IMAMU ALI (A.S) KATIKA MTAZAMO WA WASIOKUA WAISLAMU
Simon Ockley
(1678-1720) Profesa wa lugha ya kiarabu katika chuo kikuu Cambridge:
" "Jambo moja maalum ambalo lapaswa kugunduliwa kwa Ali, ni kwamba mama yake alimzaa Makka ndani ya Al-Kaaba, ambapo haijawahi kutokea kwa mtu yeyote."
[History of the Saracens, London, 1894, Uk. 331]
Washington Irving
(1783-1859) Aalijulikana kama "The first American man of letters":
"Ali alikuwa anatokana na tawi lenye heshima kuu katika matawi ya kikureishi. Alikuwa na sifa tatu zilizokuwa zikitukuzwa sana kwa waarabu: Ujasiri, ufasaha na ukarimu. Moyo wake usio na hofu ulimpatia sifa kutoka kwa Mtume ya kuwa simba wa Mungu, mifano ya ufasaha wake imebaki katika baadhi ya semi na kuhifadhiwa miongoni mwa waarabu; na ukarimu wake ulionekana dhahiri katika kupenda kwake kugawanya na watu, kila siku ya ijumaa, kile kilichobaki katika hazina. Kuhusu utukufu wake, tumetoa mifano mara kwa mara; utukufu wake ulichukia kila kitu chenye udanganyifu na uchoyo."
[Lives of the Successors of Mahomet, London, 1850, Uk. 165]"
"Yeye alikuwa ni mmoja wa miongoni mwa wa mwisho na wenye thamani miongoni mwa waislamu wa kale, ambaye alikusanya nguvu ya kidini kwa ushindi akiwa na Mtume mwenyewe, na kufuata ruwaza ya mwisho kabisa ya Mtume Muhammad. Yeye ni mtu anayetajwa kwa heshima kama khalifa wa kwanza aliye kirimu na kulinda elimu. Alikuwa ndani ya mashairi yeye mwenyewe, na nyingi miongoni mwa methali na semi zake zimehifadhiwa na kufasiriwa katika lugha mbalimbali. Pete lake ulikuwa na maandishi hili: 'Ufalme ni wa Mwenyezi Mungu'. Moja katika semi zake inaonyesha jinsi alivyokuwa hathamini vivutio vinavyopita tu vya dunia, ni (kusema kwake): 'Maisha ni kivuli tu cha mawingu - ndoto ya mwenye kulala.'"
[Lives of the Successors of Mahomet, London, 1850, Uk. 187-8]
Robert Durey Osborn
(1835-1889) Meja wa kikosi cha the Bengal Staff Corps:
" "Pamoja naye umepotea moyo hasa na Muislamu bora ambaye Historia ya Mohammad imehifadhi kumbukumbu hiyo." [Islam Under the Arabs, 1876, Uk. 120]
Namna hii anakubainishieni Mwenyezi Mungu Aya zake ili mpate kufahamu (Qur'an 2:242)
Wasiokuwa Waislamu wanasema nini juu ya … 'Ali
MRITHI WA KWANZA WA MTUME MUHAMMAD (Rehma na amani ziwe juu yao)
Imam Ali bin Abi Talib alikuwa ni mrithi wa Mtume Muhammad, amani ziwe juu yao. Huu ni mkusanyiko wa nukuu fupi fupi kumhusu yeye kutoka kwenye maelezo mbali mbali ya wasomi wa imani nyingine, wakiwamo wanataaluma, waandishi, wanafalsafa, washairi, wanasiasa na wanaharakati.
Thomas Carlyle
(1795-1881) Mwanahistoria mskochi, mkosoaji, na mwandishi wa elimu ya jamii:
" "Kuhusu huyu kijana Ali, mtu yeyote atampenda tu. Ni kiumbe mwenye akili kuu, kama anavyojionyesha yeye mwenyewe sasa, na kila siku na baadaye; mwenye mapenzi maridhawa, mwenye ujasiri wa hali ya juu. Ana uungwana; shujaa kama simba; huku akiwa na huruma, ukweli na mapenzi yafaayo kwa imani ya kikristo."
[On Heroes, Hero-Worship, And the Heroic in History, 1841, Hotuba 2: The Hero as Prophet. Mahomet: Islam., Mei 8, 1840)]
Edward Gibbon
(1737-1794) Mwanahistoria mkuu wa kiingereza katika enzi zake:
" "Sifa kuu alizokuwa nazo Ali hazikuzidiwa na mbadilishaji dini yeyote wa siku za hivi karibuni. Alichanganya sifa za kuwa ni mshairi, mwanajeshi, na mcha Mungu; busara zake bado zinapatikana kwenye mkusanyiko wa misemo yake ya kimaadili na ya kidini; na kila adui, kwenye vita vya maneno au vya upanga, alishindwa na ufasaha na ujasiri wake. Kuanzia saa ya mwanzo ya ujumbe wake wa dini mpaka mwisho wa ibada za kuzikwa kwake, Mtume Muhammad hajaachwa kuwa na rafiki mkarimu, ambaye alifurahishwa kwa kumwita kuwa ni ndugu yake, wasii wake, na kuwa yeye (Ali) ni 'Harun mwaminifu' wa 'Nabii Musa' wa pili."
