LIKO WAPI KABURI LA YESU
  • Kichwa: LIKO WAPI KABURI LA YESU
  • mwandishi: Dkt. Rashid
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 7:27:29 24-8-1403

BSMILAHI AR-RAHMANI AR-RAHIIMI

LIKO WAPI KABURI LA YESU Bismillah Al-Rahman Al-Rahiim

Wapendwa Wasomaji wa Qadiani/Ahmadiya Amani iwe juu ya wale wanaofuata uwongofu Mirza Ghulam Ahmad Qadiani, Mwasisi wa Jumuiya ya Ahmadiyah, alidai hivi: Mungu kanifunulia katika ufunuo maalum kuwa Masihi Ibn Maryam amekufa." (Tauzeeh-e-Maram, Roohani Khazain juz. 3 uk. 402). "Nimefahamishwa kaburi la Issa (nchini Kashmir). Na nimefahamishwa na Qur'an Tukufu pamoja na ufunuo wa Mungu kwangu kuhusu kifo cha Yesu." (Roohani Khazain juz 18 uk.358,361) Je hili ndilo kaburi la Yesu?

"Kaburi la Kristo" (7/24) Katika kitovu cha Ukristo, fumbo la muda mrefu kama ilivyo imani ya Ukristo, sasa liko jirani kufumbuliwa. Timu ya wataalamu wa mabaki ya kale kutoka Chuo Kikuu cha Oxford imekuwa katika pilikapilika kubwa za kujaribu kuthibitisha kuwa lile Kanisa la kaburi la Jerusalem ndipo mahali penyewe alipozikwa Yesu. Baada ya muongo mmoja, Martin Biddle na mkewe, Birthe Kj?lbye-Biddle, wame*****ua mabaki ya vitu vya kale katika eneo hilo pamoja na kaburi lenyewe la jabali la kuchongwa lililofichikana ndani ya kuta za kibanda au "kijumba" kilichokuwepo hadi karne ya 19. Kikiaminika kuwa ni alama ya kaburi la Kristo, kibanda hicho, mpaka sasa, bado hakijafanyiwa aina yoyote ya utafiti wa mabaki ya kale au uchunguzi wa kisayansi.

http://www.pbs.org/press/jul01/secretsofded.htm1
Sijui wewe ungelisemaje hili? Au je hili ndilo Kaburi la Yesu nchini Kashmir? Tovuti nyingine iitwayo "Tomb of Jesus" ("Kaburi la Yesu") inakwenda mbali zaidi kuthibitisha kuwa Kaburi la Yesu lipo Kashmir. Ingawaje mmiliki wa tovuti hiyo (Bwanakaburi) anakanusha kuwa na uhusiano na kundi lolote la kidini, lakini muda si muda nyau akatoka nje ya sanduku pale mmiliki wa tovuti hii alipokiri kwenye vyombo vya Ahmadiya kuwa yeye ni Ahmadiya na yuko jirani sana na Mirza Tahir, Khalifa wa Makadiani. Bwana huyo kaandika hivi: "Baada ya kunusurika kusulubiwa, Yesu akafika kule Kashmir ambako alijifanyia makazi kwa kipindi kilichosalia cha uhai wake. Huko akayachunga makabila ya Waisraili wa eneo hilo, akiendelea kuhubiri. Baadae akamuoa mwanamke mmoja aliyeitwa Maryan, ambaye alimzalia watoto, na hivyo, nadharia hiyo inasema, alikufa akiwa na umri wa miaka 120. Kaburi lake (tazama picha ya kaburi hili kwenye tovuti yetu) lipo katika wilaya ya Mohala Kan Yar ya mji mkuu wa Srinagar, Jammu&Kashmir, Kaskazini mwa India na linaitwa Roza bal ("eneo la Kaburi Tukufu").

http://www.tombofjesus.com/Welcomeall.htm
Bwana kaburi kaongeza hivi: "Tovuti hii, na taarifa zake, SI mali ya imani au itikadi au taasisi yoyote mahususi wala jambo hili la maisha ya Yesu baada ya tukio la kusulubiwa si uzushi wa mtu yoyote yule."
http://www.tombofjesus.com/Welcomeall.htm
Lakini mahali pengine bwana huyu anakiri mafungamano yake ya kidini: "Ni AIBU kuwa mtu anayedai kuwa AMEZALIWA Ahmadiya ASIUONE umuhimu wa Imam Mahdi! Kama hiyo ndiyo maana ya kuzaliwa Ahmadiya, BASI MIMI NAFURAHI kuwa sikuzaliwa hivyo, na kwamba nilikuja kubadili dini BAADAE!!" (chanzo: ujumbe wa tarehe 9/9/2000 unaohusu Bodi ya Ujumbe ya Ahmadiyya. "Kwa sababu mimi nilitokea tu kuamini kama wanavyoamini Ahmadiya: Kwamba Hazrat Ahmad alikuwa ni nabii *wa kweli* wa Mungu ambaye hawezi kuwekwa katika matabaka hayo." (chanzo: ujumbe wa tarehe 02/11/2000 kuhusu Bodi ya Ujumbe ya Ahmadiya Lahore.

