MTAZAMO WA HIZBU TAHRIIR
  • Kichwa: MTAZAMO WA HIZBU TAHRIIR
  • mwandishi: HIZBU TAHRIIR
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 19:39:46 1-10-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

MTAZAMO WA HIZBU TAHRIIR
WAJIBU WA SHERIA KATIKA JAMII
Ushahidi wa Faradhi ya Khilafah
Uisilam umerejeshwa kuwa ni dini tu ya nchi na usekula umefanywa kuwa ndio itikadi ya kuendeshea maisha. Makafiri wamefanikisha katika kuitenganisha dini na dunia na kutenganisha mfumo wa utawala wa Ukhalifah katika maisha na akili za Waisilamu..

"Lazima tuufishe chochote amabcho kitajaribu kuujenga tena Ummoja Kiisilam kwa kizazi cha Waisilam. Kama tulivyofanikisha kuumaliza utawala wa Khilafah, hivyo ni lazima tuhakikishe kuwa ummoja wa Waisilam haufufuki tena, ikiwa ni kifikra au kielimu." Maneno ya Waziri wa Nje wa Uingereza akimwambia hayo kwa Waziri Mkuu wake kabla ya vita vya pili vya dunia.

"Hali halisi sasa ni kuwa Uturuki imekufa na haitofufuka tena, kwa sababu tumeiangamiza nguvu yake, Khilafah na Uisilam". Maneno ya Lord Curzon, Waziri wa Nje wa Uingereza aliyoyanukuu mbele ya baraza la Wakilishi baada ya mkataba wa Lausanne wa tarehe 24/07/1924.

Hivi kweli ni ajabu leo hii kuwa Waisilam hawajui chochote kuhusiana na mfumo wao wa kweli wa utawala? Kuwa hawajawahi kabisa kusikia neno hilo hata kutajwa katika mazungumzo na harakati za kuufufua ummah? Waingereza kweli wamefanikiwa kutuelimisha hadi kufikia kuwa tunaukimbilia mfumo wao wa utawala na kuutupa mbali mfumo wetu wa haki uliotokana na dini yetu hii ya Uisilam. Hivyo basi, ni nini hii Khilafah? Na kwa nini ni muhimu katika Uislam?

Mwenendo ambao unaowezesha sisi kuishi kwa Uisilam ni kuwepo kwa Utawala wa Khilafah. Huu ni mfumo ulio sawa sawa kama Khilafah zilizotutnagulia za Khilafah Rashida uliozisimamisha sheria za Allah (swt), ulikuwepo mpaka mnamo tarehe 03/03/1924 ulipo pinduliwa na Kibaraka wa Uingereza, masaliti wa Ummah, Mustafah Kemal wa Uturuki. Mtume (saw) alisema: "Fundo za Uisilam zitakatwa moja baada ya moja mpaka zote zitakwisha. Fundo la kwanza kukatwa litakuwa ni la utawala na mwisho litakuwa ni fundo la sala". (Musnad wa Imam Ahmed)

FARADHI YA UKHALIFA
Aya za Qur'aan Tukufu:
Allah (SWT) anasema kuwa:
فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لاَ يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا )  النساء: 65)

1. " Naapa kwa (Haki ya) Mola wako, wao hawawi wenye kuamini kikweli mpaka wakufanye wewe (Mtume) ndie hakimu katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyotoa, na wanyenyekee kabisa ". (TMQ 4:65). إِ
نَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللَّهُ وَلاَ تَكُنْ لِلْخَائِنِينَ خَصِيمًا ) النساء: 105)
2. " Hakika Tumekuteremshia Kitabu (hiki), hali ya kuwa kimeshikamana na haki ili upate kuhukumu baina ya watu kama alivyokufahamisha Mwenyezi Mungu; wala usiwe mwenye kuwatetea wale wafanyao khiyana ". (TMQ 4:105).
وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الْكَافِرُونَ )  المائدة: 44
3. "Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri". (Al-Maaida: 44)
وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ ) المائدة: 45
4. "Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha mwenyezi Mungu, basi hao ni madhalimu." (Al-Maaida : 45)
وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الْفَاسِقُونَ) المائدة: 47
5. "Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ni mafasiki (waasi)." (Al-Maaida: 47)
وَأَنْ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلاَ تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَنْ يَفْتِنُوكَ عَنْ بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ
6. " Na hukumu baina yao kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe jihadhari nao wasije kukugeuza na baadhi ya yale aliyoteremshia Mwenyezi Mungu ." (Al-Maaida:49).

Aya hizi za Qur'an na zingine nyingi, ni ushahidi usio na shaka wa wajibu wa kuhukumiana kwa sheria alizoziteremsha Allah (swt). Aya ya mwanzo hasa inawalengea na kuwarejesha Waisilam moja kwa moja kuwa hatuwezi kuwa na imani ya kweli mpaka tuzifanye sheria za Allah (swt) kuwa ni kiamuzi, muongozo wa mambo yetu yote kama sheria za kiuchumi, kijamii, kielimu, mahakama na utawala. Hii ni unesho kuwa ni wajibu (faradhi) kwa Waisilam kusimamisha utawala wa kisheria za Allah (swt) kwani mtu au jamii pekee bila ya Uongozi haiwezikufanikisha wajibu hizo.

