DALILI ZA KIAKILI ZA KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU
  • Kichwa: DALILI ZA KIAKILI ZA KUMFAHAMU MWENYEEZI MUNGU
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 4:48:48 3-11-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

DALILI ZA KIAKILI ZA KUMFAHAMU MWENYEENZI MUNGU
Katika makala zilizopita tulielezea njia za kumfahamu Mwenyeezi Mungu, na tukathibitisha hayo kutokana na dalili za kiakili ambazo tulizithibitisha kutoka ndani ya Qur-ani.

Katika makala hii tutaendelea kuziorodhesha Aya za Qur-ani ambazo kiakili zinathibitisha kumfahamu na kumtambua Mwenyeezi Mungu.

Mwenyeezi Mungu Mtukufu anasema:-

يَا اَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَتَّخِذُواْ بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لاَ يَاْلُونَكُمْ خَبَالاً وَدُّواْ مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاء مِنْ اَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِى صُدُورُهُمْ اَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الآيَاتِ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ[1]

Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.   

Maelezo kuhusiana na aya
Katika jambo kubwa kabisa linaloongoza mambo ya watu yakaongoka ni kuyapanga na kuyatengeneza kwa siri,yaonekane yamekwisha kusimama; kwani kuna waovu wengi, hawapendi ya wenzao yanyoke,basi mara huyatilia kila namna ya miunda; tahamaki yamepwelewa papo hapo, hayawezi kwenda mbele.

Ndio ikakatazwa hapa kuwafanya wasiokuwa Waislamu kuwa wasiri wenu wa kuwapa habari zenu za ndani.

Ama urafiki wa hujambo sijambo haukatazwi; wala kuwafanyia mema na insafu, kama yalivyobainishwa haya katika aya ya nane ya Suratul-Mumtahina.

لاَ يَنْهَاكُمُ اللهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِى الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ اَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ إِنَّ اللهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ[2]

Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.

Basi Mwenyeenzi Mungu hatukatazi kuwafanyia makafiri wema na insafu. Bali anatuamrisha tuwafanyie haya.

لَيْسَ عَلـٰي الاَعْمَي حَرَجٌ وَلاَ عَلـٰي الاَعْرَجِ حَرَجٌ وَلاَ عَلـٰي الْمَرِيضِ حَرَجٌ وَلاَ عَلـٰي اَنفُسِكُمْ اَن تَاْكُلُوا مِن بُيُوتِكُمْ اَوْ بُيُوتِ آبَائِكُمْ اَوْ بُيُوتِ اُمَّهَاتِكُمْ اَوْ بُيُوتِ إِخْوَانِكُمْ اَوْ بُيُوتِ اَخَوَاتِكُمْ اَوْ بُيُوتِ اَعْمَامِكُمْ اَوْ بُيُوتِ عَمَّاتِكُمْ اَوْ بُيُوتِ اَخْوَالِكُمْ اَوْ بُيُوتِ خَالاَتِكُمْ اَوْ مَا مَلَكْتُم مَّفَاتِحَهُ اَوْ صَدِيقِكُمْ لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ اَن تَاْكُلُوا جَمِيعاً اَوْ اَشْتَاتاً فَإِذَا دَخَلْتُم بُيُوتاً فَسَلِّمُوا عَلـٰي اَنفُسِكُمْ تَحِيَّةً مِّنْ عِندِ اللهِ مُبَارَكَةً طَيِّبَةً كَذٰلِكَ يُبَيِّنُ اللهُ لَكُمُ الآيَاتِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُون[3]

Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu nyinyi, mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za kaka zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za shangazi zenu, au nyumba za wajomba zenu, au nyumba za dada wa mama zenu, au za mlio washikia funguo zao, au rafiki yenu. Si vibaya kwenu mkila pamoja au mbali mbali. Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu, kuwa ni maamkio yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu, yenye baraka na mema. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kubainishieni Aya zake mpate kuelewa.

اُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[4]

Aibu yenu nyinyi na hivyo mnavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Basi nyinyi hamtii akilini?

وَمَا اُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا وَمَا عِندَ اللهِ خَيْرٌ وَاَبْقَي اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[5]

Na chochote mlicho pewa ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio bora na yatakayo baki zaidi. Basi je, hamfahamu?.

وَلَقَدْ اَضَلَّ مِنكُمْ جِبِلّاً كَثِيراً اَفَلَمْ تَكُونُوا تَعْقِلُونَ[6]

Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri?

وَهُوَ الَّذِى يُحْيِى وَيُمِيتُ وَلَهُ اخْتِلاَفُ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[7]

Na Yeye ndiye anaye huisha na kufisha, na yake Yeye mabadiliko ya usiku na mchana. Basi je! Hamfahamu?

