FADHILA ZA MWALIMU
  • Kichwa: FADHILA ZA MWALIMU
  • mwandishi: Taqee Zacharia
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 19:10:14 1-10-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

FADHILA ZA MWALIMU
قال الإمام الباقر  علیه السلام
معلم الخیر یستغفر له دواب الأرض،وحیتان البحور،وکلُّ صغیرةٍ وکبیرةٍ فِي أرض اللهِ وسمائه
"Imam Baaqir (a.s) amesema:Mwenye kufundisha (jambo lolote la) kheri,wanyama wa ardhini humuombea maghfira (au msamaha kwa Mwenyeezi Mungu -s.w-),na wanyama wa baharini,na chochote kile kinachopatikana katika ardhi ya Mwenyeezi Mungu au katika mbingu yake,sawa sawa kile kidogo sana au kikubwa,humuombea maghfira na msamaha."

Ufafanuzi wa hadithi hii:
Hadithi hii,inaonyesha umuhimu wa Mwalimu na fadhila kubwa alizonazo mbele ya Mwenyeezi Mungu (s.w),hadithi inasema kwamba: viumbe wote wa Mwenyeezi Mungu (s.w) wanaopatikana ardhini na mbinguni,humuombea msamaha na maghfira Mwalimu huyu.Lakini si kila mwalimu hufanyiwa hivyo!,bali yule tu mwenye kufundisha na kuelimisha jambo lolote lile la kheri,ama yule mwenye kupotosha akidai kwamba anafundisha au anaelimisha,kumbe anawapeleka watu njia isiyokuwa yenyewe na hatimaye kuwapoteza,huyo hapati uombezi huu wa maghfira kutoka kwa kila kiumbe cha Mwenyeezi Mungu (s.w) bali hupata kinyumbe chake.

Tunawapongeza Walimu wote duniani wenye kufundisha na kuelimisha yaliyokuwa ya kheri katika "Siku hii ya Mwalimu" ambayo pia ni siku aliyo kufa kishahidi Shahidi Mutwahhariy ambaye alikuwa Mwalimu mwenye juhudi,alipigana vita na maadui wa Waislaam na Uislaam,kwa kutumia kalamu yake ambapo maadui wa Uislaam walishindwa kupambana na kalamu ya Shahidi Mutwahhariy na hii ni kwasababu watu wengi sana waliikubali sana fikra ya Shahidi na mawazo yake kupitia kuvisoma vitabu vyake ambavyo vilitarjumiwa au kufasiriwa katika lugha mbali mbali na kusambaa kote ulimwenguni.Maadui hao wakaamua kumuua kwa kutumia bunduki badala ya kupambana naye kwa kutumia kalamu kama alivyokuwa akipambana nao.Historia kamwe haiwezi kumsahau Shahidi Mutwahhariy na watu kama Shahidi Mutwahhariy.Na siku hiyo aliyouwawa kishahidi Shahidi Mutwahhariy,hujulikana kama siku ya Mwalimu.
MWISHO