WILAYATI NA WALII NDANI YA QURAN
  • Kichwa: WILAYATI NA WALII NDANI YA QURAN
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 22:16:31 1-9-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

WILAYATI NA WALII NDANI YA QUR_ANI.

UFAFANUZI WA NENO WILAYAT (WALII).

Neno walii kilugha lina maana tofauti, miongoni mwa hizo ni:-

Walii yaani kuwa karibu bila ya umbali wa masafa, kama ilivyokuja katika Qur-ani:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ آبَاءكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ اَوْلِيَاء إَنِ اسْتَحَبُّواْ الْكُفْرَ عَلـٰي الإِيمَانِ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَاُوْلَـئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ[1]

Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mngu.

* Ikiwa una maadui walio hatari kwako, muanze aliye karibu yako,umlaze vizuri, waogope walio mbali ipatikane salama.

Walii ni mtu ambaye anasimamia na kuongoza mambo bila ya kupitia kwa mtu mwengine, kama ilivyokuja ndani ya Qur-ani:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَي اَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ وَلاَ يَاْبَ كَاتِبٌ اَنْ يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللّهُ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِى عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللّهَ رَبَّهُ وَلاَ يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئاً فَإن كَانَ الَّذِى عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهاً اَوْ ضَعِيفاً اَوْ لاَ يَسْتَطِيعُ اَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ وَاسْتَشْهِدُواْ شَهِيدَيْنِ من رِّجَالِكُمْ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَاَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاء اَن تَضِلَّ إْحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الاُخْرَي وَلاَ يَاْبَ الشُّهَدَاء إِذَا مَا دُعُواْ وَلاَ تَسْاَمُوْاْ اَن تَكْتُبُوْهُ صَغِيراً اَو كَبِيراً إِلَي اَجَلِهِ ذٰلِكُمْ اَقْسَطُ عِندَ اللهِ وَاَقْومُ لِلشَّهَادَةِ وَاَدْنَي اَلاَّ تَرْتَابُواْ إِلاَّ اَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ اَلاَّ تَكْتُبُوهَا وَاَشْهِدُوْاْ إِذَا تَبَايَعْتُمْ وَلاَ يُضَآرَّ كَاتِبٌ وَلاَ شَهِيدٌ وَإِن تَفْعَلُواْ فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ وَاتَّقُواْ اللّهَ وَيُعَلِّمُكُمُ اللّهُ وَاللّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ[2]

Enyi mlio amini! Mnapo kopeshana deni kwa muda ulio wekwa, basi andikeni. Na mwandishi aandike baina yenu kwa uadilifu, wala mwandishi asikatae kuandika.Aandike kama alivyo mfunza Mwenyezi Mungu. Na mwenye deni juu yake aandikishe; naye amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala asipunguze chochote ndani yake. Na akiwa mwenye kudaiwa ni mtu aliye pumbaa au mnyonge au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe mlinzi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili katika wanaume wenu. Ikiwa hapana wanaume wawili, basi mwanamume mmoja na wanawake wawili katika mnao waridhia kuwa mashahidi. Ili ikiwa mmoja wao akipotea, mmoja wao amkumbushe mwengine. Na mashahidi wasikatae waitwapo. Wala msipuuze kuliandika deni likiwa dogo au kubwa mpaka muda wake. Hayo ndiyo haki zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo sawa zaidi kwa ushahidi, na vyema zaidi ili msiwe na shaka. Ila ikiwa ni biashara ya mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipo iandika. Lakini mnapo uziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi. Na mkifanya hivyo basi hakika hilo ni kosa kwenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anakufundisheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.

Baadhi ya wakati mja huitwa walii kwa sababu ya utiifu na upendo wake, au kufaidika kwake na rehema za Mwenyeezi Mungu. Kama anavyosema Allah (s.w) kuwaambia waumini:-

اَلا إِنَّ اَوْلِيَاء اللهِ لاَ خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلاَ هُمْ يَحْزَنُونَ[3]

Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.

[1] Surat Tawba Aya ya 123

[2] Suratul-Baqarah Aya ya 282

[3] Surat Yunus Aya ya 62

MWISHO