JE UNAMTAMBUA IMAMU MAHDI (A.S)
JINA NA UKOO WA IMAMU MAHDI (A.S)
Alikuwa ni mwana wa Imamu Hasan Askari,ambaye ni Imamu wa kumi na moja miongoni mwa maimamu wanaotokana na ukoo wa Mtume (s.a.w.) naye ametokana na kizazi cha Husain (a.s.), aliyekuwa mwana wa Fatima (a.s.) binti wa Mtume (s.a.w.) na Bwana Ali (a.s.) binamu wa Fatima (a.s) (Imani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao wote). Na Imamu Mahdi (a.s) mepewa jina Ia Mtukufu Mtume (s.a.w.) na ana umbo lifananalo na umbile la Mtume (s.a.w.w).
Mama yake ni Bibi Nargis (Narcissus), mjukuu (atokanaye na binti) wa Mfalme wa Urumi na naye anatokana na kizazi cha Simon, mwanafunzi wa Nabii Issa (a.s.).
MAJINA YA HESHIMA
Pengine Imamu Mahdi (a.s) ana majina mengi ya heshima na yu wa pili kwa wingi wa majina ya heshima baada ya Imamu 'Ali (a.s.). Majina yake ya heshima yaliyo maarufu sana ni:
1. Al-Mahdi “(Aliyeongozwa)". Jina hili linatumika badala ya jina lake na biashara nyingi za Mtume (s.a w.) na za Maimamu zinabashiria kuja kwake zimemtaja kwa jina hili. Hii ndiyo sababu kuwa imani ya kuja kwa Mahdi ina msingi katika madhehebu yote ya Kiislamu, ijapokuwa yanatofautiana madhehebu hayo katika maelezo ya jambo hilo la kuja kwa Imamu huyu (a.s).
2. Al-Qa’im. Jina hii limetokana na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.) zinazosema "Dunia haitafikia mwisho wake bila ya mtu mmoja katika ukoo wangu kusimama (maana halisi ya Al-Qa'im ni "mwenye kusimama dhidi ya dhulma)" na kuijaza dunia uadilifu.
3. Sahibuz-Zaman (Kiongozi wa Zama hizi).
4. Hujjatullah (Hoja au Dalili ya Mwenyezi Mungu).
5. Al-Muntadhar, (Anayengojewa).
Si katika Uislamu tu, bali hata katika dini zinginezo, na kwa majina na kwa kupitia majina mbali mbali zimeelezewa biashara zinazomhusu "Atakayekuja" (Imamu Mahdi a.s).
MWISHO