MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.5
  • Kichwa: MALENGO YA MITUME YA ALLAH NO.5
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 7:29:26 24-8-1403

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI

KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

MALENGO YA MITUME YA MWENYEEZI MUNGU NO.5

* Mitume Mitukufu ya Mwenyeezi Mungu imekuja kuwalingania wanaadamu katika kitu gani?.

katika makala iliyopita tulielezea kuhusu malengo ya Mitume ya Mwenyeezi Mungu, katika makala hii tutaendelea na mada yetu ile ile inayohusiana na malengo ya Mitume.
3. KUTIMIZA UADILIFU

Pindi jamii ya wanaadamu ikiwa katika hali ya usalama, hapana shaka italeta athari kubwa miongoni mwa wanaadamu, na ni kwa sababu hiyo basi Mitume yote imefanya jitihada katika kuhukumu kanuni za Mwenyeezi Mungu, na kuwafanya wanaadamu kunufaika na haki zao binafsi, na vile vile haki zao katika jamii, hakuna mtu mwenye haki ya kudhulumu, wala hakuna mwenye kudhulumiwa, kama inavyosema Qur-ani:-

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُواْ فَاْذَنُواْ بِحَرْبٍ مِّنَ اللهِ وَرَسُولِهِ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُؤُوسُ اَمْوَالِكُمْ لاَ تَظْلِمُونَ وَلاَ تُظْلَمُونَ[1]
Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.
Vile vile Mitume imefanya jitihada kuwapa watu elimu, ili wawe na uwezo wa kupambanua haki na batili, na wao wenyewe waweze kuhukumu kwa uadilifu katika jamii, kama anavyosema Allah (s.w): -
لَقَدْ اَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَاَنزَلْنَا مَعَهُمُ  الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ وَاَنزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَاْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللهُ مَن يَنصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ إِنَّ اللهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ[2]
Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anaye mnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda.

Iliposemwa "na tumeteremsha chuma" tamko la asli lililofasiriwa kwa "Anzalnaa" maana yake ni tumekiteremsha. aidha katika aya ya 6 sura ya 39 inasema:-
خلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَاَنزَلَ لَكُم مِّنْ الاَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ اَزْوَاجٍ يَخْلُقُكُمْ فِى بُطُونِ اُمَّهَاتِكُمْ خَلْقاً مِن بَعْدِ خَلْقٍ فِى ظُلُمَاتٍ ثَلاَثٍ ذٰلِكُمُ اللهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ فَاَنَّي تُصْرَفُونَ
Amekuumbeni katika nafsi moja, kisha akamfanya mwenziwe katika jinsi yake, na akakuumbeni wanyama, wanane madume na majike, hukuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo katika giza tatu, Huyo ndiye Mwenyeezi Mungu Mola wenu, ufalme ni wake hakuna aabudiwaye ila Yeye tu, basi nyinyi mnageuzwa wapi?

Maelezo kuhusiana na Aya:

Tamko asili lililofasiriwa kwa "Tumeumba" "Anzala" maana yake ni "Ameteremsha" hii huitwa "Almajazul Aqly"
[1] Suratul Baqarah Aya ya 279
[2] Surat Alhadiyd Aya ya 25

MWISHO