uliyemkifu na kumrehemu!
وَلَيْتَ شِعْرِي ياسَيِّدِي وَإِلهِي وَمَوْلايَ
Litanishangaza! Ewe Bwana wangu! Mungu wangu! Mola wangu!
أَتُسَلِّطُ النّارَ عَلى وُجُوهٍ خَرَّتْ لِعَظَمَتِكَ ساجِدَة
Endapo Utausaliti moto juu ya nyuso zilizo kuangukia kwa utukufu Wako zikakusujudia,
وَعَلى أَلْسُنٍ نَطَقَتْ بِتَوْحِيدِكَ صادِقَةً وَبُشُكْرِكَ مادِحَةً
na kwa ndimi zilizo tamka kukupwekesha kikweli-kweli, na kwa shukurani Zako zikakusifu!
وَعَلى قُلُوبٍ أَعْتَرَفَتْ بِإِلهِيَّتِكَ مُحَقِّقَةً
Na nyoyo zilizokiri uola Wako kihakika!
وَعَلَى ضَمائِرَ حَوَتْ مِنَ العِلْمِ بِكَ حَتّى صارَتْ خاشِعَةً
Na nafsi zilizopata ujuzi kutoka Kwako mpaka zikawa ni zenye kunyenyekea!
وَعَلى جَوارِحَ سَعَتْ إِلى أَوْطانِ تَعَبُّدِكَ طائِعَةً
Na viungo vilivyo kwenda kwa hima hashuoni kukuabudu kwa utwiifu!
وَأَشارَتْ بِإِسْتِغْفارِكَ مُذْعِنَةً
Na akijibidiisha kwa tamaa ya kupata maghofira Yako!
ماهكَذا الظَنُّ بِكَ وَلا اُخْبِرْنا بِفَضْلِكَ عَنْك ياكَرِيمُ
Hata! sivyo hivi tunavyo kudhania wala sivyo tulivyoelezwa kuhusu fadhila Zako zitokazo Kwako Ewe Uliyemkarimu!
يارَبِّ وَأَنْتَ تَعْلَمُ ضَعْفِي عَنْ قَلِيلٍ مِنْ بَلاءِ الدُّنْيا وَعُقُوباتِها وَمايَجْرِي فِيها مِنَ المَكارِهِ عَلى أَهْلِها
Ewe Mlezi wangu! Wewe waujua udhaifu wangu wa kutoweza uchache wa matatizo ya kilimwengu na mateso yake, na maudhi yanayo endelea humo kwa wakazi wake.
عَلى أَنَّ ذلِكَ بَلاٌ وَمَكْروهٌ قَلِيلٌ مَكْثُهُ ، يَسِيرٌ بَقاؤهُ قَصِيٌر مُدَّتُهُ
Na hakika, balaa hizo na maudhi hayo ni ya kipindi kidogo, huwepo kwa tahafifu na muda wake ni mfupi,
فَكَيْفَ إِحْتِمالِي لِبَلاءِ الاخِرَةِ وَجَلِيلِ وُقُوعِ المَكارِهِ فِيها
basi vipi nitayahimili mimi matatizo ya Akhera na kukumbwa na maudhi makubwa mno humo?
وَهُوَ بَلاٌ تَطُولُ مُدَّتُهُ وَيَدُومُ مَقامُهُ وَلايُخَفَّفُ عَنْ أَهْلِهِ
Nazo ni balaa ambazo muda wake ni mrefu, na zenye kudumu, wala hamna tahafifu kwa wakazi wake.
أَهْلِهِ لاَنَّهُ لايَكُونُ إِلاّ عَنْ غَضَبِكَ وَانْتِقامِكَ وَسَخَطِكَ وَهذا ما لاتَقُومُ لَهُ السَّماواتُ وَالارْضُ
Kwani hilo haliwi ila kwa ghadhabu Zako na malipo Yako na ukali Wako,
kwazo hata mbingu na ardhi katu hazihimili!
ياسَيِّدِي فَكَيْفَ لِي وَأَنا عَبْدُكَ الضَّعِيفُ الذَّلِيلُ الحَقِيرُ المِسْكِينُ المُسْتَكِينُ
Ewe Bwana wangu! Basi kefu mimi? Na mimi ni mja Wako dhaifu, mnyonge, duni hali,
masikini mwenye kubeheneka.
