BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
UONGOZI WA IMAMU MUOKOZI NO.1
UONGOZI WA IMAM KINDANI NA KIDHAHIRI
Moja kati ya nyadhifa za Imam ni kuwaongoza watu katika njia ya haki, na anafanya jitihada ili kutekeleza wadhifa huo, watu ambao wamejitakasa nyoyo zao na kuifanya tayari kupokea nuru ya uongofu hufaidika na msaada wa uongozi wa Imam (yaani Imam watu hawa huwaongoza kwa kutumia nguvu maalum alizonazo na huielekeza mioyo yao katika kupenda mema na mambo mazuri,Imam ili kutekeleza wajibu wake huo huwasiliana na wanaadamu kidhahiri, na huwapa muongozo ili kufuata njia ya haki.
Na baadhi ya wakati hutumia nguvu alizopewa na Mola wake na huzitia athari nyoyo ambazo zimejitakasa kwa kupendelea kufanya mema.
Kutokana na maelezo ya hapo juu ni lazima tuzingatie kwamba kuwepo Imam kidhahiri hakumaanishi kwamba Imam ana mawasiliano na wanaadamu kila siku, bali inawezekana akawasiliana na mtu lakini mtu huyo asiweze kumfahamu Imam. Imam Aliy kuhusiana na maelezo hayo anasema:-
Ewe Mola, sio kwamba ni lazima kwako Wewe kumtuma mjumbe awaendee watu kidhahiri, ili watu wakuabudu Wewe, basi hata kama Imam atakuwa hayupo machoni mwa watu, lakini bila ya shaka mafunzo yake yatakuwa yameenea katika mioyo ya waumini, na watakuwa wanakuabudu Wewe kwa kupitia mafunzo hayo[1].
Kwa hiyo tumefahamu kwamba Imam ni mwenye nguvu za kuwaongowa watu, na kutokana na nguvu hizo basi wakati atakapodhuhuru ataleta mapinduzi katika dunia, basi watu ambao tayari wamejitakasa watakuwa pamoja na Imam, na hii ni moja katika mipango ya Imam.
KULETA AMANI KUTOKANA NA MABALAA YANAYOTOKEA KATIKA DUNIA.
Hakuna shaka kwamba kuwepo amani ndani ya dunia ni jambo muhimu sana katika maisha ya wanaadamu, katika dunia kunatokea mabalaa mbali mbali ambayo yanaleta athari mbaya kwa wanaadamu, na Wataalamu hutumia nyezo mbali mbali ili kuzuia mabalaa hayo yasitokee, ama ni lazima tuzingatie kwamba kuwepo Imam kunaleta amani katika dunia, na hii ndio sababu kuu inayozuia mabalaa yasitokee.
Imam Mahdiy anasema:-
"Mimi ndiye ninayeleta amani kutokana na mabalaa ambayo yanatokea katika dunia.
Mwenyeezi Mungu huwaletea wanaadamu mabalaa kutokana na madhambi na ufisadi ambao wanafanya katika dunia.
Qur-ani kariym inasema kumwambia Mtume Muhammad (s.a.w.w):-
Lakini Mwenyeezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu maadamu Wewe (Nabii Muhammad) umo pamoja nao (hapa Makka), wala Mwenyeezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu pia hali ya kuwa (baadhi yao wamesilimu) wanaomba msamaha[2].
Imam Mahdiy mbali ya kuwa ni hoja kutoka kwa Allah (s.w), vile vile ni mwenye kuwaepusha wafuasi waake na mabalaa, hata kama wafuasi hao hawatilii maanani ukarimu huo, na hawajui kwamba kutokana na msaada wake Imam wameepukwa na mabalaa mengi.
Imam Mahdiy anasema:-
Mimi ndiye mfuasi na kiongozi wa mwisho wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), na Allah (s.w) kutokana na kuwepo kwangu huwaondolea watu mabalaa.
Katika sehemu hii natuangalie matokeo yaliyotokea katika nchi ya Iran, matokeo ambayo yangelisababisha mabalaa katika nchi hiyo, lakini kutokana na ukarimu wake Imam amewasaidia Waislamu katika nchi hiyo ili kuepukana na mabalaa hayo:-
Mfano, Kuanguka na kushindwa serekali ya Shoh ndani ya tarehe 21 mwezi wa11 mwaka 1357, kuanguka Hercopter ya America katika mwaka 1359.
MWISHO
[1] Rejea kitabu Ith-bati-lhadaat, juzuu ya 3, ukurasa wa 463.
[2] Surat-al- Anfal aya 33