هُوَ الَّذِى خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلاً ثُمَّ لِتَبْلُغُوا اَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا شُيُوخاً وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّي مِن قَبْلُ وَلِتَبْلُغُوا اَجَلاً مُّسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ[8]

Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la damu, kisha akakutoeni katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikilia utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanao kufa kabla, na ili mfikie muda ulio kwisha wekwa, na ili mpate kufahamu.

وَبِاللَّيْلِ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[9]

Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?

فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُواْ الْكِتَابَ يَاْخُذُونَ عَرَضَ هَـذَا الادْنَي وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِن يَاْتِهِمْ عَرَضٌ مِّثْلُهُ يَاْخُذُوهُ اَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِم مِّيثَاقُ الْكِتَابِ اَن لاَّ يِقُولُواْ عَلـٰي اللهِ إِلاَّ الْحَقَّ وَدَرَسُواْ مَا فِيهِ وَالدَّارُ الآخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ اَفَلاَ تَعْقِلُونَ[10]

Na wakafuatia baada yao kizazi kibaya walio rithi Kitabu. Wakashika anasa za haya maisha duni, na wakasema: Tutasamehewa! Na ikiwajia tena anasa kama hiyo wataishika pia. Je, hawakufanyiwa agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila Haki tu? Nao wamekwisha soma yaliomo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wanao jikinga na maasi. Basi je, hamtii akilini? .
Maelezo kuhusiana na aya
Sifa hii ya Mayahudi wabaya ya kufanya uovu bila ya kujali kwa kutaraji kusamehewa juu ya ubaya wao huo; sifa hiyo imerithiwa na baadhi ya Waislamu sasa. Kuna chungu ya Waislamu- na wengineo katika wao ni wajuzi wa dini- wanaodhulumu huku na kufisidi huku, wakiambiwa wanasema: “Mwenyeenzi Mungu Ghafur” uwongo maneno haya; na Mwenyeenzi Mungu anayakataa hapa aliyoyakataa mahala pengi kabisa penginepo kama katika aya ya 17 na 18 suratul-Nisaa. Na Mtume pia amekanusha habari hii.

إِنَّمَا التَّوْبَةُ عَلـٰي اللهِ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السُّوَءَ بِجَهَالَةٍ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٍ فَاُوْلَـئِكَ يَتُوبُ اللّهُ عَلَيْهِمْ وَكَانَ اللّهُ عَلِيماً حَكِيماً

وَلَيْسَتِ التَّوْبَةُ لِلَّذِينَ يَعْمَلُونَ السَّيِّئَاتِ حَتَّي إِذَا حَضَرَ اَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ إِنِّى تُبْتُ الآنَ وَلاَ الَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمْ كُفَّارٌ اُوْلَـئِكَ اَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَاباً اَلِيماً[11]

Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima .Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia. Wala wale wanao kufa na hali wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu.

Hii ni itikadi mbaya tuliyowafuata Mayahudi. Na kuna mengineyo pia tuliowafuata Mayahudi na Manasara na wenye dini nyenginezo.

Na Mtume alitwambia haya kuwa tutapotea baadhi yetu; tutafuata itikadi na nyendo za watu wenye dini nyengine tuache itikadi za dini yetu na njia yake iliyonyooka, alisema haya Mtume Kwa lafdhi hizi: “ Mtafuata nyendo za wale waliokuwa kabla yenu. Mtawafuata shubiri kwa shubiri. Hata lau wangeingia katika shimo la kenge basi na nyinyi mtaingia” Kama mambo haya ya kujitumainisha uwongo, mambo ya kukumbusha misiba na kuacha yaliyo muhimu wakashughulikia ya upuzi.
Na kila aya zilizowateremkia makafiri basi na wabaya hawa wanaowafuata zinawachukua. Husemwa hivi ndani ya vitabu, husemwa” Kila aya iliyowateremkia makafiri basi huwakokota na maasi wa kiislamu.” Basi natutahadhari na kutupa mwendo wetu na itikadi zetu za Kiislamu.

Kutokana na aya hizo tulizoziorodhesha hapo juu inathibitisha ya kwamba qur-ani kariym inawaamrisha watu kuzingatia na kufikiri, hii ni kwa sababu ya dalili ambazo zinamuongoza mwanaadamu katika njia ya Mwenyeenzi Mungu mtukufu. Katika sehemu hii tutaashiria baadhi ya dalili na kutoa mifano yake.

[1] Surat Al-im-rani aya ya 118

[2] Suratul-mumtahina aya ya 8

[3] Surat Nuur aya ya 61

[4] Surat Anbiyaa aya ya 67

[5] Suratul-Qasas aya ya 60

[6] Surat Yaasin aya ya 62

[7] Suratul-Muu-minuun aya ya 80

[8] Surat Ghaafir aya ya 67

[9] Surat Ghaafir aya ya 138

[10] Suratul-Al-aaraf aya ya 169

[11] Suratul-nisaa aya ya 17-18


MWISHO