[The Decline and Fall of the Roman Empire, London, 1911, Juz. 5, Uk. 381-2]
Philip Khuri Hitti
(1886-1978) Profesa wa lugha za kisemiti, Chuo kikuu cha Princeton:
" "Shujaa vitani, mwenye busara katika ushauri, fasaha wa kuzungumza, mkweli kwa marafiki zake, anayeheshimiwa na maadui zake. Yeye alikuwa ni ruwaza wa heshima na maadili mema ya kiislamu. Na alikuwa ni Suleiman wa utamaduni wa kiarabu, ambapo kwake mashairi, methali, hotuba na simulizi - zisizo na idadi - zimekusanyika."
[History of the Arabs, London, 1964, Uk. 183]
Sir William Muir
(1819 - 1905) Msomi na kiongozi wa kiskochi. Alikuwa na wadhifa wa Waziri wa mambo ya nchi za nje katika serikali ya India, pia alikuwa Lieutenant Gavana wa mkoa wa Kaskazini Magharib:
" "Alijaaliwa kipaji cha maarifa, mwenye mapenzi, na mwenye kujifunga na urafiki, tangu uvulana wake alikuwa amejitolea roho na moyo wake kwa Mtume. Mnyenyekevu, mpole, na asiyependa makuu. Ambapo baada ya kupita siku kadhaa, alipotawala nusu ya ulimwengu wa kiislamu, kwa hakika alilazimishwa pasi na kutaka."
[The Life of Mahomet, London, 1877, Uk. 250]
Dr. Henry Stubbe
(1632-1676) Muhafidhina, Mwanafizikia, na mwanafalsafa:
" "Hakuipenda dunia na mapambo yake bali alimcha sana Mwenyezi Mungu, alitoa sadaka nyingi, alikuwa mwadilifu katika vitendo vyake vyote, mnyenyekevu na mwepesi wa kuzoeana na watu; huku akiwa na maneno ya ya haraka ya kufurahisha na ubunifu usio wa kawaida, alikuwa na elimu maridhawa, sio elimu zinazoishia kwa maneno tu bali zinazoendelea kwa vitendo." [An Account of the Rise and Progress of Mahometanism, 1705, Uk. 83]
Gerald de Gaury
(1897 - 1984) Mwanajeshi mahiri na mwanadiplomasia:
" "Alikuwa ana hekima sana katika kutoa ushauri, na shujaa vitani, mkweli kwa marafiki zake na mkarimu kwa maadui zake. Yeye daima alikuwa ni ruwaza ya heshima na maadili mema ya kiislamu."
[Rulers of Mecca, London, 1951, Uk. 49]
Wilferd Madelung
Profesa wa lugha ya kiarabu, chuo kikuu cha Oxford:
" "Kwenye madai ya uongo ya Bani Umayya ya kuuhaalisha utawala wa Mwenyezi Mungu kuwa wao ni makhalifa wa Mungu duniani, na ulaghai wao na serikali yao yenye mizozo na kulipiza kisasi, pamoja na hayo yote, waliukubali uaminifu wake kutolegalega kwake na kujitolea katika kuutumikia uongozi wa kipindi hicho wa kiislamu, uaminifu wake binafsi, kuwatendea usawa wote waliomuunga mkono na pia ukarimu wake wa kuwasamehe maadui wake aliowashinda."
[The succession to Muhammad: a study of the early caliphate, Cambridge, 1997, Uk. 309-310]
Charles Mills
(1788 - 1826) Mwanahistoria bingwa wa enzi zake:
" "Akiwa ni kiongoazi wa familia ya Hashim na binamu na mkwe wa (Mtume) ambaye waarabu walimheshimu… inashangaza kuwa Ali hakuandaliwa kuwa khalifa mara tu bada ya kufa Muhammad. Pamoja na heshima ya kuzaliwa kwake na ndoa yake, pia alikuwa na urafiki na Mtume. Huyu mtoto wa Abu Talib alikuwa ni wa mwanzo kuingia Uislam na alikuwa ni kipenzi cha Mohammad, kwani alikuwa ni wa pili kama alivyokuwa Harun kwa Musa. Kipaji chake kama msemaji, na ujasiri wake kama shujaa, vilitukuzwa na taifa ambalo ujasiri ulikuwa ni sifa njema na ufasaha ulikuwa ni busara."
[An history of Muhammedanism, London, 1818, Uk. 89]
MWISHO