IBADA ZA VITENDO
  • Kichwa: IBADA ZA VITENDO
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 18:50:1 2-10-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

IBADA ZA VITENDO
1) Kusimamisha Sala

MwenyeziMungu anasema:
"Wala hawakuamrishwa ila kumwabudu MwenyeziMungu kwa kumtakasia dini, wawache dini za upotofu (upotevu) na wasimamishe Sala na kutoa Zaka, hiyo ndio dini iliyo sawa . (Suratul - Bayyinah - 5)

Na anasema katika kuelezea wasfu wa walioamini: "Watu ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi (hakuwasahaulishi) kumkumbuka MwenyeziMungu na kusimamisha Sala na kutoa Zaka, wanaiogopa siku ambayo nyoyo zitadahadari na macho pia", (An - Nur -37).

Na anasema:
"Wale ambao tukiwamakinisha (tukiwaweka uzuri) katika ardhi, husimamisha Sala na wakatoa Zaka na Wakaamrisha yalio mema na Wakakataza yalio mabaya. Na marejeo ya mambo ni kwa MwenyeziMungu". (Al - Hajj - 41). Na anasema:-
"Na waamrishe watu wako kusali na uendelee mwenyewe kwa hayo. Hatukuombi riziki bali Sisi ndio tunaokuruzuku na mwisho mwema utawathubutukia wamchao Mungu." (Taha - 132)

2) Kutoa Zaka

MwenyeziMungu anasema:-
"Wala hawakuamrishwa ila kumuabudu MwenyeziMungu kwa kumtakasia dini, wawache dini za upotofu(upotevu) wasimamishe Sala na watoe Zaka hiyo ndiyo dini iliyo sawa . (Suratul - Bayyinah -5).

Na anasema:-
"Na simamisha Sala na toeni Zaka na kheri mtakazozitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtazikuta kwa MwenyeziMungu ………" (Al Baqarah - 110)

Na anasema:-
"Lakini wale waliozama barabara katika elimu miongoni mwao (hawa waliopewa kitabu) na Waislamu (ambao wote hao) wanaamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako, na (wale) wanaodumisha Sala na kutoa Zaka na wanaomwamini MwenyeziMungu na (wanaamini) Siku ya mwisho. Hao tutawapa malipo makubwa ". (An - Nisaa -162)

2) Kufunga mwezi wa Ramadhani

MwenyeziMungu anasema:-
"Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuja kabla yenu ili mpate kumcha Mungu". (Al - Baqarah -183).
Na anasema:-
"(Mwezi huu mlioambiwa mfunge) ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika (mwezi) huo hii Qurani ili iwe uwongozi kwa watu na hoja zilizo wazi wa uwongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batil) atakae kuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge." (Al - Baqarah - 185)

Na Mtume (SAW) amesema:-
<>. Bukhari, Muslim, Abu Daud, Attirmdhyna, Ibni Majah,na Ahmad

4) Kuhiji Makka (Kaaba) Kwa Mwenye Uwezo

MwenyeziMungu anasema:-
"Na MwenyeziMungu amewawajibishia watu wafanye Hijja katika nyumba hiyo; yule awezaye kufunga safari kwenda huko na atakae kanusha (asende na hali ya kuwa anaweza ) basi MwenyeziMungu si mhitaji kuwahitajia walimwengu " Aal - Imran -97).

Na anasema :-
"Na (tukamwambia) "Utangaze kwa watu habari za Hijja watakujia (wengine) kwa miguu na wengine juu ya kila mnyama aliyekonda (kwa machofu ya njiani) wakija kutoka njia ya mbali". (Al - Hajj - 27).
Na Mtume (SAW) akasema :-
<>. Bukhari na Muslim

2) Kuhukumu Kwa Sheria Iliyoteremshwa na MwenyeziMungu

Hana haki mtu yeyote ya kuwawekea wanadamu sheria, isipokuwa yule Aliyewaumba - Subhanahu wa Taala. MwenyeziMungu anasema:- "Fahamuni kuumba (ni kwake tu MwenyeziMungu) na amri zote ni zake (MwenyeziMungu) ametukuka kabisa MwenyeziMungu Mola wa walimwengu wote". (Al -Aaraf 54).

