KUYAHUDISHWA KWA AQSA
  • Kichwa: KUYAHUDISHWA KWA AQSA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 22:31:44 6-10-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

KUYAHUDISHWA KWA AQSA

Viongozi wa Palestina wametahadharisha juu ya njama zinazofanywa na Wazayuni za kubomoa na kuharibu nyumba za Wapalestina katika mji unaoukaliwa kwa mabavu wa Quds kwa ajili ya kuufanya mji huo kuwa wa Kiyahudi.
Kwa mujibu wa ripoti ya televisheni ya al-Alaam viongozi wa Palestina wanasema kuwa kitendo hicho ni sawa na kutangazwa vita, mauaji ya kizazi na jinai za kivita dhidi ya Wapalestina. Wanasisitiza kwamba, siasa hizo za Wazayuni zinahatarisha kizazi kizima cha Wapalestina katika mji huo mtakatifu.

Kuhusiana na suala hilo, Maad az-Zatari, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya al-Maqdis ameiambia televisheni ya al-Alaam kwamba, utawala wa Israel unatekeleza siasa za kubomoa na kuharibu nyumba za Wapalestina wanaoishi katika mji wa Quds ili kuwalazimisha kuondoka katika mji huo na hivyo kutoa fursa ya kufanywa kuwa wa Kiyahudi.
Kwa mujibu wa ripoti ya al-Alam, Meya wa Kizayuni wa mji wa Quds ametoa amri ya mabuldoza ya utawala wa Israel kubomoa makumi ya nyumba za Wapalestina wasio na hatia katika mji wa huo ili kuwafukuza kabisa Waislamu wa Palestina katika mji huo. Utawala huo umekusudia kubomoa nyumba 220,000 za Wapalestina katika mji huo unaoukaliwa kwa mabavu.

MWISHO