IMAMU HUSSEIN KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI
  • Kichwa: IMAMU HUSSEIN KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 9:51:26 2-10-1403

BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI.

IMAMU HUSSEIN KATIKA NDIMI ZA WAMAGHARIBI

 Edward G. Brown
Sir Thomas Adams Profesa wa lugha ya kiarabu na masomo ya kimashariki katika chuo kikuu cha Cambridge:
" "… ni kumbukumbu ya uwanja uliojaa damu wa Kerbala, ambapo mjukuu wa Mtume alianguka, akateswa na kiu na kuzungukwa na miili ya watu wake waliouwawa, kifo hicho wakati wowote chatosha kuchemsha hisia kali hata za asiyejali, na moyo ambao uchungu, hatari na kifo hupungua na kuwa mdogo mno."
[A Literary History of Persia, London, 1919, p. 227]

Ignaz Goldziher
(1850-1921) Mhangari mashuhuri na msomi wa kimashariki:
" "Tangu siku ile nyeusi ya Karbala, historia ya kizazi hiki…imekuwa ni mlolongo wa kutabika na mateso. Haya huelezwa kwenye mashairi na tungo fasihi za kuhusu kufa shahid - kwenye madhehebu ya Shia - na kufanya majilisi za Shia kuwapo katika mwanzo wa mwezi wa Muharram, ambapo siku ya kumi (a'shura) huwekwa kuwa ni siku maalum ya kumbukumbu ya msiba wa Karbala. Matukio ya janga hilo huwa yanaonyeshwa kwa njia ya ta'aziya. 'Sikukuu zetu ni siku za maombolezi', akitimiza mashairi haya ni amiri wa kuieleza hali ya Mashia akikumbusha mitihani mingi iliyokipata kizazi cha Mtume. Manung'uniko na maombolezo juu ya maovu na mateso waliyofanyiwa kizazi cha Ali, na maombolezo juu ya watu wake waliokufa mashahid: Haya ndiyo mambo ambayo wafuasi wao waaminifu hawawezi kuyaacha. Hata kuna methali isemayo: '..Yahuzunisha zaidi kuliko machozi ya Shia..' imekuwa ni methali itumikayo ya kiarabu."
[Introduction to Islamic Theology and Law, Princeton, 1981, Uk. 179]

Edward Gibbon
(1737-1794) Anayechukuliwa kuwa ni mwanahistoria mkuu wa kiingereza enzi zake:
" "Katika enzi hizo na hali ya hewa ya wakati huo, mandhari ya huzuni ya kifo cha Husein yataamsha hisia za huruma za msomaji asiye na huruma."
[The Decline and Fall of the Roman Empire, London, 1911, Juz. 5, Uk. 391-2] Wala usiwadhani wale waliouwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu (maiti). Bali wa hai, wanaruzukuiwa kwa Mola wao. (Qur'an 3:169)
Wanayosema wasio Waislamu juu ya…
Husein
MRITHI WA TATU WA MTUME MUHAMMAD (Rehma na Amani ziwashukie)
Imam Husein alikuwa ni mjukuu wa Mtume Muhammad, amani ziwashukie, aliyeuwawa shahid na majeshi maovu ya utawala wa kiimla. Ufuatao ni mkusanyiko wa nukuu fupi fupi kuhusu yeye kutoka kwa watu mbalimbali mashuhuri duniani.

Peter J. Chelkowski
Profesa wa elimu ya mambo ya Mashariki ya kati, Chuo kikuu cha New York:
" "Husein alikubali mwito na akaondoka Makka akiwa amefuatana na familia yake na kikosi cha wafuasi wake wapatao sabini. Lakini alipofika ardhi kame ya Karbala, walishtukizwa ghafla na uvamizi uliofanywa na khalifa Yazid. Japokuwa walionekana wazi kushindwa, lakini Husein alikataa kuukubali utawala wa Yazid. Wakiwa wamezingirwa na jeshi kubwa la maadui, Husein na watu wake walikaa bila ya kuwa na maji kwa siku kumi wakiwa katika jangwa lenye joto kali la Karbala. Hatimaye, Husein, watu wazima na baadhi ya wavulana katika familia yake na ya maswahaba wake walikatwakatwa kwa mishale na mapanga ya jeshi la Yazid; wanawake upande wake na watoto waliosalia walitekwa nyara na kupelekwa kwa Yazid mjini Damascus. Mwaandishi mashuhuri wa historia, Abu Rayhan al-Biruni asema: '… kisha moto uliwashwa kwenye kambi zao na miili yao kukanyagwa na kwato za farasi; ambapo katika historia ya mwanaadamu hakuna aliyepata mauaji mabaya kama hayo.'"
[Ta'ziyeh: Ritual and Drama in Iran, New York, 1979, Uk. 2]

