IMAMU HUSSEIN NI NEMBO YA HAKI
  • Kichwa: IMAMU HUSSEIN NI NEMBO YA HAKI
  • mwandishi:
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 9:28:2 2-10-1403

IMAMU HUSSEIN NI NEMBO YA HAKI KATIKA UISLAM

Mara tu baada ya kifo cha Mtume Muhammad na kabla ya kukamilika kwa shughuli za mazishi, walijitokeza watu wengi waliokimbia mazishi hayo na badala yake kukimibilia katika ukumbi uliojulikana kwa jina la Saqifa Bani Saida.

Lengo la kukimbilia katika ukumbi huo, ni kupitisha maazimio ya kutokubaliana na wasia aliouwacha Mtume na kuusisitiza kwa muda wa miaka yote 23 ya kipindi cha utume wake.

Wasia huo ulikuwa ni kufuata uongozi wa watu wa nyumba ya Mtume (Ahlilbayt) ambao ni maimamu 12, kuanzia Imamu Aly Bin Abii Talib hadi kumalizia imamu Mahdi.

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Saqif Banii Saida, kiliibuka na mfumo mpya wa Utawala Haramu ambao ni kinyume na wasia wa Mtume.

Katika mfumo huu wa utawala ulioanzia Sqifa Banii Saida historia ilishuhudia na kusajili watawala kama vile:
Abuubakar, Omar Bin Khatab, Othman Bin Afan, Muawiya Bin Abi Sufiyan, Yazid Bin Muawiya na Wengineo.

Wakati huo huo kulikuwepo na uongozi halali wa Ahli Bayt, ambao tayari Mtume alishausia uwepo na kuwatambulisha jambo hilo waislam wote duniani tangu kipindi cha uhai wake, na ndiyo historia pia ikashuhuduia na kusajili maimamu wote 12 wa Ahlilbayt kwa kuanzia na:-

Imamu Aly Bin Abii Talib,Imamu Hasan Bin Ali, Imam Husseyn Bin Ali, na maimamu wengine 9 kutokana na kizazi cha Imamu Husseyn hadi kufikia Imamu Mahdi (AS).

Maimamu wote wa Ahlibayt pamoja na wafuasi wao waliishi katika hali ya kudhulumiwa, kupigwa, kufukuzwa, kuporwa, haki zao, kuuwawa kwa kuchinjwa kukatwa katwa viungo, kuchomewa nyumba zao moto nk.

Na dhulma zote hizo zilitokana na watawala waliopatikana kwa mfumo ulioanzia Saqifa Banii Saida.

Na Katika mwaka 61 Hijria, ndipo aliposimama Imamu Huseyn akisaidiwa na kizazi chake na watu wa ukoo wake ( Banii Hashim) pamoja na wafuasi wake kuzitowa muhanga roho zao tukufu huko katika ardhi ya karbalaa nchini Iraq, kwaajili ya kuupigiania uislam wa asili uliofundishwa na babu yake Mtume, pamoja na baba yake Imam Amirul muuminiina, Aly Bin Abii Talib

Huku Imamu Husseiyn akisisitiza mara kwa mara kuwa uislamu uliofundishwa na babu yake pamoja na baba yake ndio uislam wa asili na ndio pekee wenye dhamana ya kuwafikisha wanadamu kwenye radhi za Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Mapambano kati ya Imamu Huseyn na yazidi ilikuwa ni mapambano kati ya watetezi wa haki na watetezi wa batili.

Imamu Huseyn ni mjukuu wa Mtume na mteule wa Mwenyezi Mungu alietakaswa na madhambi (33: AHZAB), pia ni Imamu wa tatu kati ya maimamu 12 wa Ahlilbyt aliousia Mtume wafuatwe baada yake, wakati yazid bin Muawiya Bin Abii Sufiyan ni mlevi wa kila aina za pombe, muovu, mzinifu, dhalimu, muuwaji wa waislamu wasiokuwa na hatiya N.k

Imamu Husein alikataa kata kata kutowa ahadi ya utiifu kwa yazidi Bin Muawiya, na ndipo alipoamuwa kupambana na yazidi kwa lengo la kuunusuru uislam na kuurudishia heshima yake, hata kama atagharamika kutoa roho yake tukufu na roho za kizazi chake.

Jeshi la Yazidi lililokuwa na idadi ya watu 30,000 lilifanya mauwaji ya kinyama kwa Imamu Huseyn na kizazi chake, pamoja na wafuasi wake wasiozidi idadi ya watu 72 tu, kwa kuwanyima maji ya mto Furat, uliokuwepo mbele yao, wakati Mayahudi, mbwa na Nguruwe wakiruhusiwa kunywa na kuogelea katika mto huo mbele ya Imamu Husseyn na familia yote ya Mtume na wafuasi wake.

Jeshi hilo la yazidi, liliuwa kizazi hicho cha Mtume na kuwakata kata viungo, kuwachinja shingoni, na kutenganisha baina ya vichwa vyao na miili yao, pamoja na yote hayo, jeshi la Yazidi halikuishia hapo tu. Bali waliuponda ponda mwili mtukufu wa Imamu Huseyn kwa kutumia mafarasi waliobeba watu migongoni mwao.

Na baadae kuiacha miili hiyo mitukufu jangwani huku jeshi hilo likiondoka na vichwa vya watukufu hao na kuvipachika juu ya mikuki na kuvitembeza kila mji huku wakifurahia jambo hilo.
 Mauwaji hayo yalitokea siku ya tareje 10 Mfunguo 4 mwaka 61-Hijiria.

Mwenyezi Mungu awalani watu wote waliomdhulumu Imam Husein, na awalani wale wote walioasisi dhulma hii kwa watu wa nyumba ya Mtume. Laana hizo ziendelee mpaka siku ya Kiyama.

MWISHO