HADITHI YA UMMU SALAMAH
  • Kichwa: HADITHI YA UMMU SALAMAH
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 20:3:42 24-8-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

HADITHI YA UMMU SALAMAH

HADITHI YA UMMU SALAMAH KATIKA MAPOKEZI YA BUKHARIY

Katika Mustadrak As-Sahihain amepokea Al-Hakim kwa Isinadi yake kutoka kwa Hanashi Al-Kinaaniy, amesema: " Nilisikia Abudhar anasema akiwa ameshika mlango wa Ka'aba: Enyi watu anayenijua basi mimi ni yule mnayemjua na asiyenijua basi mimi ni Abudhari, nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema mfano wa Ahlul-baiti wangu kwenu ni kama mfano wa jahazi la nuhu atakayelipanda amenusurika na atakayeacha kulipanda ameghariki" .13

Vilevile katika Mustadrak As-Sahihain kwa Isnad yake kutoka kwa Ibunu Abbas: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) "nyota ni tumaini kwa watu wa ardhini kutokana na kughariki, na Ahlul-baiti ni tumaini kwa umma wangu kutokana na Ikhitilafu, kama kabila katika waarabu litawakhalifu basi watakhitalifiana na kuwa kundi la Iblisi". 14

Na kwa kufafanua zaidi na kuongezea katika yaliyopita miongoni mwa dalili katika kuthibitisha kuwa Ahlul-baiti, ndio wenye vyeo hivyo vitukufu kwa kutakaswa, wamefanywa kuwa ni maalumu kwa kupewa sifa ya tamshi la "Alayhi Salam" bila ya masahaba wengine wote na wake wa Nabii, na hiyo ni kutokana na vyeo vyao vitukufu na kwa yale aliyoyafanya Mwenyezi Mungu kuwa ni maalumu kwao kwa kuwatakasa kutokana na uchafu na makosa madogo kwa wakubwa kama yanavyo dhihirika hayo katika sehemu nyingi katika Sahihi Bukhariy, Ali (a.s.) amesema "nilikuwa na ngamia katika hisa yangu ya ngawira na Nabii (s.a.w.w.) alikuwa amenipa katika (mali ya) Khumsi, basi nilipotaka kumuoa Fatma (a.s) binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) …..." 15

Katika mlango wa kuhimiza Nabii (s.a.w.w.) Sala ya usiku na sunna bila ya kuifanya kuwa ni wajibu, akasema "Nabii aliwagongea Fatma na Ali (a.s.) mlango usiku, kwa ajili ya Sala ya Usiku. 16 Kutoka kwake amesema: "Nilimuona Nabii (s.a.w.w.) na Hassan bin Ali (a.s.) na alikuwa anafanana naye nikamwambia Juhaifah anielezea sifa zake". 17 Hakika Hussein bin Ali (a.s.) amemwambia kwamba Ali bin Abutalib amemwambia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimgongea mlango usiku yeye na Fatma binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, akawaambia je, hamsali? *[1] Na ni mashuhuri kwamba sifa hii ya (Alayhi As-salam) hakupewa asiye kuwa Ahlul-baiti isipokuwa Manabii (a.s.).

Na alipoulizwa Mtume (s.a.w.w.) namna ya kumsalia alijibu: "Semeni Allahumma Swalli alaa Muhammad wa aali Muhammad kamaa Swallayta alaa Ibrahiyma wa aali Ibrahiym....". Ametusimulia Al-hakimu amesema: "Nilimsikia Abdur-rahman bin Abiy Layla amesema: Alimkuta Kaabu bin Ujurah akasema: Je, nikupe zawadi? Hakika Nabii (s.a.w.w.) alitokea basi tukasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tumeshafahamu namna ya kukusalimia, basi ni namna gani tutakusalia? Akasema: Semeni: Allahumma Swalli alaa Muhammad wa aali Muhammad kamaa Swallayta alaa Ibrahiyma Wa Aali Ibrahiym Innaka Hamiydu MMajiydu".18 Hiyo ni kwa sababu Ibrahiym alikuwa ni Nabii na Ali zake walikuwa ni Manabii na wenye kulinda sheria baada yake, vivyo hivyo walikuwa aali Muhammad lakini tofauti ni kwamba wao wamekuja ili wawe Maimamu na wala sio Manabii kama alivyobainisha hayo Nabii (s.a.w.w.) alipomwambia Ali (a.s.).

"Nafasi yako kwangu ni kama nafasi ya Haruna kwa Mussa isipokuwa hakuna Nabii baada yangu" 19 kama yatakavyokuja hayo baadae, inafahamika katika yote yaliyotangulia miongoni mwa hadithi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu kama alivyomfanya Mtume wake (s.a.w.w.) kuwa ni maalumu anayeteremshiwa wahyi - Kwa Umaasum na kutakaswa kwa kuwa sifa yake ni kufikisha ujumbe na dhamana ya usalama wa Tablighi yake vinginevyo watu wasingeamini maneno yake na wala waasingekuwa na uhakika wa ujumbe wake, vile vile amewafanya Maimamu wa Ahlul-baiti kuwa ni maalumu kwa Umaasumu na kutakaswa kwa dalili ya Aya ya "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoloeni Uchafu Ahlul-baiti na kuwatakasa kabisa kabisa" ,20 na kwa sifa yao ya kujaza nafasi ambayo ameiacha Mtume (s.a.w.w.), na hiyo ni kwa kubeba sheria ya Mwenyezi Mungu kwa vizazi vijavyo kwa ajili ya kuihifadhi dini kutokana na upotovu wa wapotoshaji, uongo wa wadanganyifu na shaka za wenye shaka, kwani kitu kibaya mno kilicho kumba sheria zilizotangulia ni kwamba wafuasi wake walikuwa wanachukua hukumu za Manabii wao baada ya kuondoka kwao kwa kila mtu. Basi upotovu ukawa kama ilivyosema Qur'an tukufu, "Mnatumaini ya kwamba watakuaminini (hao Mayahudi) na hali baadhi yao walikuwa wanasikia maneno ya Mwenyezi Mungu kisha wanayabadilisha baada ya kuwa wameyafahamu, na hali wanajua",22 basi wakapotoka na kupotea.

Na kwa hiyo Uimamu unazingatiwa kuwa ni mlolongo wa Unabii katika jumla ya kazi zake isipokuwa kinachohusiana na wahyi kwani huo ni maalumu kwa Manabii, na makusudio ya kuwa Uimamu ni mlolongo wa Unabii ni kule kuhifadhi sheria kinadharia na kivitendo. Hivyo ikawa ni wajibu Maimamu wawe Maasumu kutokana na uwajibu wa kunukuu sheria ya Mwenyezi Mungu - ambayo alikuja nayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) - Kwa vizazi vijavyo kupitia katika Njia safi na ya asili ambayo imepitia kwa Maimamu kumi na mbili wa Ahlul-baiti.

Na kuna dalili za Qur'an zinazoashiria kuwa Uimamu ni cheo kitukufu hakipati mtu, dhalimu au fasiki, amesema Mwenyezi Mungu, "Akamwambia: Hakika mimi nitakufanya kuwa Imamu kwa watu; akasema, Je na katika kizazi changu? Akasema, (ndio) lakini ahadi yangu haitawafikia madhalimu"23, hivyo makosa madogo na makubwa yanamfanya anayeyatenda kuwa ni dhalimu, hivyo ikawa hakuna budi ya Imamu kuwa ni Maasumu kutokana na makosa yoyote au dhambi kama ilivyoonyesha Aya iliyotangulia.

MWISHO