HOTUBA YA IJUMAA
  • Kichwa: HOTUBA YA IJUMAA
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 20:14:4 24-8-1403

BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

HOTUBA YA IJUMAA 

VITENDO VYA MWENYEZI MUNGU

Kwa Jina Lake, Aliye Tukuka
Lazima iwepo sababu juu ya kila kitu kilichoumbwa na Mwenyezi Mungu. Lakini si lazima tuifahamu kila sababu. Tunasema kwamba kila kazi ya Mwenyezi Mungu ni ya ajabu na ikiwa jambo barabara kutendwa. Mara nyingi tunasumbuka kutokana na baadhi ya matukio au baadhi ya matatizo kwa sababu hatujui ni nini hasa sababu zilizo nyuma yake. Mfano unaweza kuonekana katika Qurani, ambapo kukutana kwa Nabii Musa (a.s.) na mtu mwingine mwenye elimu zaidi kuliko Nabii Musa (a.s.) unaelezwa. Mtaalamu alimruhusu Musa kufuatana naye kwa sharti kwamba "Usiniulize kuhusu jambo lolote mpaka mimi mwenyewe nikuelezee."

Hii ni hadithi nzima:-
"Akasema (yule mtaalamu): Hakika wewe huwezi kuvumilia kuwa pamoja nami. Na unawezaje kuvumilia juu ya lile usilolijua? Akasema (Musa): Kwa yakini Akipenda Mwenyezi Mungu utanikuta mvumilivu wala sitaasi amri yako (18:67 69) Nabii Musa (a.s.) na mtalaamu walipanda jahazini. Na walipokuwa jahazini, mtaalamu akalitoboa. Musa akapinga, na wakaelekea mjini, huko mtaalamu alimkuta kijana mmoja, akamkamata na kumchinja. Kwa jambo hilo, Musa hakuweza kujizuia, akamlaumu kwa maneno makali. Akakumbushwa tena ile ahadi yake ya kutouliza maswali.

Hapo tena walifika katika mji ambao watu wake waliwanyima chakula. Wakakuta huko ukuta unaotaka kuanguka, na mtaalamu akausimamisha. Musa akasema, "…, bila shaka ungelipwa ujira kwa kazi hii" (18:77)
Kwa kumhoji mara hii ya tatu, mtaalamu alimwambia Musa, "Hii ndiyo faraka baina ya mimi na wewe:…" (18:78)

Kisha kabla hawajaachana, alimweleza sababu zote za vitendo vyake: "Ama safina, basi ilikuwa ya maskini wafanyao kazi baharini; na nilitaka kuiharibu na nyuma yao kulikuwa mfalme aliyekamata kila safina kwa nguvu." (18:79)
"Na ama kivulana, basi wazazi wake walikuwa waaminio, na tukahofia kwamba asije kuwahangaisha kwa uasi na kufuru. Basi tulitaka ya kwamba Mola wao Awabadilishie aliye bora kuliko yeye kwa kutakasika na aliye karibu zaidi kwa huruma. (18:80-81)

"Na ama ukuta, basi ulikuwa wa watoto wawili mayatima mjini, na chini yake kulikuwa hazina yao, na baba yao alikuwa mwema; kwa hiyo Mola wako alitaka wafikie balehe yao na wajitolee hazina zao: ni rehema kutoka kwa Mola wako; nami sikufanya (haya) kwa amri yangu… ( 18:82)

Natumai kuwa mfano huu unatosha kufahamisha fikra zetu kuhusu vitendo vya Mwenyezi Mungu. Kuna msemo wa Maulamaa (wenye elimu) usemao:
"Chochote kilichoamriwa kwa hekima, kimeamriwa na Sheria; na chochote kilichoamriwa na Sheria, kimeamriwa kwa Hekima". Mtu wa kawaida mara nyingi hafahamu msemo huu. Yeye hufikiri kwamba chochote tunachoamua kuwa ni kizuri lazima kitiliwe nguvu na Sheria, kiwe kilivyo. Hivo sivyo. Maana hasa ya msemo wa juu ni hii; ikiwa sisi tungelitaka kujua sababu za maamrisho fulani ya sheria, akili yetu ingelikubali kwa hakika kwamba maamrisho hayo yawe kama yalivyo. Na kwamba maamrisho yote ya Sheria yanatokana na busara.

SIFA ZA SURA AL - HAMD ( AL - FATIHA)

Miongoni mwa Sura za Qur'ani Tukufu, Sura hii inayo hadhi ya juu, ambayo huchimbuka kutoka kwenye sifa zifuatazo:
1. Uzito wa Sura hii:
Kimsingi, sura hii inayo tofauti iliyo wazi na sura nyingine za Qur'ani Tukufu kutokana na mtazamo wa uthabiti na uzito, kwa sababu sura nyingine zote zinatoka kwenye usemi wa Mungu ambapo Sura hii inatoka kwenye ulimi wa waja. Na kutoka kwenye Mtazamo mwingine katika Sura hii, Mungu amewafundisha waja wake namna ya kusema na kuwasiliana na Yeye"

Utangulizi wa Sura hii umeanza na kumsifu na kumtukuza Mola Mlezi. Inaendelea na imani mwanzoni na baada ya maisha ya hapa duniani (kumtambua Mungu na imani katika ufufuo), inaishia na mahitaji na masharti ya waja. Wakati mtu mwenye hadhari, ambaye moyo wake umezinduka anaposoma sura hii huhisi kwamba amewekwa kwenye mabawa na manyoya ya malaika, kwamba ananyanyuka kwenda mbinguni, na kwenye uwanja wa kiroho, hatua kwa hatua, anasogea karibu zaidi kwa Mungu (s.w.t.).

Hili ni wazo bora sana, kwamba Uislamu, katika kukinzana na mifumo mingi ya imani za uwongo (ambapo husemekana kwamba wapatanishi wameteuliwa kati ya Mungu na viumbe), umetangaza kwa wanadamu kwamba bila ya mpatanishi, wanatakiwa kuanzisha uhusiano na Muumbaji wao!

Sura hii ni mfano, ambamo uhusiano huu wa karibu kati ya Mungu na wanadamu umeegemezwa (bila ya wapatanishi), kati ya vilivyoumbwa na Muumbaji. Mahali hapa yeye (mja) humuona Yeye tu, husema Naye tu, husikiliza ujumbe Wake kwa masikio yake na mwili wake, hivyo kwamba hapana hata Mtume au Mjumbe au mmoja wapo wa Malaika wa karibu sana anakuwa mpatanishi katika uhusiano huu. Na inastaajabisha kwamba muunganiko huu na uhusiano wa moja kwa moja wa vilivyoumbwa kwa Muumbaji ndio mwanzo wa Qur'ani Tukufu.

MWISHO