UPORWAJI WA FADAK NA WAPORAJI 2
  • Kichwa: UPORWAJI WA FADAK NA WAPORAJI 2
  • mwandishi: Hassani Bussi
  • Chanzo: mailto:busihassan@gmail.com
  • Tarehe ya Kutolewa: 17:40:0 2-11-1403

UPORWAJI WA FADAK NA WAPORAJI

Sehemu ya pili

KUTEREMSHWA KWA AYA YA "MPE HAKI JAMAA WA KARIBU"

Wakati Mtukufu Mtume saww aliporudi Madina, Jibril aliteremsha Aya ifuatayo:

وآت ذاالقربى حقه والمسكين وابن السبيل ولا تبذر تبذيرا

"Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake, na masikini na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo. " 17:26

Mtukufu Mtume saww alitafakari juu ya umuhimu wa wahyi huu. Jibril alitokea tena na akamjulisha kwamba Mwenyezi Mungu ameamrisha kwamba: "Fadak itolewe kwa Fatimah." Mtukufu Mtume saww akamuita Fatimah na akasema:  "Mwenyezi Mungu ameniamuru kuitoa Fadak kama zawadi kwako." Hivyo mara moja alimpa Fatimah umiliki wa Fadak..

Malik:

Tafadhali fafanua unachosema kuhusu tukio ambalo Aya hii tukufu imeteremshwa. Je, imeandikwa kwenye vitabu vya historia na Tafsiri vya Shi'ah, au vilevile umeiona habari hii katika vitabu vyetu Ahlisuna vya kutegemewa?

Sulayman:

Mkuu wa wafasiri, Ahmad bin Tha'labi Sijistani katika kitabu chake "Kashful Bayan", Jalalu Dini Asuyuti katika Tafsiri yake Jz 4, akisimulia kutoka kwa Hafidh Ibn Mardawaiyya: yule mfasiri mashuhuri Ahmad bin Musa aliyefariki mwaka 352 hijiria akisimulia kutoka kwa Abu Sa'id Khudri na Hakim Abu l Qasim Haskani; Ibn Kathir; Imadu Dini Ismail; Ibn Umar Damishqi; Faqih Shafii katika kitabu chake cha Ta'rekh na Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiul Mawadda Sura ya 39 akisimulia kutoka kwa Tafsiri Tha'labi, Jamuu l Fawaid na Uyunul Akhbar" wote wanasimulia kwamba:

wakati Aya, "Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake....,"  

وآت ذاالقربى حقه والمسكين وابن السبيل ولا تبذر تبذيرا

Ilipoteremshwa Mtukufu Mtume saww alimuita Fatimah na akampa Fatimah Fadak kubwa kama zawadi kwake kwa hiyo, kadiri Mtukufu Mtume saww alivyoishi, Fadak ilibakia katika miliki ya Fatimah. Bibi yule Mtukufu aliikodisha ardhi ile; mapato yake yalikusanywa katika awamu tatu. Kutoka katika hesabu hii alichukua pesa ya kutosha kwa ajili ya chakula chake na watoto wake na akagawanya kilichobaki kwa watu masikini wa Bani Hashim.

Baada ya kifo cha Mtume saww, maofisa wa Abu Bakr alipotawala (kwa nguvu ya upanga) walinyakua Mali hii kutoka kwa Fatimah.

Nakuulizeni Enyi waheshimiwa, mnieleze katika jina la Uadilifu mtakiitaje kitendo hiki?

Malik,:

Hii ndiyo mara ya kwanza nimesikia kwamba Mtukufu Mtume saww alimpa Fatimah umiliki wa Fadak kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Sulayman:

Inawezekana kwamba hukuweza kusikia kuhusu suala hili. Lakini kama ambavyo nimekuambia, wengi wa maulamaa wenu Ahlisuna wakubwa wameandika kuhusu suala hili katika vitabu vyao vya kutegemewa. Ili kuthibitisha nukta hii kwa uwazi nakurejeshea kwa Hafidh Ibn Mardawaiyya, Waqidi na Hakim Angalia Tafsiri na Ta'rekh zao; Jalalu Dini Asuyuti katika Durrul Manthur Jz 4 UK 177; "Kanzul Ummal" ya Mullah Ali Muttaqi na maelezo mafupi ambayo ameandika juu ya Kitabu l Akhalaki ya Musnad ya Ahmad bin Hanbal kuhusu tatizo la Silat rahm; na Sherehe Nahjul Balagha ya Ibn Abi Hadid Muutazili Jz 4.

Maulamaa wote hawa wamesimulia katika njia tofauti, isipokuwa maelezo kutoka kwa Abu Sa'id Khudri, kwamba Aya hiyo Hapo juu ilipoteremshwa Mtukufu Mtume saww aliitoa Fadak na kumpa Fatimah Zahraa