ياإِلهِي وَرَبِّي وَسَيِّدِي وَمَوْلايَ ، لايِّ الاُمُورِ إِلَيْكَ أَشْكُو
Ewe Mungu wangu, Mlezi wangu, Bwana wangu, Mola wangu! Nikushitakie yapi?
وَلِما مِنها أَضِجُّ وَأَبْكِي لاَلِيمِ العَذابِ وَشِدَّتِهِ ، أَمْ لِطُولِ البَلاءِ وَمُدَّتِهِ
Na kwa lipi nilie na kuomboleza? Kwa uchungu wa adhabu na uzito wake, ama kwa kurefuka kwa mateso na muda wake?!
لَئِنْ صَيَّرْتَنِي لِلْعُقُوباتِ مَعَ أَعْدائِكَ ، وَجَمَعْتَ بَيْنِي وَبَيْنَ أَهْلِ بَلائِكَ وَفَرَّقْتَ بَيْنِي وَبَيْنَ أَحِبّائِكَ وَأَوْلِيائِكَ
Iwapo Utaniadhibu pamoja na adui Zako, na Ukanijumuisha mimi pamoja na waliyostahili adhabu Yako, na Ukanitenga mbali na wapenzi Wako na mawalii Wako;
فَهَبْنِي ياإِلهِي وَسَيِّدِي وَمَوْلايَ وَرَبِّي
basi Ewe Mungu wangu, Bwana wangu, Mola wangu, Mlezi wangu!
صَبَرْتُ عَلى عَذابِكَ فَكَيْفَ أَصْبِرُ عَلى فِراقِكَ؟
Tuseme nimeistahimilia adhabu Yako, nitawezaje kustahamili kuwa mbali Nawe?
وَهَبْنِي صَبَرْتُ عَلى حَرِّ نارِكَ فَكَيْفَ أَصْبِرُ عَنِ النَّظَرِ إِلى كَرامَتِكَ ، أَمْ كَيْفَ أَسْكُنُ فِي النّارِ وَرَجائِي عَفْوُكَ ؟
Na tuseme nimeuvumilia ukali wa moto Wako, nitawezaje kuvumilia kunyimwa ukarimu Wako? Ama vipi niwe mtulivu motoni na matarajio yangu ni msamaha Wako?
َبِعِزَّتِكَ ياسَيِّدِي وَمَوْلايَ اُقْسِمُ صادِقاً
Naapa kwa Utukufu Wako Ewe Bwana wangu, Mola wangu!
لَئِنْ تَرَكْتَنِي ناطِقاً لاَضِجَّنَّ إِلَيْكَ بَيْنَ أَهْلِها ضَجِيجَ الامِلِينَ
Kihakika, lau utaniacha nimwenye kutamka! Nitakulilia kwa mayowe katikati ya wakazi wake (motoni), kilio cha wenye matarajio.
وَلاَصْرُخَنَّ إِلَيْكَ صُراخَ المُسْتَصْرِخِينَ وَلاَبْكِيَنَّ عَلَيْكَ بُكأَ الفاقِدِينَ
Nitakupigia unyende wa kweli, unyende wa wanao taka kupatilizwa, na nitakulilia kilio cha wenye kukatikiwa na matumaini.
وَلاُنادِيَنَّكَ أَيْنَ كُنْتَ ياوَلِيَّ المُؤْمِنِينَ ، ياغايَةَ اَّمالِ العارِفِينَ ياغِياثَ المُسْتَغِيثِينَ ،
ياحَبِيبَ قُلوُبِ الصّادِقِين وَيا إِلهَ العالَمينَ
Na nitakulingania 'Ukowapi Ewe Msimamizi wa waumini? Ewe Mwisho wa tumaini la wajuzi! Ewe Msaidizi wa wenye kuomba usaidizi! Ewe kipenzi cha nyoyo za wakweli! Ewe Mola wa viumbe vyote!'
أَفَتُراكَ سُبْحانَكَ ياإِلهي وَبِحَمْدِكَ
Itakuwaje tena? Ewe Mungu wangu Uliyetakasika na Mwenye sifa njema!
