KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU NDANI YA QUR_ANI
  • Kichwa: KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU NDANI YA QUR_ANI
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 20:17:49 19-8-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU NDANI YA QUR-ANI

NJIA ZA KUMFAHAMU MWENYEENZI MUNGU 2

katika makala iliyopita (makala namba moja ) tulielezea nyenzo zinazomuongoza mwanaadamu katika kumfahmu Mwenyeezi mungu. katika sehemu hii ya pili tutaendelea kuzielezea nyenzo hizo na kuzithibitisha kwa aya za qur_ani.

DALILI ZA KIAKILI.

Hivi kweli kiarabu hiki cha Qur-ani yuko binaadamu anayeweza kukiandika au kukisema?

Ndani ya kitabu kitukufu cha Mwenyeezi Mungu kuna aya nyingi za Qur-ani kariym zinazomtaka mwanaadamu afikiri kiakili na awe makini . Miongoni mwa aya hizo ni hizi zifuatazo:-

Madhalimu kweli hawa- kama ilivyo katika aya ya 17- wa nafsi zao na kuwadhulumu viumbe wengine wanaowapoteza makusudi. Sio kama wanavyodai baadhi yao, na tunathibitisha hayo kutokana na aya hizi zifuatazo:-

والَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِمَا اُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا اُنزِلَ مِن قَبْلِكَ وَبِالآخِرَةِ هُمْ يُوقِنُونَ[1]

Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo.

وَلِلّهِ الْمَشْرِقُ وَالْمَغْرِبُ فَاَيْنَمَا تُوَلُّواْ فَثَمَّ وَجْهُ اللهِ إِنَّ اللّهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ[2]

Na mashariki na magharibi ni za Mwenyezi Mungu. Basi kokote mnako elekea, huko Mwenyezi Mungu yupo. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa na Mjuzi.

صِرَاطَ الَّذِينَ اَنعَمتَ عَلَيهِمْ غَيرِ المَغضُوبِ عَلَيهِمْ وَلاَ الضَّالِّينَ[3]

7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.

يَا قَوْمِ لا اَسْاَلُكُمْ عَلَيْهِ اَجْراً إِنْ اَجْرِيَ إِلاَّ عَلـٰي الَّذِى فَطَرَنِى اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[4]

Enyi watu wangu! Sikuombeni ujira kwa ajili ya haya. Haukuwa ujira wangu ila kwa Yule aliye niumba. Basi hamtumii akili?

وَمَا اَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلاَّ رِجَالاً نُّوحِى إِلَيْهِم مِّنْ اَهْلِ الْقُرَي اَفَلَمْ يَسِيرُواْ فِى الاَرْضِ فَيَنظُرُواْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَدَارُ الآخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ اتَّقَواْ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[5]

Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipo kuwa wanaume tulio wafunulia wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Je! Hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ni bora kwa wamchao Mungu. Basi hamfahamu?

لَقَدْ اَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ كِتَاباً فِيهِ ذِكْرُكُمْ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[6]

Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?

وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلاَّ لَعِبٌ وَلَهْوٌ وَلَلدَّارُ الآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[7]

Na maisha ya dunia si chochote ila ni mchezo na pumbao tu. Na hakika nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanao mcha Mungu. Basi, je, hamtii akilini?

اَتَاْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبِرِّ وَتَنسَوْنَ اَنفُسَكُمْ وَاَنتُمْ تَتْلُونَ الْكِتَابَ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[8]

Je! Mnawaamrisha watu mema na mnajisahau nafsi zenu, na hali nyinyi mnasoma Kitabu? Basi je, hamzingatii?

Maelezo kuhusiana na aya

Baadhi ya wanavyuoni wa Kiyahudi wakisilimu jamaa zao wakapata habari, huwaendea kwa siri wakawaambia “ Dini hii mliyoifuata aliyokuja nayo nabii Muhammad ni haki, shikamaneni nayo; lakini sisi hatuwezi kukosa ukubwa wetu” ndiyo Mwenyeenzi Mungu anawasimanga kwa aya hii.

إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآناً عَرَبِيّاً لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ[9]

Hakika Sisi tumeifanya Qur'ani kwa Kiarabu ili mfahamu.

قَالَ رَبُّ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَا إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ[10]

(Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini.

يَا اَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تُحَآجُّونَ فِى إِبْرَاهِيمَ وَمَا اُنزِلَتِ التَّورَاةُ وَالإنجِيلُ إِلاَّ مِن بَعْدِهِ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[11]

Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake? Basi hamzingatii?

اعْلَمُوا اَنَّ اللهَ يُحْيِى الاَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ[12]

  Jueni kwamba Mwenyezi Mungu huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Tumekubainishieni Ishara ili mpate kuzingatia.

فَقُلْنَا اضْرِبُوهُ بِبَعْضِهَا كَذٰلِكَ يُحْيِى اللّهُ الْمَوْتَي وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ[13]

Tukasema: Mpigeni kwa kipande chake (huyo ng'ombe). Ndivyo hivi Mwenyezi Mungu huwahuisha wafu; na anakuonyesheni Ishara zake ili mpate kufahamu.

كَذٰلِكَ يُبَيِّنُ اللّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ[14]

وَإِذَا لَقُواْ الَّذِينَ آمَنُواْ قَالُواْ آمَنَّا وَإِذَا خَلاَ بَعْضُهُمْ إِلَيَ بَعْضٍ قَالُواْ اَتُحَدِّثُونَهُم بِمَا فَتَحَ اللّهُ عَلَيْكُمْ لِيُحَآجُّوكُم بِهِ عِندَ رَبِّكُمْ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[15]

Na wanapo kutana na wale walio amini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke yao, wao kwa wao, husema: Mnawaambia aliyo kufunulieni Mwenyezi Mungu ili wapate kukuhojieni mbele ya Mola wenu Mlezi? Basi hamfahamu nyinyi .

Maelezo kuhusiana na aya

Mayahudi walipokuwa wakimnafikia Mtume (s.a.w.w) na wafuasi wake na wakiwakubalia kuwa kweli Mtume Muhammad (s.a.w.w) katajwa katika Tawrati, wenzao walikuwa wakiwalaumu kwa kule kuwafunulia Waislamu mambo ambayo mayahudi wamewafikiana kuwa wayafiche. Basi Mwenyeenzi Mungu Anawajibu kwa aya ifuatayo, kwamba Yeye anayajua wanayoyaficha na wanayoyadhihirisha.

[1] Suratl_baqara aya ya 4

[2] Suratul-baqara aya ya 115

[3] Suratul-Faatiha aya ya 7

[4] Surat Hud aya ya 51

[5] Surat Yussuf aya ya 109

[6] Surat Anbiyaa aya ya 10

[7] Surat Al-an-am Aya ya 32

[8] Suratul-Baqar aya ya 44

[9] Surat Azukhruf aya ya 3

[10] Surat ashuaraa aya ya 28

[11] Surat Al-imrani aya ya 3

[12] Surat alhadiyd aya ya 17

[13] Surat Albaqara aya ya 73

[14] Surat Albaqara aya 242

[15] Surat Albaqara aya ya 76

MWISHO