NI KINA NANI WALIOKUWAMO KATIKA AHLUL-BAYT?
  • Kichwa: NI KINA NANI WALIOKUWAMO KATIKA AHLUL-BAYT?
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 14:10:59 6-10-1403

BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI

NI KINA NANI WALIOKUWAMO KATIKA AHLUL-BAYT?

Imeonyesha kwamba familia ya Mtume (s.a.w.) mara kwa mara hutajwa kama Ahlul-Bayt, 'Itrah na Aal - ikiwa ni pamoja na bintiye Fatima al-Zahra', mumewe Imam 'Ali, na watoto wao Imam al-Hasan na al-Huseyn (a.s.). Ikiwa ni familia ya watu watano, Mtume (s.a.w.) akiwa ni kiongozi wao, ambao walikuwa hai wakati Aya za Qur'an zikishuka kuhusu sifa zao kwa Mtume (s.a.w.). Hata hivyo, maimamu tisa kutoka kwa wajukuu wa Imam Husein (a.s.) pia ni katika wateule wa familia hii, wa mwisho akiwa ni Imam Mahdi (a.s.). Mtume (s.a.w.) amesema:
" "Mimi na 'Ali na al-Hasan na al-Huseyn na wajukuu tisa wa al-Huseyn ni watakatifu na wenye heshima." [al-Juwayni, Fara'id al-Simtayn, (Beirut, 1978), Uk. 160. Fahamu kwamba heshima ya al-Juwayni kama Mwanachuoni mkuu wa Hadith imethibitishwa na al-Dhahabi katika Tadhkirat al-Huffaz, Juz. 4, Uk. 298, na pia Ibn Hajar al-'Asqalani katika al-Durar al-Kaminah, Juz. 1, Uk. 67] " "Mimi ni mkuu wa Mitume na 'Ali ibn Abi Talib ni mkuu wa mawasii, na baada yangu mawasii wangu watakuwa ni kumi na wawili, wa mwanzo wao akiwa ni 'Ali ibn Abi Talib na wa mwisho ni al-Mahdi." [al-Juwayni, Fara'id al-Simtayn, Uk. 160] " "Al-Mahdi ni katika sisi Ahlul-Bayt" na "al-Mahdi atakuwa ni katika familia yangu, katika wajukuu wa Fatima" [Ibn Majah, al-Sunan, Juz. 2, Uk. 519, Na.s 4085-6; Abu Dawud, al-Sunan, Juz. 2, Uk. 207]

Vipi kuhusu wakeze Mtume (s.a.w.)?
Aya ya utakaso: "Hakika Mwenyezi Mungu anataka… " ilishuka wakati Mtume (s.a.w.) yuko kwenye nyumba ya mkewe Umm Salama (Mungu amuelee radhi); Mtume (s.a.w.) akamwita al-Hasan, al-Huseyn, Fatima na 'Ali, na akawakusanya wote hao na kuwafunika ndani ya shuka. Kisha akasema, "Ewe Mwenyezi Mungu, hawa ndio watu wangu wa nyumbani, watakase na uchafu wowote na uwatakase kabisa." Umm Salama akasema, "Je mimi ni pamoja nao ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Mtume (s.a.w.) akasema, "Kaa hapo ulipo, wewe u katika kheri."
" al-Tirmidhi, al-Sahih, Juz. 5, Kurasa 351 na 663
" al­Hakim al­Naysaburi, al­Mustadrak `ala al-Sahihayn, Juz. 2, Uk. 416. Amesema kwamba hii ni sahih kulingana na al-Bukhari " al-Suyuti, al-Durr al-Manthur, Juz. 5, Uk. 197

Mwanzo wa Aya 33:33 na maelezo yaliyofuata yawazungumzia wake za Mtume (s.a.w.) kama inavyoonyesha wazi dhamiri ya wanawake, lakini katika Aya ya Utakaso dhamiri yabadilika na kuwa ya kiume au ya kike na kiume. Hii pia yaonyesha kuwa wahyi pekee unaelezea watu tofauti. "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume (Ahlul-Bayt) na kuwatakasa kabisa." [Aya ya Utakaso, Qur'an 33:33]