Hadithi za Mtume (saw):
Miongoni mwa hadithi za Mtume Muhammad (saw) zinazoelezea juu ya Faradhi hii ni kama: 1. Imam Muslim anasimulia kutoka kwa Abu Hazim ambaye alisema kuwa: "Nilikuwa na Abu Huraira kwa miaka mitano na nilimsikia akisimulia ya kuwa Mtume (saw) alisema:
كا نت بنو اسرائيل تسوسهم الا نبياء كلما هلك نبي خلفه نبي وأنه لا نبي بعدي وستكون خلفاء فتكثر
قالوا فما تأمرنا يا رسول الله قال فواببيعة الأول فالأولا وأعطوهم حقهم فإن الله سألهم عما أسترعا هم
" Mitume ilikuwa ikitawala ukoo za Wana wa izraili. Kila anapokufa Mtume, mwingine huchukuwa nafasai yake, lakini hakutokuwa na utume badala yangu badala yake kutakuwa na Makhalifah na watakuja wengi". Masahaba waliuliza, unatuamuru tufanye nini? Timizeni utiifu wenu kwao mmoja baada ya mmoja. Wapeni haki zao za (uongozi), kwani hakika Mwenyezi Mungu atawauliza juu ya majukumu yao aliyowapa ".

Hadithi hii ni kauli iliyowazi ya ukweli wa kuwepo kwa serikali katika Uisilam baada ya Mtume (saw) ni serikali ya Ukhalifah na si serikali ya kijamuhuri (Republican) au serikali ya ujamaa (socialist) au serikali ya Ufalme (Sultanat) au serikali ya kidemokrasia. Ufahamu huu unashikamana na ushahidi mwingi wa hadithi tofauti za Mtume (saw) ambazo zinaonesha kwa uwazi kuwa utawala uliokubalika katika uisilam ni utawala wa Ukhalifah peke yake.

2. Imam Muslim amesimulia kutoka kwa Abdullah bin Omar ambaye amesema kuwa Mtume (saw) amesema ya kuwa:
وَمن مَاتَ وَلَيسَ فِى عُنِقه بَيعَة مَاتَ مِيتَةً جَا هِلِيةِ
"Yeyote atakaye kufa bila ya kuwa na kiapo cha utiifu (ba'ya) kwa Kiongozi (Khalifah) atakua amekufa kifo cha kijahiliya". 3. Ahmed and Ibn Abi'Asim wamesimulia kutoka kwa Mtume (saw) ya kuwa: "Yeyote atakaye kufa bila ya kuwa na Kiongozi katika uhai wake, atakuwa amekufa kifo cha kijahiliya". Mtume (saw) amewajibisha kwa kila Muisilam kuwepo kwa uongozi (Khalifa) katika maisha yake, jambo ambalo linawakilishwa kwa kuwepo kwa kiapo cha utiifu (ba'ya) kwa kiongozi. Kwani kiapo hicho hapewi mtu yeyote isipokuwa Khalifah. Hadithi yatuonesha kuwa anaetakiwa kuwaongoza Umma wa Waisilam ni Khalifah au kwajina lingine hujulikana kwa Imam au Amiri Muuminina. Hii ni dalili ya kuwepo kwao an utelifu wao.

Kauli za Masahaba:
Ali ibn Taalib (r.a) amesema kuwa "Watu hawato sawawika bila ya kuwepo kwa Imam (khalifah), ima awe ni mbaya au mzuri". (Bayhaqi: 14286, Kanz ul-ummal) Abdullah bin Omar (r.a) amwsema kuwa "Umma hauto taabika hata kama watakauwa ni madhalim wa nafsi zao na waovu ikiwa viongozi wao wameongoka na wanawaongoa. Lakini umma utataabika na kupotea hata kama wataongoka na kuongoa ikiwa viongozi wao ni madhalim na waovu". (Nakala ya Abu Nu'aim katika Hulayat Awliyyah)

Omar bin Al-Khatab (r.a) amesema kuwa :
لاإسلام بلاجماعة ولاجماعة بلاإمارة ولا إمارة بلا سمع و طاع
" Hakuna Uisilam bila ya kuwepo kwa umoja wa Umma, na hakutokuwa na ummoja bila ya kuwepo kwa Uongozi, na hautokuwepo uongozi bila ya kuwepo kwa usikilivu na utiifu kwa (Uongozi) ".