"hebu "tujaalie" kuwa mimi ni Ahmadiyya wa Kiafrika. Kwa VIPI NIJALI kile anachohisi Mpakistan wa Punjub kuhusu mimi? Mathalani nilianzisha tovuti yangu PASIPO msaada wala ruhusa yao. Naye kiongozi wa Ahmadiya (au fulani ninayesikia) ameipa idhini yake binafsi tovuti hiyo." (chanzo: ujumbe wa tarehe 6/6/2000 kuhusu Bodi ya Ujumbe ya Ahmadiyya Lahore. Sasa nyau katoka sandukuni. Basi tena....... Wafuasi wote wa Kadiani (wale wa Lahori na Kadiani) wanaamini kuwa Yesu Kristo (Sayyidina Issa Ibn Maryam (as)) alikufa na kuzikwa Kashmir. Nini msingi wa imani hii? Bila shaka, kwa sababu mwasisi wenu, nabii wenu, masihi wenu aliyeahidiwa, imam mahdi wenu na kadhalika na kadhalika, kasema hivyo. Je niko sahihi?

Bwanakaburi anasema: "Umuhimu wa Hazrat Ahmad uko wazi kabisa, na unakubaliwa na mtu yeyote anayesoma na kuelewa historia ya nadharia ya maisha ya Yesu baada ya tukio la kusulubiwa: Hazrat Ahmad ndiye mtu wa *kwanza* kutambuliwa ambaye alitoa ufafanuzi wenye mtiririko na uwiano juu ya nadharia hii. Kila mwandishi wa Yesu ndani ya India analitambua hili. Yeye (Mirza) ndiye aliyefichua maandiko ya Mulla Nadri na wengineo: alivitumia vipaji vyake vikubwa vya kiroho NA kiakili, kukusanya taarifa kutoka vyanzo vya Waislamu, Wahindu, Mabudha na vinginevyo ikiwa ni pamoja na vitabu vya historia, historia simulizi, historia andishi, n.k na akakusanya vyote hivi pamoja katika muundo wa Kitabu na kwa mtiririko. *Hakuna mtu* katika historia ya mwanadamu aliyefanya hivyo kabla yake. Ndiyo maana anastahili kutambuliwa kama ndiye yule mtu ambaye Mtume Muhammad alisema "atavunja-vunja msalaba"." (chanzo: ujumbe wa tarehe 9/9/2000 kuhusu Bodi ya Ujumbe ya Ahmadiyya Lahore)

Je kuna Kadiani yeyote aliyewahi kuchambua maandiko ya Mirza Ghulam, kujua kile hasa ambacho ameandika kuhusu mahali alipozikwa Yesu? Nina hakika hakuna yeyote kati yenu aliyefanya hivyo, na kama mmefanya hivyo, basi yote hiyo ni nyongeza tu ya kampeni kubwa ya uwongo, au la basi huko ni kukwepa kwa makusudi kuukabili ukweli.. Hebu sasa nikwambieni kile nilichokigundua mimi katika maandiko ya Mirza Ghulam. Bila shaka, mna hiyari ya kukubaliana au kutokubaliana nami, lakini tafadhalini, tafadhalini, hiyo iwe ni baada tu ya kuwa mmeshathibitisha nukuu nilizokupeni. Jukumu langu mimi si jingine ila ni kuwasilisha ujumbe, baada ya hapo ni baina yenu na MwenyeziMungu.

Katika vitabu vyake mbalimbali, Mirza Ghulam A. Qadiani, ametaja mahali patatu tofauti penye kaburi la Yesu. Wapi mahali sahihi?

