UPELELEZI WA WATAWALA WA ZA ZAMA ZILE
  • Kichwa: UPELELEZI WA WATAWALA WA ZA ZAMA ZILE
  • mwandishi:
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 7:30:10 24-8-1403

UPELELEZI WA WATAWALA ZA ZAMA ZILE

Kama vile ambavyo Firauni aliposikia kwamba mtoto atazaliwa katika Mayahudi, atakayeangamiza utawala wake, hakuacha hata njia moja ya kujaribia kuzuia kuzaliwa kwa yule mtoto, na hata ikiwa mtoto huyo keshazaliwa, kujaribu kumwua, vile vile mtawala wa ukoo wa Bani Abbas alijua kwa njia ya hadithi za mara kwa mara zisimuliwazo kuwa atazaliwa mwana wa Imamu Hasan Askari (a.s.) atakayekuwa mwangamizaji wa serikali yake hiyo ovu. Hivyo, alijaribu kuzuia kuzaliwa kwa mtoto huyo na akamweka Imamu Hasan Askari (a.s.) katika kifungo cha maisha. Lakini, kama vile Nabii Musa (a.s.) alivyozaliwa Iicha ya juhudi zote za Firauni, vivyo hivyo, Imamu “anayengojewa” alikuja duniani. Na kuzaliwa kwake, kufuatana na Maamrisho ya Mwenyezi Mungu na Rehma Yake, kulikuwa siri.

Imamu Hasan Askari (a.s.) alipofariki na ulipowadia wakati wa kumsalia sala ya maiti, Mwenyezi Mungu akaliondoa pazia Ia Ughaibu kwa muda mfupi. Watu wote wanaohusiana na jamii ya wafuasi wa ukoo wa Mtume (s.a.w.) walikuwa wamesimama katika safu kwa ajili ya sala ya maiti na Bwana Jaafar, ndugu wa Imamu Hasan Askari (a.s.) alikuwa kesha simama mbele kuiongoza sala hiyo, alitokea kwa ghafla kijana mdogo tokea nyuma ya pazia Ia chumba cha wanawake, na akaenda pale aliposimama Bwana Jaafar kupitia katikati ya safu. Akalivuta joho Ia Bwana Jaafar na kumwambia, "Rejea nyuma, Ami: Mimi nina haki zaidi ya kuongoza sala ya maiti ya baba yangu". Bwana Jaafar alirudi nyuma, na Imamu Kijana akaiongoza sala. Baada ya sala Imamu akatoweka tena nuyuma ya lile pazia.

Haiwezekani kwa Khalifa wa wakati ule kutofahamu kuwa yule mtoto amezaliwa. Hivyo juhudi za kumtafuta Imamu kijana asiyeonekana zikaanza kwa juhudi maradufu na kila njia ilitafutwa ya kumkamata na kumfunga au hata ya kumuua.

MWISHO