UFAFANUZI JUU YA UIMAMU NDANI YA QURANI NA HADITHI
Katika riwaya mbalimbali limeelezewa suala la kua Maimamu (a.s) ni watambuzi wa mambo yaliopita na yajayo, na kumesisitizwa vilevile kua elimu na utambuzi huu walionao ni yenye kutokana na Mwenye enzi Mungu (a.s), naye ndiye aliyewapatia elimu hii na Wao hawana uwezo wowote mbele ya Mola wao na yote wayafanyayo ni kwa uwezo wa Mola wao, na Gheibu walionayo maimammu (a.s) sio Gheibu ya kujua kila kitu bali ni baadhi mambo tu, kwani hawana habari ya kua siku gani Kiama kitasimama, kwani mjuzi wa siku hii Mwenye enzi Mungu tu peke yake.
ELMU GHAIBU YA MAIMAMU (A.S)
Elimu ya Mwenye enzi Mungu iko katika namna mbili:
Elimu ambayo hakuna aijuayo ila Yeye tu peke yake, na hata Malaika na Mitume (a.s) hawana habari nayo, na sehemu ya pili ya elimu ni ile elimu ambayo huwafunulia Malaika wake na Malaika nao huifikisha elimu hiyo kwa mitume wanaohusika, kama vile ilivyomfikia elimu hiyo Mtume wetu (s.aw) yeye pamoja na kizazi chake (Ahlul bait) (a.s) , ili elimu hiyo ibakie milele hadi siku ya Kiama kwa kupitia kizazi chake, na Mwenye enzi Mungu (s.w) ameliashiria suala hili katika Qurani akisema: (Yeye ni mjuzi wa yale ya ghaibu (asiotambulikana) na yale yalio dhahiri (yenye kujulikana au kushuhudiwa, naye hayadhihirishi yaliofichika (yale ya ghaibu) kwa mtu yeyote yule, isipokua huwadhihirishia wale aliowaridhia miongoni mwa mitume).
Katika dua ijulikanayo kwa jina la (Ziaratul jaamia), tunakuta maneno haya : (na amekuridhieni Mola wenu kwa kukufunulieni (nyinyi Muimau) Ghaibu yake na kukufanyeni kua nyinyi ndio maficho ya siri zake).
Na ndani ya kitabu (Nahjulbalagha) kilichokusanya maneno ya Imamu Ali (a.s) kuna maelezo yenye kutoa habari za mambo yajayo, miongoni mwa maelezo hayo ni zile bishara za Imamu Ali (a.s) alizowabashiria watu kuja kwa kiongozi mkorofi ajulikanaye kwa jina la (Hajjaj bin Yusuf) na tokeo hili lilithibitika, naye mwenyewe Ali bin abiiTaalib (a.s) ameiita habari hii kua ni Elmul ghaibu pale alipowambia watu wake akisema: (mgelikua limekufunukieni lile lililonifunukia mimi na ingelikua mnaielewa Ghaibu ninayoielewa mimi, basi mgekwenda majangwani kwa huku mkilia na kujigaragaza kwenye dongo lake na mgelijipiga vifuani na vichwani kwa majuto na khofu na mgeliziacha mali zenu bila ya kuziwekea walinzi na msingeamini kua laweza kutokea jambo hilo (hiyo habari ambayo itatokea baadae), kwa hakika hivi karibuni atakuzukieni kiongozi alie dhalimu ajulikanae kwa jina la Hajjaj bin yusuf Athaqafiy, naye atakupeni mateso ya hali ya juu kabisa naye hana huruma hata kidogo.
Kwa hiyo basi imamu Ali (a.s) atakua ni mmoja wa wale walioridhiwa na Mwenye enzi Mungu na kupewa elimu ya Gaibu, Imamu Aali (a.s) akiyanukuu maeneno yanayomzungumzia yeye kutoka kwa Mtume (s.a.w) anasema : (Mtume (s.a.w) amesema ewe Ali wewe unayasikia yake ninayoyasikia na unayaona yalw niniyoyaona ila tu wewe si mtume). Kwa kutokana na riwaya hii inafahamika kua Ali (a.s) alikua akiudiriki Wahyi pale ulipokua ukiteremshwa pamoja na kuyadiriki mazingira yote ya Wahyi kwa ujumla.
Mmoja kati ya wafuasi wa Imamu Ali (a.s) alishangazwa sana kwa kumuona Imamu (a.s) alipokua akitoa jawabu za masula tofauti bila yakua na gati gati, naye akamuuliza Imamu Ali (a.s): (hivi wewe una elimu ya Ghaibu?) Imamu (a.s) akamjibu: (hii si elimu ya Ghaibu kwani elimu ya Ghaibu ni ya Mwenye enzi Mungu pekee, elimu yangu mimi nimeichukua kwa yule alionayo, na elimu ya Ghaibu ni elimu ihusianayo na siku ya Kiama na elimu hii hakuna aijuayo ila Yeye tu (Mwenye enzi Mungu, kama Yeye mwenyewe asemavyo: (hakika Mwenye enzi Mungu ndiye alioimiliki elimu ihusianayo na siku ya Kiama).
Imamu Ali (a.s) anasema: (wallahi nikitaka ninao uwezo wa kumuelezea mmoja mmoja miongoni mwenu kua ametoka wapi, anakwenda wapi, na mwishowe ataishia kwenye matendo gani, lakini kinachonizuia ni kukhofia kua mwaweza mkanihukumu vyengine au kunidhania kua mimi ni Mtume.
Ali bin Abii Talib, amesema: (naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, kua yale yote aliokua mtume akiyafahamu, nami vilevile ninayafahamu, na matokeo yote yaliotokea na yatakayotokea baadae hadi kufika siku ya Kiama yote ninayafahamu.
Ndani ya vitabu vinavyokubalika mmeja riwaya zenye kuelezea kua maimamu ni wenye elimu ya Ghaibu na niwatambuzi wa mambo yajayo, miongoni mwa vitabu hivyo ni mjaladi wa 26 wa kitabu (Biharul anuwar) mwanzo wa ukurasa wa 226 kwenye mada izungumzayo kuhusiana na upana wa elimu ya Maimu (a.s) ikiwemo vilevile elimu ya Ghaibu na ndani ya kitabu hichi mmetjwa Hadithi chungu nzima zenye kulithibitisha jambo hili.
Sheikh Saduku kwenye kitabu Uyunil akhbarir Ridhaa kwenye mlango wenye kuhusiana na elimu ya Ghaibu ya Imamu Al-ridhaa (a.s) amenukuu Hadithi 44.
Mtu yeyote yula mwenye macho yaliowazi, ataelewa kua ili mtu aweze kua kiongozi wa waislamu ni lazima awe na sifa nne nazo ni (kchaguliwa na Mwenye enzi Mungu, kuashiriwa kuteuliwa kwake katika Riwaya, awe na elimu ya Ghaibu, na vilevle awe amehifadhika kutokana na maasi).
Sifa tulizozitaja hapo juu si kua waliozizungumzia sifa hizo kwa mara ya kwanza kabisa walikua ni maulamaa wa Akida walioisha katika karne ya tatu na karne ya nne, bali sifa hizi zilikuawa tayari zimeshatajwa ndani ya Hadithi za Maimamu (a.s).
MWISHO