Mtume Muhammad (s.a.w.) aliulizwa na Maswahaba wake: "Kwa namna gani tukutakie rehema?" … Akajibu: "Semeni: 'Ewe Mola! Mtakie rehma Muhammad na familia yake, kama ulivyomtakia rehma Ibrahim na familia yake, hakika Wewe uko mwenye kuhimidiwa, Mtukufu.'"
[Sahih al-Bukhari, Juz. 4, Kitabu 55, Hadith Na. 589]

Kwa nini kufuata familia (Ahlul-bayt) ya Mtume (s.a.w.)?
Shia wanaammini kwamba tirathi mbili za Mtume Muhammad (s.a.w.) ni Qur'an na Ahl ul-Bayt (watu maalum katika familia yake). Ahlul-Bayt ndio msingi wa kupata Sunnah sahihi za Mtume (s.a.w.). Ni kwa kupata maelezo kutoka katika misingi hii miwili tu ndipo mtu anaweza kuwa na matumaini ya kupata uongofu.

Turathi ya Mtume Muhammad (s.a.w.)
"Mimi niko karibu na kuitikia mwito (wa mauti). Hakika nawaachia vitu wiwili vizito vya thamani (thaqalayn): Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul Bayt wangu. Hakika viwili hivyo havitatengana mpaka vinijie kwenye hodhi." Hadith hii sahihi ya Mtume Muhammad (s.a.w.) imepokewa na zaidi ya Maswahaba wake thelathini na kunakilwa na Wanavyuoni wengi wa Kisunni, miongoni mwao ambao ni mashuhuri ni pamoja na:
" al­Hakim al­Naysaburi, al­Mustadrak `ala al-Sahihayn (Beirut), Juz. 3, Kurasa 109-110, 148, na 533). Huyu amesisitiza kuwa Hadith hii ni sahih kulingana na al­Bukhari na Muslim; al­Dhahabi amethibitisha hukmu yake
" Muslim, al-Sahih, (Tafsiri ya Kiingereza), Kitabu 031, Na. 5920-3
" al­Tirmidhi, al-Sahih, Juz. 5, Kurasa 621-2, Na.s 3786 na 3788; Juz. 2, Uk. 219
" al-Nasa'i, Khasa'is'Ali ibn Abi Talib, Hadith Na. 79
" Ahmad b. Hanbal, al-Musnad, Juz. 3, Kurasa 14, 17, 26; Juz. 3, Uk. 26, 59; Juz. 4, Uk. 371; Juz. 5, Kurasa 181-2, 189-190
" Ibn al­'Athir, Jami` al­'usul, Juz. 1, Uk. 277
" Ibn Kathir, al­Bidayah wa al­nihayah, Juz. 5, Uk. 209. Akimnukuu al-Dhahabi na amesema kwamba Hadith hii ni sahih.

" Ibn Kathir, Tafsir al-Qur'an al-'Adhim , Juz. 6, Uk. 199
" Nasir al-Din al-Albani, Silsilat al-AHadith al-Sahiha (Kuwait: al-Dar al-Salafiyya), Juz. 4, Kurasa 355-8. Yeye ametaja mapokezi mengi ambayo anayaona kuwa ni yenye kuaminika. Kuna mapokezi mengi ya Hadith ambayo hatuwezi kuyataja hapa.

Je, Mtume (s.a.w.) hakusema: "Nawaaachia Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah zangu"?
Suala hili lina utata. Ukweli ni kwamba hapana msingi wa ukweli wa kutegemewa wa kauli hii katika ile hotuba yake ya mwisho ya Mtume (s.a.w.) Kwa hakika haimo kabisa katika kitabu chochote miongoni mwa vitabu sita vya Sihah!! Maelezo katika kitabu cha Malik, al- Muwatta', cha Ibn Hisham, Sirat Rasul Allah, na kutoka kwake katika Tarikh ya al-Tabari, mapokezi yote ya hawa hayana mlolongo wa uliokamilika wa mapokezi, kwani baadhi ya msururu huo umekatika! Isitoshe mapokezi mengine ambayo yana mlolongo wa mapokezi (isnad) - ambao pia ni wachache mno - wote una wapokezi ambao, kiujumla, huchukuliwa - na Wanavyuoni wakubwa wa Sunii wa elimu ya Rijal -kuwa si waaminifu. Ukweli huu ulio wazi unaweza kuthibitishwa kwa kurejea vitabu vifaavyo vinavohusika na uwanja huo kwa wale wanaopenda kufanya utafiti.

