IDADI YA AYA ZA QUR_ANI
  • Kichwa: IDADI YA AYA ZA QUR_ANI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 16:40:39 3-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI 

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

IDADI YA AYA ZA QUR_ANI

Watu wamehitilafiana nadhari kuhusiana na adadi ya aya za Qur-ani, lakini hitilafu hizo haimaanishi kwamba Qur-ani zinahitilafiana. Kwani ni jambo lililowazi na lisiloshaka ndani yake ya kwamba Qura-ni haijazidi wala kupunguwa Qur-ani zote ni moja na ni zenye kufanana hitilafu zilizopo ni katika adadi ya aya za Qur-ani, baadhi yao wamesema ya kwamba chanzo cha hitilafu hizo kinatokana pale Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu alipokuwa akisoma aya kwa masahaba zake alisita kidogo ili waelewe mwanzo na mwisho wa aya,  lakini kwa bahati mbaya baadhi ya masahaba wa Mtume walidhani kuwa pale Mtume alipokuwa akisita hakumaanishi kupambanua baina ya aya mbili, kwa hiyo waliziunganisha aya hizo na aya zinazofuata na kuhesabu kuwa ni aya moja tu, na baadhi ya masahaba wengine pale ambapo Mtume alipokuwa akisita walihesabu kuwa ni mwisho wa aya.

Sababu hizo basi ndizo zilizosababisha kutokea hitilafu kuhusiana na adadi ya aya za Qur-ani.

 AMA KUHUSIANA NA IDADI YA AYA ZA QUR_ANI

Kijumla jamala idadi ya aya za Qur-ani ni alfu sita na mia mbili, watu wote wamekubaliana ya kwamba kuhusiana na aya alfu sita hakuna hitilafu yoyote bali hitilafu iliyopo ni aya mia mbili zilizobakia. Ama kauli inayokubalika zaidi ni kwamba aya za Qur-ani ni 6236.

NADHARI MASHUHURI (MAARUFU) ISIYO SAHIHI KUHUSIANA NA IDADI YA AYA ZA QUR_ANI

Kauli iliyo mashuhuri ni kwamba idadi ya aya za Qur-ani ni 6666, hapana shaka ya kwamba kauli hiyo sio sahihi na haina ukweli wowote, na hakuna mtu yoyote aliyeithibitisha kauli hiyo, tunategemea kwamba tutafanya jitihada ili kuiondoa nadhari hiyo isiyo sahihi.

MWISHO