UHAKIKI WA DINI KATIKA NJIA YA HERMENUTICS
  • Kichwa: UHAKIKI WA DINI KATIKA NJIA YA HERMENUTICS
  • mwandishi: NDUGU ZETU WA KIISLAMU
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 2:21:0 23-8-1403

 

BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
UHAKIKI WA DINI KWA NJIA YA HERMENUTICS

Uhakiki wa dini hauwezi kufanywa kwa kutumia au kutegemea nadharia za watu wa fani ya Hermenutics. Wafuasi wa nadharia hizo wana itikadi ya kuwa kwa ajili ya kufahamu kile kilichoandikwa hakuna ulazima wa kufahamu makusudio ya muandishi, (yaani muandishi anakusudia nini katika matini au kitabu chake), bali msomaji kwa kujitosheleza na akili yake tu anaweza akachukua maamuzi au kupata ufumbuzi au kufahamu kile alichokisoma, la muhimu ni kujua kile alichokifahamu kutokana na akili yake, kwa hiyo kuifahamu ibara ni tendo lisilokuwa na mwisho, na ibara moja inaweza ikawa na ufahamu tofauti, leo ikafahamika vyengine, na kesho mtu mwengine akafahamu kwa mtindo mwengine, alimradi ibara hiyo moja inaweza ikawa na ufahamu zaidi ya hamsini, basi njia hiyo haikubaliki kwa sababu inaweza ikampotosha muhakiki, kwa upande mwengine baadhi ya elimu ni mahasusi kwa ajili ya Allah (s.w) tu. Kama anavyosema Yeye Mola Mtakatifu:-

وَيَسْاَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ قُلِ الرُّوحُ مِنْ اَمْرِ رَبِّى وَمَا اُوتِيتُم مِّن الْعِلْمِ إِلاَّ قَلِيلاً[1]

Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu.

Hizo zilikuwa ni njia tatu zisizokubalika katika uhakiki wa dini, hivyo kila muhakiki inamlazimu kufanya uhakiki wake kwa kutumia njia sahihi ambazo zitamuongoza katika malengo yake, ikiwa malengo ni kutambua haki na uhakika.

 Kazi ya uhakiki wa dini ni kufichua uhakika na kuzalisha matunda ya dini ndani ya jamii. Na kwa sababu haki na uhakika wa dini unaweza kupatikana katika vitengo mbali mbali vya uhakiki wa dini, kwa hiyo, kuna njia nyingi zilizoenea na kusambaa kila pande ya dunia ambazo zinaweza kumuongoza kila mtu katika kufanya uhakiki wake na kufikia katika natija na malengo anayoyakusudia, muhakiki anaweza kutumia njia mbali mbali katika uhakiki wake, kufahamu taaluma za dini kwa kutumia njia za kimaadili, vile vile muhakiki anayehakiki uhakika wa dini anaweza kutumia njia kuu na misingi ya taaluma iliyo maarufu katika kufanya utafiti wa mambo yanayohusiana na dini.

Katika uhakiki wa dini ni lazima kuzingatiwe vigezo vinavyotumiwa katika uhakiki huo, kwa sababu, baadhi ya vigezo haviendani sawa, kwa mfano: baina ya yale yaliyoandikwa katika vitabu vya baadhi ya dini, na utendaji amali wake haufanani, hivyo muhakiki anawadhifa wa kufahamu kuwa yale yaliyoandikwa na yale yaliyoamrishwa kutendwa ni lazima yaendane sambamba kimaandiko na kimatendo, isiwe yale yaliyoandikwa au kunakiliwa yanasema vyengine na utendaji amali wa hayo yaliyonakiliwa ni vyengine, udhaifu na upungufu kama huo unaonekana katika dini na madhehebu tofauti, lakini baadhi ya madhehebu hayana udhaifu huo, kwa sababu yale yaliyonakiliwa katika baadhi ya madhehebu yamenakiliwa kwa mazingatio ya hali ya juu kabisa, na yamenakiliwa na watu ambao wameridhiwa na Mwenyeezi Mungu na wana elimu ya hali ya juu, na ndio wanaostahili kuiongoza jamii kuelekea katika njia ya haki yenye uhakika, na hao sio wengine isipokuwa na Mitume yake Allah (s.w) na Ahlulbayt (a.s). Hivyo ukiwa uhakiki utafanywa kupitia mafunzo na elimu waliyoitoa watukufu hao basi muhakiki hawezi kupata matatizo yoyote katika uhakiki wake.

 


[1] Surat Al-Israa aya ya 85