BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
UHAKIKI WA DINI NO.1
UHAKIKI WA DINI KUPITIA MSINGI WA IJTIHADI.
Hatua ya kwanza:
Umuhimu wa maudhui (mada).
1. Kila haki imebeba maumbile mawili, umbile la ndani na umbile la nje, maumbile hayo huthibitishwa na kusadikishwa kutokana na ukweli wa haki hiyo, kwa ufafanuzi zaidi tunaweza kusema hivi:-
Haki ni kama kombe na lulu, lulu ambayo hupatikana katika kombe hiyo, kombe ni umbile la nje na lulu ni umbile la ndani, hivyo kuna uwiano baina ya vitu hivyo viwili, bila ya kuonekana kombe hatuwezi kuthibitisha kuwa katika kombe hiyo mna (lulu) ndani yake au mna kitu chengine. Kwa hiyo kadiri itakavyoonesha kuwa umbile la nje lina thamani na muhimu, basi umbile la ndani pia litakuwa ni muhimu na lenye thamani zaidi.
Madhumuni ya ufafanuzi huo tunakusudia kusema hivi:-
Dini nayo ni mfano wa kombe na lulu hiyo, - kadiri ya umbile la nje la dini lilivyo na thamani. Basi umbile la ndani la dini pia lina thamani- umbile la ndani la dini limebeba elimu na hukumu za mambo tofauti ya dini, umbile hilo haliwezi kusadikishwa au kuthibitishwa bila ya kuwepo umbile la nje la dini, umbile ambalo linaonyesha msingi wa dini, tukizingatia kuwa umbile la nje la dini ni lazima liwiane na umbile la ndani la dini, kwa hiyo ili kuifahamu dini (ambayo ni umbile la nje) ni lazima tuelewe umuhimu wa elimu na hukumu zote (ambazo ni umbile la ndani) - moja baada ya nyengine - zilizomo katika dini.
Kutokana na maelezo hayo, tumefahamu kuwa ni lazima kuelewa umuhimu na falsafa ya dini, na tunaweza kufahamu falsafa hiyo kwa kuzingatia umbile la ndani na la nje la dini.
2. Thamani ya mbile la ndani la kila teknologia inathibitishwa na kupatikana kutokana na umuhimu wa vitu vilivyomo katika umbile la ndani la teknolojia hiyo, ni sahihi kuwa umbile la nje la kitu (teknolojia) linawiana na umbile la ndani kitu (teknologia) hicho kulingana na umuhimu wa vitu hivyo vilivyomo ndani ya umbile la ndani, lakini baadhi ya wakati umbile la nje la teknolojia ni muhimu na lina thamani kubwa zaidi katika kutambulisha umbile la ndani la teknolojia.
Na dini basi ndio hivyo hivyo, kwa sababu kuifahamu dini katika umbile lake la nje kuna umuhimu na thamani ile ile ya kuifahamu dini katika umbile lake la ndani, kwa hiyo ni lazima tuitazame dini katika maumbile yote mawili na kwa mtazamo mmoja,kwani yote ni kitu kimoja.
3. Kuwepo kwa tata nyingi zinazohusiana na dini kijumla, - tata ambazo zaidi zinarushwa au kutokea kwa Meterialist, Orientalists, n.k. kijumla ni fikra na mitazamo ya watu wa nchi za kimagharibi - kumesababisha kuonekana umuhimu wa kuifahamu dini katika umbile lake la nje, au tunaweza kusema, umuhimu wa kufahamu falsafa ya dini. Katika dunia ya kileo ya nchi za kimagharibi, au kwa maelezo mengine fikra na mitazamo ya watu wa nchi za kimagharibi, falsafa ya dini ni nyenzo moja wapo wanayoitumia watu wa kimagharibi katika kuharibu umbile la ndani la dini (elimu na hukumu za mambo mbali mbali zilizomo ndani ya dini) na umbile la nje la dini. Katika sehemu hii natutizame kauli za baadhi ya wanafaqihi wasiokuwa waadhamu na wasiostahili kuwa viongozi wa dini ya Kiislamu:-
“Yale yanayosemwa na Wanafaqihi, (yanayotokana na rai na mitazamo yao binafsi) ambayo yanaweza kuwa sio uhakika, wala sio wahyi ulioteremshwa na ndio chanzo kinacholeta vurugu na ghasia, ni hizo hukumu za fiqhi ambazo pengine zinaweza kutolewa kwa mtazamo wa mtu binafsi na sio hukumu zilizoelezewa ndani ya dini, basi hatuwezi kuzifanyia amali hukumu hizo zilizotolewa kwa rai ya mtu binafsi, na dini inatukataza hayo, na ili kuleta dalili zinazothibitisha kukabiliana na ghasia au vurugu za baadhi ya wanafaqiyh inatupasa kujua na kuelewa umuhimu wa falsafa ya dini na sio kwenda katika hukumu za fiqhi zilizotolewa kutokana na rai au mtazamo wa mtu binafsi”.[1]
Kwa hiyo kama kuzitatua tata hizo kwa kuzipatia majibu yake ni wadhifa na jukumu la dini, na kama tata hizo zinaweza kutatuliwa kwa kuzingatiwa na kukubalika kwa kutumia upande mmoja tu, ambao ni “umuhimu wa kuitambua falsafa ya dini” kupitia umbile la ndani la dini (elimu na hukumu za mambo mbalimbali ya dini). Basi natija tunayoipata kutokana na maelezo hayo ni kwamba, wana dini wote inawapasa kuitambua falsafa ya dini kupitia maumbile mawili hayo, umbile la nje la dini na umbile la ndani la dini.
[1] Mustafa Malikiyan, toleo la gazeti la Khurdad, tarehe 3/7/1378. Uk.6
MWISHO