VIPI QURANI NA WATU WA NYUMBA YA MTUME
  • Kichwa: VIPI QURANI NA WATU WA NYUMBA YA MTUME
  • mwandishi:
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 9:46:51 13-8-1403

VIPI QURANI NA WATU WA NYUMBA YA MTUME WANALIANGALIA SUALA LA UONGOZI

KWA NINI SHIA WANAAMINI KUA IMAM ALI (A.S) NI KHALIFA WA KWANZA BAADA YA MTUME?

Shia Ithna Ashariya wanaamini kua Imam Ali bin Abitalib ni Khalifa na Imam wa kwanza baada ya Mtume (S.A.W.W) kwa kuzingatia sababu moja rahisi sana na iliyo wazi. Sababu hii ni kuwa; "Imam Ali bin Abii Taalib (A.S) aliteuliwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu kua Khalifa wa kwanza wa Waislamu na Mtume mwenyewe kwa amri ya Mwenyezi Mungu (s.w. t). Hii ndio sababu na hakuna sababu nyengine. Katika Qur'an tukufu (59: 7) Mwenyezi Mungu anasema: "…….Na anachokupeni Mtume basi pokeeni na anachokukatazeni jiepusheni nacho". Qur'an (33:36): "Na haiwi kwa Muumini wa kiume wala kwa Muumini wa kike, pale Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, waumini hao wawe ni wenye kuyatenda mambo yao kwa rai zao au wawe chaguo katika kuyatenda yale waalioamrishwa. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotevu ulio wazi"'. Shia wanaamini kwamba maadamu Mtume (S.A.W.W) mwenyewe kwa amri ya Mwenyezi Mungu alimteua Imam Ali (a.s) kuwa Khalifa, basi Waislamu hawana hiari yoyote isipokuwa kuitii amri hii.

MWISHO