تَسْمَعُ فِيها صَوتَ عَبْدٍ مُسْلِمٍ سُجِنَ فِيها بِمُخالَفَتِهِ
Hivi Uisikie sauti ya mja Wako Mwislamu, aliyefungwa humo kwa uhalifu wake,
وَذاقَ طَعْمَ عَذابِها بِمَعْصِيَتِهِ ، وَحُبِسَ بَيْنَ أَطْباقِها بِجُرْمِهِ وَجَرِيرَتِهِ
na akaonja uchungu wa adhabu kwa maasia yake, amezuiliwa kati ya matabaka humo kwa ajili ya makosa yake na jeuri zake,
وَهُوَ يَضجُّ إِلَيْكَ ضَجِيجَ مُؤَمِّلٍ لِرَحْمَتِكَ
huku anakulilia kilio cha matumaini atazamia rehema Zako,
وَيُنادِيكَ بِلِسانِ أَهْلِ تَوْحِيدِكَ ، وَيَتَوَسَّلُ إِلَيْكَ بِرُبُوبِيَّتِكَ
na akikulingania kwa ulimi wa wenye kukupwekesha na kujikurubisha Kwako kwa Uola Wako!
يامَوْلايَ فَكَيْفَ يَبْقى فِي العَذابِ وَهُوَ يَرْجوُ ماسَلفَ مِنْ حِلْمِكَ ؟
'Ewe Mola wangu' Basi hwendaje abakiye kwenye adhabu na yeye atarajia upole Wako uliomtangulia.
أَمْ كَيْفَ تُؤْلِمُهُ النَّارُ وَهُوَ يَأْمَلُ فَضْلَكَ وَرَحْمَتَكَ ؟
Ama vipi moto umuumize naye ana matumaini ya fadhila zako na rehema Zako!
أَمْ كَيْفَ يُحْرِقُهُ لَهِيبُها وَأَنْتَ تَسْمَعُ صَوْتَهُ وَتَرى مَكانَهُ ؟
Ama vipi ndimi za moto zimchome na Wewe waisikia sauti yake na wamuona alimo?
أَمْ كَيْفَ يَشْتَمِلُ عَلَيْهِ زَفِيرُها وَأَنْتَ تَعْلَمُ ضَعْفَهُ ؟
Ama vipi vishindo vimkusanyikie humo, hali Wewe waujua udhaifu wake?
أَمْ كَيْفَ يَتَقَلْقَلُ بَيْنَ أَطْباقِها وَأَنْتَ تَعْلَمُ صِدْقَهُ ؟
Ama vipi ahangaike baina ya matabaka yake (humo) na Wewe waujua ukweli wake?
أَمْ كَيْفَ تَزْجُرُهُ زَبانِيَتُها وَهُوَ يُنادِيكَ يارَبَّاه ؟
Ama ni vipi Mazabaaniya wamzuilie humo na yeye akulingania 'Ewe Bwana wangu'?
أَمْ كَيْفَ يَرْجُو فَضْلَكَ فِي عِتْقِهِ مِنْها فَتَتْرُكُهُ فِيها ؟
Ama ni vipi, atarajia fadhila Zako umwepushe na moto kisha wamuacha mumo humo?
هَيْهاتَ ! ما ذَلِكَ الظَنُّ بِكَ ، وَلا المُعْروفُ مِنْ فَضْلِكَ
Si lakuwa hilo! Kwani si laiki Yako kuwa hivyo, wala si ule umaarufu wa fadhila Zako,
وَلامُشْبِهٌ لِما عامَلْتَ بِهِ المُوَحِّدِينَ مِنْ بِرِّكَ وَإِحْسانِكَ
na wala hayalingani na wema Wako na hisani Yako uliyowatendea wenye kukupwekesha.
فَبِالْيَقِينِ أَقَطَعُ ، لَولا ماحَكَمْتَ بِهِ مِنْ تَعْذِيبِ جاحِدِيكَ وَقَضَيْتَ بِهِ مِنْ إِخْلادِ مُعانِدِيكَ
Naamini kwa yakini kabisa, lau Hukuhukumu kuwaadhibu wanao kukanusha, na hivyo Ukaamua wabaki humo milele wapinzani Wako,
لَجَعْلْتَ النَّارَ كُلَّها بَرْداً وَسَلاماً ، وَما كَانَ لاَحَدٍ فِيها مَقَرّاً وَلامُقاماً
Ungeliufanya moto wote kuwa baridi na salama, na haitakuwa humo ni makazi wala makao kwa yeyote.
لكِنَّكَ تَقَدَّسَتْ أَسْماؤُكَ
Lakini yametakasika majina Yako,
أَقْسَمْتَ أَنْ تَمْلاَها مِنَ الكافِرِينَ ، مِنَ الجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ، وَأَنْ تُخَلِّدَ فِيها المُعانِدِينَ
Ulishakata kuwajaza humo makafiri kutokana na majini na watu pamoja, na kuwabakisha humo milele walokaidi.