Kauli za Maulamaa:
Imam al-Qurtubi (rh.a) amesema katika Tafsiri yake ya Qur-an kuhusiana na aya hii:
إِنِّي جَاعِلٌ فِي الأَرْضِ خَلِيفَة
"Mimi nitajaalia katika ardhi Msimamizi, Kiongozi (Khalifah)". (Al-Baqarah:30)
هذه الأية الأسأل فى نسب إمام وخليفة يسمعوله ويطاعو لتجتمعى به إ لا كلمة وتنفذو به الأحكام الخليفة
ولاخلاف فى وجوب ذالك بين الأمة ولابين الأإمة إلا ما روي أن الأسم المعتزل
"Aya hii ni chanzo cha kuteuliwa kiongozi (Imam, Khalifah), ambaye ni wajibu juu yake kusikilizwa na kutiiwa, ulimwengu umejiunga chini yake na sheria (ahkam) za Kalifah zinasimamishwa na yeye na hakuna tofauti kwa hilo na wajibu wa umma kwake wala kwa maimam wote isipokuwa kwa yaliyosemwa na Al-Asam, Mu'tazilli (kundi lilopotevu).." (Tafsiri ul-Qurtubi 264/1).

Imam al-Qurtubi (rh.a) amesema pia: "Khalifah ni nguzo ambayo nguzo zingine husimamishwa nayo". Imam an-Nawawi (rh.a) amesema:
إجمعو على أنه يجب على المسلمين نسب خليفة
"Maulamaa wamekubaliana kuwa ni wajibu kwa waisilam kumchagua Khalifah wao". (Sharhu Sahih Muslim ukurasa 205 vol 12). Imam al-Ghazali (rh.a) alipokuwa anaandika kuhusiana na hatima ya ukosefu wa Khalifah amesema kuwa: "Mahakim wataondoshwa, Mawalii wataondoshwa….amri ya walio na uongozi hazitofuatwa na watu watakuwa ukingoni mwa haram". (Al-Iqtisaad fil Itiqaad ukurasa 240). Ibn Taymiyya (rh.a) amesema:
يجب عن يعرف أن ولاية أمر الناس من عضم واجبات الدين بالا قيام الدين ألابها
" Ni wajibu kujuwa ya kuwa ofisi ya uongozi wa watu (Khilafah) ni moja ya wajibu mkubwa katika dini. Ukweli ni kuwa dini haisimami bila ya Uongozi… huu ndio mtazamo wa Salaf kama al-Fadl ibn Iyaad, Ahmed ibn Hanbal na wengineo". (Siyaasah Shariyyah - chapter : Wajibu wa utiifu kwa Kiongozi).

Imam abu ul-Hasan al-Mawardi (rh.a.) amesema,
عقض الإمامة لى من يقوم بها فى الأمة وجب بالإجماع
"Kuwepo kwa Mkataba wa utiifu kwa kiongozi (imam), ni wajibu kwa umma (ijmaa) kukubaliana". (al-Ahkam us-Sultaniyyah [Arabic] p 56.) Imam Ahmed (rh.a.) amesema:
الفتنة أذا لم يكن أمام يقوم بالأمرالمسلمين
kumaanisha ya kuwa, "Machafuko (Fitina) hutokea pindipo hapatokuwepo kiongozi (Imam) kusimamia mahitajio ya watu". Abu Hafs Umar al-Nasafi (rh.a.) mwanazuoni maarufu wa karne ya sita Hijiri alisema: "Waisilamu ni lazima wawe na kiongozi (Khalifah), ambaye atasimamisha sheria, kusimamisha hudud za Allah (swt), atakaye ihami ardhi ya Waisilam, atakaye liimarisha jeshi, atakaye kusanya zakka, atakaye waadhibu wote watakao ipinga dola, wote watakao peleleza kinyume na dola, atakaye simamisha sala ya Ijumaa na Eid mbili, atakaye tatua mizozo baina ya waja wa Mungu, atakaye kubali kiapo cha mashahidi katika kuitetea haki na uadilifu, kuwaozesha vijana na masikini wasiokuwa na familia na uwezo na ndie atakaye gawanya zakka kwa wanaohitajia".

Imam Al-Juzayri, mtaalamu wa Fiqhi wa maimamu wa madhahebu nne amesema kuhusiana na ma-imamu wanne hao kuwa: "Ma-imam wanne (Shafi, Hanafi, Maliki na Hanbali (r.a.h) wamekubaliana kuwa Kiongozi (khalifah) ni wajibu, na Waisilam ni lazima wamchaguwe Kiongozi (khalifah) ambaye atsimamisha mwenendo wa dini na kuwapa haki zao wanaodhulumiwa kutoka kwa madhalimu". (Fiqh ul-Madhahib ul- Arba'a, volume 5, kurasa 416).

Imam al-Haythami amesema,
أعلم أن صحابة رضي الله عنهم أجمعو على أن نسب ألإمامة بعد إنقراض زمان النبوى
بالجعلواه أهم واجبات حيث أشتغلو به عن دفن رسول الله واجب
"Inafahamika wazi kuwa Masahaba (r.a.h) walikubaliana kumchaguwa kiongozi (khalifah) baada ya kumalizika kwa Utume ni Wajibu. Na walilifanya jambo hilo kuwa ni la muhimu zaidi kuliko wajibu zingine kama maziko ya Mtume (saw)". (A-Haythami katika Sawaa'iq ul-haraqah:17). Allah (SWT) ni mjuzi zaidi
MWISHO