ATHARI YA UISLAMU NDANI YA UINGEREZA
  • Kichwa: ATHARI YA UISLAMU NDANI YA UINGEREZA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 22:32:15 6-10-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

ATHARI YA UISLAMU NDANI YA UINGEREZA

Waziri wa Sheria wa Uingereza amesema kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamekuwa na athari kubwa katika ulimwengu wa Kiislamu na kwamba athari hizo pia zinaonekana miongoni mwa Waislamu wa Uingereza.

Akizungumza katika mazungumzo ya meza duara yaliyokuwa yakijadili mchango wa Waislamu katika jamii ya Uingereza, Jack Straw amesema kuwa athari za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu mwishoni mwa muongo wa sabini zilihisika pia nchini Uingereza ambapo Waislamu wa nchi hiyo pia walijihisi kuwa na nguvu.

Katika sehemu nyingine, Straw amesema kuwa Waislamu, Wakristo na Mayahudi wanapasa kuimarisha uhusiano wao na kwamba serikali ya London inapasa kusisitiza umuhimu wa suala hilo kupitia vyombo vya habari. Hata hivyo Straw amedai kwamba Uislamu umekuwa ukitumiwa vibaya na baadhi ya makundi ya kisiasa katika miongo ya hivi karibuni.

Kuhusiana na matamshi hayo, Baraza la Waislamu wa Uingereza lililazimika kutoa taarifa siku ya Alkhamisi likisema kuwa Waislamu wamekuwa na mchango mkubwa na wa muda mrefu katika jeshi la nchi hiyo na hasa katika kipindi cha Vita vya Kwanza vya Dunia. Muhammad Abdul Bari, Katibu Mkuu wa baraza hilo amesema kuwa, Waislamu wa Uingereza wamekuwa na mchango mkubwa katika kueteta nchi hiyo na kwamba kama walivyo raia wengine wa nchi hiyo, wanapinga vita va uvamizi wa kigeni nchini Afghanistan. MWISHO