Ni wazi kwamba hakuna apendekezaye kwamba Sunnah za Mtume (s.a.w.) zisifuatwe. Bali kama illivyoelezwa hapo awali kwamba Mtume (s.a.w.) aliwataka Waislamu kuwarejea Ahlu-Bayti wake wakiwa wao ndio waaminifu, watakatifu, na kwa hali yoyote ndio msingi wa Sunnah zake.

Kuna jambo gani mahsusi kuhusu familia ya Mtume (s.a.w.)?
Wakati Aya ii iliposhuka: "Sema ewe Muhammad, siwaombi malipo yoyote (Kwa Mtume kuleta ujumbe huu) ila muwapende watu wangu wa karibu," Waislamu walimuuliza Mtume (s.a.w.): "Ni kina nani hao jamaa zako wa karibu ambao imetupasa tuwapende?" Akajibu, "Ali, Fatima, na watoto wao wawili."
" al­Hakim al­Naysaburi, al­Mustadrak `ala al-Sahihayn, Juz. 2, Uk. 444
" al-Qastallani, Irshad al-Sari Sharh Sahih al-Bukhari, Juz. 7, Uk. 331
" al-Suyuti, al-Durr al-Manthur, Juz. 6, Kurasa 6-7
" al-Alusi al-Baghdadi, Ruh al-Ma'ani, Juz. 25, Kurasa 31-2

Daraja ya uaminifu na heshima ya Ahlul-Bayt waliyokuwa nayo imethibitishwa zaidi na Qur'an wakati wa majadiliano na Wakristo wa kutoka Najran. Wakati Aya ii iliposhuka: "Watakaokuhoji (sasa) baada ya kukufikia ilimu, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na sisi na nyinyi, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo." (3:61), Mtume (s.a.w.) aliwaita 'Ali, Fatima, al-Hasan na al-Huseyn na akasema: 'Ewe Mwenyezi Mungu, hawa ndio familia yangu (Ahli)'.

" Muslim, al-Sahih, (Tafsiri ya Kiingereza), Kitabu 031, Na. 5915
" al­Hakim al­Naysaburi, al­Mustadrak `ala al-Sahihayn, Juz. 3, Uk. 150. Amesema kwamba hii ni sahih kulingana na al-Bukhari na Muslim
" Ibn Hajar al-'Asqalani, Fat-h al-Bari Sharh Sahih al-Bukhari, Juz. 7, Uk. 60
" al-Tirmidhi, al-Sahih, kitab al-manaqib, Juz. 5, Uk. 596
" Ahmad b. Hanbal, al-Musnad, Juz. 1, Uk. 185
" al-Suyuti, History of Khalifas Who Took The Right Way, (London, 1995), Uk. 176

Je yatosha kuonyesha heshima kwa Ahlul-Bayt?
Je yatosha kuonyesha heshima kwa Qur'an? Hakika Waislamu ni lazima waifuate ikiwa ni Msingi wa mwongozo wa Mwenyezi Mungu katika mambo yao yote. Mtume Muhammad (s.a.w.) aliacha vitu viwili hivi ikiwa ni tirathi kwa Waislamu, na akaahidi kwamba havitatengana mpaka siku ya Kiyama. Mtume (s.a.w.) alipoviweka pamoja vitu hivi viwili, Qur'an na Ahlul Bayt alikuwa akitwambia kwamba tusiviheshimu tu bali tuchukue ufananuzi wa mafunzo ya Kiiislamu, matendo, Hadith na tafsir kutoka kwenye viwili hivyo.

"Tazama! Ahlul-Bayt wangu ni kama jahazi la (Nabii) Nuh, atakayelipanda basi ataokoka, na atakayeliepuka ataangamia".
" al­Hakim al­Naysaburi, al­Mustadrak `ala al-Sahihayn, Juz. 3, p. 151 na Juz. 2, Uk. 343. Yeye amesema kwamba hii ni sahihi kulingana na maelezo ya Muslim
" al-Suyuti, al-Durr al-Manthur, Juz. 1, Kurasa 71-72
" Ibn Hajar al-Makki, al-Sawa'iq al-Muhriqa, Uk. 140. Huyu amesema kwamba Hadith hii imepitia mlolongo mrefu wa mapokezi unaoshikana imara.

MWISHO