وَأَنْتَ جَلَّ ثَناؤُكَ قُلْتَ مُبْتَدِئاً ، وَتَطَوَّلْتَ بِالاِنْعامِ مُتَكَرِّماً
Na Wewe sifa Zako zimetukuka, Ulisema mbeleni na Ukiendeleza kuneemesha Ukikirimu,
أَفَمَنْ كانَ مُؤْمِناً كَمَنْ كانَ فاسِقاً ، لايَسْتَوُونَ
"Je! aliye Muumini na mpotovu huwa sawa? La! Hawawi sawa."
إِلهِي وَسَيِّدِي ، فَأَسأَلُكَ بِالقُدْرَةِ الَّتِي قَدَّرْتَها وَبِالقَضِيَّةِ الَّتِي حَتَمْتَها وَحَكَمْتَها ، وَغَلَبْتَ مَنْ عَلَيْهِ أَجْرَيْتَها
Mungu wangu, Bwana wangu! Basi nakuomba kwa uwezo Ulioukadiria, na kwa uamuzi Uliyoupasisha na kuupitisha, na ukamshinda Uliyempangia.
أَنْ تَهَبَ لِي فِي هذِهِ اللّيْلَةِ وَفِي هذِهِ السَّاعَةِ
Uwe ni Mwenye kunisamehe katika usiku huu na saa hii,
كُلَّ جُرْمٍ أَجْرَمْتُهُ وَكُلَّ ذَنْبٍ أَذْنَبْتُهُ ، وَكُلَّ قَبِيحٍ أَسْرَرْتُهُ ، وَكُلَّ جَهْلٍ عَمِلْتُهُ ، كَتَمْتُهُ أَوْ أَعَلَنْتُهُ ، أَخْفَيْتُهُ أَوْ أَظْهَرْتُه
kila ovu nililolitenda na kila dhambi niliyoifanya, na kila uchafu nilioufanya kwa siri na kila ujinga nilioutekeleza kwa kuficha au waziwazi, kwa kuuficha au kwa dhahiri;
وَكُلَّ سَيِّئَةٍ أَمَرْتَ بِإِثْباتِها الكِرامَ الكاتِبِينَ ، الَّذِينَ وَكَّلْتَهُمْ بِحِفْظِ مايَكُونُ مِنِّي
na kila mabaya Uliyoamrisha kusajiliwa na Waandishi watukufu Uliowaakilisha kuyadhibiti yangu yote.
وَجَعَلْتَهُمْ شُهُوداً عَلَيّ مَعَ جَوارِحِي
Na Ukawafanya wao na viungo vyangu pia kuwa ni mashahidi juu yangu,
وَكُنْتَ أَنْتَ الرَّقِيبَ عَلَيَّ مِنْ وَرائِهِمْ ، وَالشَّاهِدَ لِما خَفِي عَنْهُمْ ، وَبِرَحْمَتِكَ أَخْفَيْتَهُ ، وَبِفَضْلِكَ سَتَرْتَهُ
huku ukiwa Wewe juu yao ni Mchungaji wangu, Ukiyashuhudia yale yaliyofichamana kwao, kwa rehema Zako Uliyaficha na kwa fadhila Zako Ukayasitiri.
وَأَنْ تُوَفِّرَ حَظِّي مِنْ كُلِّ خَيْرٍ أَنْزَلْتَهُ ، أَوْ إِحْسانٍ فَضَّلْتَهُ أَوْ بِرٍّ نَشَرْتَهُ، أَوْ رِزْقٍ بَسَطْتَهُ ، أَوْ ذَنْبٍ تَغْفِرُهُ أَوْ خَطأ تَسْتُرُهُ
Nizidishie fungu langu kwa kila kheri Unayoiteremsha au wema Unaoutoa, au zuri Unalolieneza au riziki Unayoigawa, au dhambi Unayoighofiria au kosa Unalolisitiri.