1.Yesu AS alizikwa Al-Khaliili (Guilailii) Mnamo mwaka 1891 Mirza aliandika juzuu kubwa, Izala Auham, ambayo ilifikia kurasa 948. Katika juzuu ya pili ya kitabu hiki, akaandika ufafanuzi wa kina na wa ajabu mno akijaribu kuthibitisha kuwa Yesu hakunyanyuliwa kimwili kwenda mbinguni (kama wanavyoamini Waislamu), bali alishushwa msalabani, akaenda kwao, Al-Khalil, akafa na kuzikwa huko. Mirza kaandika hivi: "Hii ni kweli kuwa Masihi alikwenda mahali pa asili yake, na akafia huko, lakini hii si kweli kuwa mwili huo uliozikwa, ukawa tena hai....aya ya 3 sura ya 1 ya Matendo ni uthibitisho kuhusu kifo cha kawaida cha Yesu kilichotokea Al-Khaliil. Baada ya kifo hiki, Masihi aliweza kuonwa na wanafunzi wake kama kivuli (KASH) kwa siku 40." (Izala-e-Auham, Roohani Khazain juz.3 uk.353-354).
1. Kaburi la Yesu Quds Hata hivyo, miaka mitatu baadae, mnamo mwaka 1894, Mirza akabadili hadithi yake. Katika kitabu chake kingine, Atmam-e-Hujjat (Roohani Khazain juzuu ya 8) akajaribu kwa mara nyingine tena kuthibitisha kuwa Isa Ibn Maryam (as) kafa. Katika jaribio la kuthibitisha hilo, alitoa uthibitisho wa mmoja wa wanafunzi wake wa nadra wa Kiarabu, Molvi Mohammed Al-Saiidi Trabilisi Al-ashaami. Kaandika hivi: "Hii hapana budi ikubalike kuwa Sayidina Isa naye pia kafa, na cha kuvutia zaidi kaburi lake pia liko Syria na kwa ufasaha zaidi, katika tanbihi, najumuisha na ushahidi wa ndugu Yangu, Kipenzi changu kwa Allah, Molvi Mohammad Al-Saiidi Trablisi. Yeye ni mkaazi wa Tripoli, katika nchi ya Syria na kwenye eneo lake ndipo lilipo kaburi la Sayidina Isa AS (Yesu). Mkisema kuwa Kaburi hilo sio lenyewe, basi inawabidi mtoe uthibitisho wa kuwa hili silo, na mthibitishe udanganyifu huu ulitokea lini. Na kwa kitendo hiki, hatutakuwa na uhakika wa makaburi ya nabii yeyote yule na imani ndio basi itapotezwa, na itatubidi tuseme kuwa makaburi yote si yenyewe." Atmam E. Hujat, Uk: 18-19, Roohani Khazain juz.8 uk. 296-297, tarehe 1894.

Barua ya Molvi Mohammed Al-Saiidi Trabilisi: "Ewe Hazrat Maulana & Imamu wangu. Assalaam alaikum wa rahmatullah wa barakatuhu. Namuomba MwenyeziMungu akupe tiba (Nilipokea barua hii ya Shaami Saheb wakati nikiumwa). Vyovyote ambavyo umeuliza kuhusu Kaburi la Isa alaihi assalam na mambo mengine, ndivyo ninavyokuandikia kwa kina, navyo ni hivi: Sayidina Issa alaihi assalam alizaliwa kule Bait-ul-Lehm ambapo baina ya Baitul-hehm na Quds kuna umbali wa maili thelathini na Kaburi la Sayidina Isa alaihi assalam lipo katika Nchi ya Quds, na lipo hadi hivi sasa, na kuna Kanisa lililojengwa juu yake, na kanisa hilo ndilo kanisa kubwa kabisa kuliko makanisa yote, na ndani yake mna Kaburi la Sayidina Isa na mumo humo ndani ya kanisa mna Kaburi la Maryam, Mkweli. Na makaburi hayo mawili yametengana." (Atmam-ul-Hujjat, Roohani Khazain juz.8 uk. 299).

Hiyo inaonekana kumaliza jambo hili. Kwa mtazamo wa Mirza, Yesu alikufa na kaburi lake lilikuwa kule al-Quds. 1.Kaburi la Yesu kule Kashmir: Hata hivyo, miaka minane baadae, Mirza akabadili tena hadithi. Sasa akaanza kueneza nadharia yake mpya: Yesu kazikwa Kashmir. Inathibitika kwa yakini kuwa Isa AS (Yesu) alihamia Kashmir. Baada ya vile MwenyeziMungu kumkomboa kwa rehema zake na kumuweka aendelee kuishi huko kwa muda mrefu hadi alipofariki na akajumuishwa miongoni mwa wafu. Na kaburi lake bado lipo mpaka leo katika mji wa Srinagar (Kaburi la Yus Asif)" (Al-Huda, 12 Juni 1902, uk. 109) "Nimefahamishwa kuhusu kaburi la Isa (kule Kashmir)." (Roohani Khazain juz.18 uk. 358, 361).
"Kaburi la Yesu lipo Kashmir." (Roohani Khazain juz. 18 uk.320.Nuzool-e-Maseeh, kilichopigwa chapa mwaka 1909, baada ya kifo cha Mirza) Hivyo basi, tuna kauli tatu tofauti za Mirza Ghulam Ahmad Qadiani kuhusiana na kaburi la Yesu. Swali langu kwa Makadiani ni ipi kati ya kauli hizo ni sahihi? Al-Khalil au Quds au Kashmir? Amani iwe juu ya wale wanaofuata uwongofu.

MWISHO