UCHOCHEZI NA FITINA
  • Kichwa: UCHOCHEZI NA FITINA
  • mwandishi: BARAZA
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 22:23:19 6-10-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

UCHOCHEZI NA FITINA

Licha ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufanya juhudi za pande zote na pia wasomi na wanafikra wa ulimwengu wa Kiislamu kuchukua hatua muhimu za kuleta umoja miongoni mwa Waislamu katika pembe mbalimbali za dunia, kwa bahati mbaya bado inasikika sauti ya fitina na mifarakano kutoka kwa baadhi ya watu na nchi zisizopenda kuona umoja na utulivu ukidumishwa katika umma wa Kiislamu.

Bila shaka sauti hii haitakuwa na manufaa ila kwa maadui wa Uislamu. Ni wazi kuwa sauti hii ni hatari kubwa inayopasa kuleta muamko miongoni mwa Waislamu na kuwafanya waepuke kutumbukia kwenye shimo la fitina na mifarakano. Je, ni kwa hoja gani juhudi za miaka mingi za kuleta umoja na mshikamano kati ya Waislamu, zilizofanywa na wasomi pamoja na wanafikra wakubwa wa Kiislamu wakiwemo Sayyid Jamal, Sheikh Shaltut na Imam Khomeini zimechukuliwa kuwa mchezo na baadhi ya watu ambao wanajichukulia kuwa ndio walio kwenye njia ya haki na kuwatuhumu waumini kwa mambo yasiyo na msingi, bila ya kuwa na hoja yoyote ya maana?

Ni wazi kuwa Mawahabi wa Saudi Arabia wameazimia kuwahudumia kwa nguvu zao zote maadui wa umoja wa Uislamu, na hakuna njia nyingine yoyote ya kufikia lengo hilo isipokuwa kuchochea fitina na mifarakano katika jamii ya Kiislamu.

Habari za hivi karibuni zinasema kuwa katika taarifa yao ya kichochezi ya hivi karibuni, mamufti 42 wa Kiwahabi wa Saudi Arabia wametoa fatuwa wakitahadharisha juu ya kile wamekitaja kuwa hatari ya hilali ya Kishia! Kwa mujibu wa tovuti ya ar-Raswid, viongozi hao wa Kiwahabi wamedai kwamba Iran inachochea vita dhidi ya ufalme wa Saudia na kuituhumu kwamba inataka kueneza na kuimarisha kile wamekitaja kuwa fikra ya shirk nchini humo.

Mamufti hao wanaowakufurisha Waislamu, wamewatahadharisha Waislamu kuhusiana na kile kinachotajwa kuwa hilali ya Kishia, na kuwataka wakabiliane na suala hilo kupitia hatua za kiusalama na kipropaganda. Waliotia saini taarifa hiyo ya mamufti 42 wa Kiwahabi, ni pamoja na Sheikh Nassir al-Umar ambaye anatajwa na wapinzani wa Saudia kuwa 'Hitler wa Waarabu' kutokana na matamshi yake ya kichochezi dhidi ya madhehebu ya Kiislamu na hasa Ushia.

Mamufti hao ni watu ambao kufuatia kulipuliwa kwa mabomu makaburi ya Maimamu Askariyein (as) nchini Iraq, walitoa taarifa ya fitina wakiwataka magaidi wazidishe vitendo vyao vya mauaji na mifarakano ya kimedhehebu na kikabila miongoni mwa Waislamu. Katika taarifa yao ya hivi karibuni mamufti hao wachochezi wamedai kuwa wapiganaji wa kundi la al-Huthi nchini Yemen wanataka kuleta utukufu wa waovu na kuzidisha mashinikizo dhidi ya watu wema nchini humo!!

MWISHO