يارَبِّ يارَبِّ يارَبِّ ، ياإِلهِي وَسَيِّدِي
Ewe Mlezi wangu! Ewe Mlezi wangu! Ewe Mlezi wangu! Ewe Mungu wangu, Bwana wangu,
وَمَوْلايَ وَمالِكَ رِقِّي ، يامَنْ بِيَدِهِ ناصِيَتِي ياعَلِيماً بِضُرِّي وَمَسْكَنَتِي ، ياخَبِيراً بَفَقْرِي وَفاقَتِي
Mola wangu! Ewe Mwenye kumiliki utumishi wangu! Ewe Ambaye uongofu wangu uko mikononi Mwake! Ewe Mjuzi wa madhara yangu na makazi yangu! Ewe Mwenye kuujua ufakiri wangu na mahitaji yangu!
يارَبِّ يارَبِّ يارَبِّ أَسأَلُكَ بِحَقِكَ وَقُدْسِكَ وَأَعْظَمِ صِفاتِكَ وَأَسْمائِكَ
Ewe Mlezi wangu! Ewe Mlezi wangu! Ewe Mlezi wangu! Nakuomba kwa haki Yako na utukufu Wako na ubora wa sifa Zako na majina Yako,
أَنْ تَجْعَلَ أَوْقاتِي مِنَ اللّيْلِ وَالنَّهارِ بَذِكْرِكَ مَعْمُورَةً ، وَبِخِدْمَتِكَ مَوْصُولَةً
Unijaalie katika nyakati zangu za usiku na mchana, daima niendelee kukukumbuka, na niambatane na utumishi Wako.
وَأَعْمالِي عِنْدَكَ مَقْبُولَةًً ، حَتَّى تَكُونَ أَعْمالِي وأوْرادِي كُلُّها وِرْداً وَاحِداً، وَحالِي فِي خِدْمَتِكَ سَرْمَداً
Na amali zangu ziwe kabuli Kwako hadi vitendo vyangu na nyuradi zangu ziwe kitu kimoja, na kwa milele niwe nakutumikia.
ياسَيِّدِي يامَنْ عَلَيْهِ مُعَوَّلِي ، يامَنْ إِلَيْهِ شَكَوْتُ أَحْوالِي
Ewe Bwana wangu! Ewe Ambae tegemeo langu li-Kwake! Ewe Ambae Kwake nashitakia hali zangu!
يارَبِّ يارَبِّ يارَبِّ ، قَوِّ عَلى خَدْمَتِكَ جَوارِحِي
Ewe Mlezi wangu! Ewe Mlezi wangu! Ewe Mlezi wangu! Vithibitishe viungo vyangu nikutumikie,
وَاشْدُدْ عَلى العَزِيمَةِ جَوانِحِي وَهَبْ لِيَ الجِدَّ فِي خَشْيَتِكَ
Liamirishe kusudio langu lakujihifadhi, Uniwezeshe nijiogopee Kwako,
وَالدَّوامَ فِي الاِتِّصالِ بِخِدْمَتِكَ حَتَّى أَسْرَحَ إِلَيْكَ فِي مَيادِينِ السابِقِينَ
Na daima nishikamane na utumishi Wako mpaka nikufikilie vyeo vya waliotangulia,
واُسْرِعَ إِلَيْكَ فِي البارِزِينَ ، وَأَشْتاقَ إِلى قُرْبِكَ فِي المُشْتاقِينَ
nikuananie kati ya wanao kukimbilia, niwe na shauku ya kuwa karibu Nawe pamoja na wakupendao.
وَأَدْنُوَ مِنْكَ دُنُوَّ المُخْلِصِينَ ، وَأَخافَكَ مَخافَةَ المُوقِنِينَ ، وَأَجْتَمِعَ فِي جِوارِكَ مَعَ المُؤْمِنِينَ
Na nsiogelee Kwako na wanao sogea kwa ikhlasi, na nikuche kwa kicho cha wenye yakini na nijiunge pamoja na Waumini kuwa karibu nawe.
اللّهُمَّ وَمَنْ أَرادَنِي بِسُؤٍ فَأَرِدْهُ ، وَمَنْ كادَنِي فَكِدْهُ
Ewe Mwenyeezi Mungu! Na anayenitakia ubaya mrudishie, na mwenye kunichimbia nayeye mrudi.
وَاجْعَلْنِي مِنْ أَحْسَنِ عَبِيدِكَ نَصِيباً عِنْدَكَ ، وَأَقْرَبِهِمْ مَنْزِلَةً مِنْكَ ، وَأَخَصِّهِمْ زُلْفَةً لَدَيْكَ فِإِنَّهُ لايُنالُ ذلِكَ إِلا بِفَضْلِكَ
Na unijaalie niwe katika waja Wako bora wenye fungu Kwako, na wa daraja ya karibu mno Kwako na cheo maalumu mbele Yako, kwani hakika kwa amri na shani Yako hayo hayapatikani ila kwa fadhila Zako.
