BISMILAHI RAHMANI RAHIYMI
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
QUR_ANI NA WATOTO
UTANGULIZI
Baada ya kupita miaka mingi na kuonekana uzoefu na tajruba (experience) ya kutoa mafunzo ya Qur-ani katika maudhui tofauti yanayowafunza watoto kuielewa Qur-ani, mafunzo hayo yanafundishwa kwa njia ya ishara ili kuwasaidia watoto kuihifadhi Qur-ani kwa urahisi zaidi. Na watu wengi wameyapokea mafunzo hayo na kuridhika nayo, na kwa sababu hiyo basi imetulazimika kutayarisha kitabu hiki ambacho kimekusanya maudhui tofauti , aya za qur-ani, tarjuma (translate), na michoro ambayo inamaanisha na kuonesha ufahamu wa aya hizo za qur-ani, nah ii inasaidia watoto kutamka herufi za Qur-ani kwa urahisi zaidi.
NJIA ZA KUTUMIA KITABU HIKI
1- Baada ya kuthibitika kwamba mtoto amefahamu ishara ya aya, inamlazimika achore picha inayoonesha maana ya aya hiyo.
2- Wazazi inawapasa wawatake watoto wao wachore picha zinazooana na aya hizo.
3- Watake watoto wenu wachore picha inayoonesha maudhui ya aya katika mabuku yao wanayochorea picha.
4- Wazazi wanatakiwa kuwafahamisha watoto wao kwa upole na upendo pindi wanapochora picha zao zinazohusiana na aya za Qur-ani wazingatie utukufu na wachore michoro yao kwa heshima.
Dua ya kuongeza kiwango cha elimu
Aya:
وَقُل رَّبِّ زِدْنِى عِلْما[1]
Tarjuma:
Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.
Kutoa katika vile mnavyovipenda
Aya:
لَن تَنَالُواْ الْبِرَّ حَتَّي تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَ[2]
Tarjuma:
Kabisa hamtafikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda.
[1] Surat Taha Aya ya 114
[2] Surat Al_imrani Aya ya 92
MWISHO