Simon Ockley
(1678-1720) Profesa wa lugha ya kiarabu katika chuo kikuu cha Cambridge:
" "Kisha Husein akapanda farasi wake, akaichukua Qur'an na kuilaza mbele yake, akaenda kwa watu na kuwataka watekeleze jukumu lao: akiongeza, 'Ewe Mola, wewe ndiye tegemeo langu katika kila tatizo, na ni tumaini langu katika kila janga!'… Kisha akawakumbusha utukufu wake, heshima ya kuzaliwa kwake, ukuu wa nguvu zake, akasema, 'Hebu fikirieni wenyewe mtu kama mimi niwe ni bora au si bora kwenu; Mimi ni mtoto wa binti ya Mtume wenu, asiye na mfano wake duniani. Ali ni baba yangu; Jaafar and Hamza, viongozi wa mashahid, wote ni ammi zangu; na Mtume wa Mwenyezi Mungu - amani zimshukie - alisema, mimi na ndugu yangu, sisi sote ni viongozi wa vijana wa peponi. Ikiwa mwaniamini niyasemayo ni ya kweli, wallahi, sijasema uongo tangu niwe na fahamu zangu; kwa sababu Mwenyezi Mungu anachukia uongo. Ikiwa hamuniamini, waulizeni maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu [hapa aliwataja], na watawaambia hivyo hivyo. Hebu nirejee nyuma kwa nilicho nacho.' Wakamuuliza, 'Ni nini kilichomzuia asiongozwe na mahusiano yake hayo.' Akajibu, 'Mungu akataza mimi nisiache kupigania haki yangu kiholela tu. Nina sababu ya Mungu ya kupambana na kila mtawala wa mabavu asiyeamini siku ya hisabu.'"
[The History of the Saracens, London, 1894, Uk. 404-5]

Reynold Alleyne Nicholson
(1868-1945) Sir Thomas Adams Profesa wa kiarabu, chuo kikuu cha Cambridge:
" "Husein alianguka, akadungwa na mshale, na wafuasi wake mashujaa wakakatwakatwa wakiwa pamoja naye hadi mtu wa mwisho. Mila ya Muhammad, ambayo daima ilipinga utawala wa Bani Umayya, humzingatia Husein kama shahid, na Yazid kama muuaji wake."
[A Literary History of the Arabs, Cambridge, 1930, Uk. 197 ]

Robert Durey Osborn
(1835-1889) Meja wa Kikosa cha Bengal:
" "Husein alikuwa na mwana mwenye umri wa mwaka mmoja tu aitwaye Abdallah. Alikuwa amefuatana na baba yake katika kuelekea kwenye janga. Huku Husein akiwa ameathiriwa na kulia kwa mwanawe, alimbeba na kumuweka mkononi kwake na akaanza kulia. Wakati huo huo, mtoto alidungwa na maadui na kutobolewaa sikio lake, na kufariki mikononi mwa babake. Husein aliiweka maiti hiyo ndogo ardhini na kusema: 'Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea!' Kisha akalia akisema: 'Ee Mola! Nipe nguvu ya kuvumilia misiba hii!' … Akilemewa na kiu, na amechoka kutokana na majeraha aliyokuwa nayo, alipigana kishujaa sana na kuwaua baadhi ya maadui. Hatimaye alikatwa kutokea upande wa nyuma; akadungwa kwa nguvu mgongoni na kuanguka chini; wakati muuaji wake alipokuwa akiitoa silaha yake, mwanawe Ali alianguka akiwa tayari ameshakufa.

Kichwa ikilikuwa kimeharibiwa kwa kukatwa; na mwili wake usio na kichwa ukakanyagwa na kwato za farasi wa maadui; asubuhi iliyofuata watoto na wanawake waliobaki hai walipelekwa mji wa Koufa. Miili ya Husein na wafuasi wake waliouwawa iliachwa bila kuzikwa pale ilipoanguka. Kwa siku tatu ilibaki ikipigwa na jua na umande wa usiku, na kuvamiwa na tai na wanyama wengineo; lakini kisha wakaazi wa viji vya jirani walihuzunishwa kuwa mwili wa mjukuu wa Mtume uwe katika hali hiyo ya aibu ukiachiwa wanyama wachafu, hivyo hawakujali hasira za Ubaidallah, waliuzika mwili wa shahid huyo na ya marafiki zake mashujaa.
[Islam Under the Arabs, Delaware, 1976, Uk. 126-7]

Sir William Muir
(1819-1905) Msomi Mskochi na kiongozi. Alikuwa waziri wa mambo ya nchi za nje katika serikali ya India na Luteni Gavana wa mkoa wa Kaskazini Magharibi. " "Msiba wa Karbala haukuamua tu majaaliwa ya ukhalifa, bali pia ufalme wa ummah ya Mohammed muda mrefu baada ya ukhalifa kutoweka." [Annals of the Early Caliphate, London, 1883, Uk. 441-2]

MWISHO