وَجُدْ لِي بِجُودِكَ، وَاعْطِفْ عَلَيَّ بَمَجْدِكَ، وَأَحْفَظْنِي بِرَحْمَتِكَ
Unipe kwa upaji Wako, Unisikitikie kwa utukufu Wako, na kwa rehema Zako unihifadhi.
وَأَجْعَلْ لِسانِي بِذِكْرِكَ لَهِجاً ، وَقَلْبِي بِحُبِّكَ مُتَيَّماً وَمُنَّ عَلَيَّ بِحُسْنِ إِجابَتِكَ
Ufanye ulimi wangu kwa kukukumbuka ni wenye kukutaja, na moyo wangu uenee mapenzi Yako, na kwa wema Wako nitakabalie.
وَأَقِلْنِي عَثْرَتِي ، وَاغْفِرْ زَلَّتِي فَإِنَّكَ قَضيْتَ عَلى عِبادِكَ بِعِبادَتِكَ ، وَأَمَرْتَهُمْ بِدُعائِكَ ، وَضَمِنْتَ لَهُمُ الاِجابَةَ
Nipunguzie maovu yangu na unighofirie kusepetuka kwangu. Hakika uliwaamuliya waja Wako wakuabudu, na ukawaamrisha wakuombe, na umewadhamini majibu.
فَإِلَيْكَ يارَبِّ نَصَبْتُ وَجْهِي ، وَإِلَيْكَ يارَبِّ مَدَدْتُ يَدِي
Basi Kwako Ewe Mlezi wangu, nimeuwelekeza uso wangu, na Kwako Ewe Mlezi wangu nimeinyanyua mikono yangu.
فَبِعِزَّتِكَ أَسْتَجِبْ لِي دُعائِي ، وَبَلِّغْنِي مُنايَ وَلاتَقْطَعْ مِنْ فَضْلِكَ رَجائِي
Kwa utukufu Wako, nikubalie maombi yangu na unitimizie makusudio yangu, wala usinikatishe tamaa yangu kwa fadhila Zako.
وَاكْفِنِي شَرَّ الجِنِّ وَالاِنْسِ مِنْ أعْدائِي
Niakifishia shari za majini na watu katika maadui zangu.
سَرِيعَ الرِّضا إِغْفِرْ لِمَنْ لايَمْلِكُ إِلا الدُّعأَ ،فَإِنَّكَ فَعَّالٌ لِما تَشأُ
Ewe Mwenye kuridhika upesi! Mghofirie asiyemiliki kitu ila dua, kwani hakika Wewe hulitenda ulitakalo.
يامَنْ إِسْمُهُ دَوأٌ ، وَذِكْرُهُ شِفأٌ ، وَطاعَتُهُ غِنىً
Ewe Ambaye jina Lake ni dawa! Utajo Wake ni shufaa, na Utii Wake ni kutosheka,
إِرْحَمْ مَنْ رَأسُ مالِهِ الرَّجأُ وَسِلاحُهُ البُكأُ
mrehemu ambae rasilimali yake ni matumaini, na silaha yake ni kilio.
ياسَابِغَ النِّعَمِ ، يادافِعَ النِّقَمِ ، يانُورَ المُسْتَوْحِشِينَ فِي الظُّلَمِ
Ewe Mweneza neema! Ewe Mkinga balaa! Ewe Nuru ya waliyo wakiwa gizani,
ياعالِماً لايُعَلَّمُ ، صَلِّ عَلى مُحَمَّدٍ وَآلِ مُحَمَّدٍ ، وَأَفْعَلْ بِي ماأَنْتَ أَهْلُه
Ewe Mjuzi usiyefunzwa! Mswalie Muhammad na Aali Muhammad,
unifanyie yale ambayo ni laiki Yako.
وَصَلَّى اللّهُ عَلى رَسُولِهِ وَالاَئِمَّةِ المَيامِينَ مِنْ آلِهِ وَسَلَّمَ تَسْلِيماً كَثِيرا.
Swala za Mwenyeezi Mungu zimshukie Mtume Wake pamoja na Maimamu waaminifu katika Aali zake na salamu kamili nyingi mno.

MWISHO