Kwa hivyo mwenye kujipa yeye mwenyewe, au kumpa mtu mwengine haki ya kuwatungia wanadamu sheria na nidhamu ambazo MwenyeziMungu hajazitolea amri yake, atakuwa ametenda kitendo cha shirki na atakuwa amewalingania watu wamwabudu asiyekuwa MwenyeziMungu.
MwenyeziMungu anasema:-
"Oh! Wana washirika wa (MwenyeziMungu) waliowawekea dini asiyoitolea MwenyeziMungu ruhusa (yake)?" (Ashuraa - 21) Na anasema:-
"Haikuwa hukumu ila hii ya MwenyeziMungu tu; ameamrisha msimuabudu yeyote yule isipokuwa Yeye tu". Yussuf -40

Kwa hivyo Mwislamu anatakiwa asalimu amri mbele ya sheria ya MwenyeziMungu na aitii sheria hiyo kwa nafsi iliyoridhika. MwenyeziMungu anasema:- "Naapa kwa haki ya Mola wako, wao hawawi wenye kuamini (kweli kweli) mpaka wakufanye (wewe ndie) hakimu (mwamuzi) katika yale wanayokhitilafiania kisha wasione uzito nyoyoni mwa juu ya hukumu uliyoitoa, na wanyenyekee kabisa." (AN - Nisaa -65)

3) Kuipigania Dini Ya MwenyeziMungu

"Enyi mlioamini! Jee! nikujulisheni juu ya biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo? (Basi biashara yenyewe ni hii): Muamini MwenyeziMungu na Mtume wake piganieni dini ya MwenyeziMungu kwa hali zenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu ikiwa mnajua (kuwa ni bora basi fanyeni)". (As - Saff -10 11)

Na anasema:
"Jee! Mnadhani mtaingia Peponi hali MwenyeziMungu hajapambanua wale waliopigania dini ya MwenyeziMungu miongoni mwenu, na kuwapambanua wale walofanya subira?" (Aal - Imran - 142)

4) Kuweka Nadhiri Kwa Ajili Ya MwenyeziMungu.

MwenyeziMungu anasema:
"Wanaotimiza wajibu (wao) (Nadhiri walizoziweka) na wanaoigopa siku ambayo shari yake itaenea (sana)". (Ad - Dahr -7) Na Mtume (SAW) amesema:-
(Bukhari, Ahmad, Attirmdhy na wengine na imepokewa kutoka kwa Bibi Aisha (RA). 5) Kutufu Nyumba Tukufu Ya MwenyeziMungu:
MwenyeziMungu anasema:-
"Na tulimuusia Ibrahim na Ismail (tukawaambia): "Itakaseni (isafisheni) nyumba yangu kwa ajili ya wale wanaozunguka kwa ajili ya kutufu na wanaokaa hapo na (kwa ajili ya) wanaorukuu na kusujudu hapo pia". (Al - Baqarah - 125)

Na anasema:-
"Na waizunguke nyumba ya kale (Nyumba kongwe Al-Kaaba)". (Al - Hajj -29)
6) Kuchinja Kwa Ajili Ya MwenyeziMungu

MwenyeziMungu anasema:-
"Sema hakika Sala zangu na Ibada zangu (zote nyengine) na uzima wangu na kufa kwangu (zote) ni kwa MwenyeziMungu. Mwumba wa walimwengu wote. (Likinisibu jambo limenisibu kwa kutaka MwenyeziMungu. Si kwa kutaka viumbe vyake, na yote ninayofanya nafanya kwa ajili yake) Hana mshirika wake, na haya ndiyo niliyoamrishwa na mimi ni wa kwanza wa waliojisalimisha (kwa MwenyeziMungu)". (Al - Anam -162-163)

Na kuchinja ni miongoni mwa ibada maana MwenyeziMungu anasema:- "Basi Sali kwa ajili ya Mola wako na Uchinje (kwa ajili ya Mola wako). (Na kila utakalolifanya lifanye kwa ajili ya Mola wako siyo mizimu wala mapango wala makaburi )." (Suratul - Kawthar - 2)

MWISHO