BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM
IBADA ZA MATAMSHI
1- Kuzitamka Shahada Mbili
Hauwi sahihi Uislamu wa mtu iwapo hajazitamka shahada mbili, isipokuwa bubu ambaye vinatosheleza vitendo vyake vitakavyoonyesha dalili ya imani yake. Mtume (SAW)amesema:
Nimeamrishwa nipigane vita mpaka watu washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni Mtume wa MwenyeziMungu na wasimamishe Sala na Watoe Zaka. Watakapotimiza hayo watakuwa wamezuilika kwangu damu zao na mali zao ila kwa haki ya Uislamu [6]na hesabu yao itakuwa kwa MwenyeziMungu>>. (Bukhari na Muslim).
2- Kumtaja na kumtukuza Mungu
Kumdhukuru(kumtaja) MwenyeziMungu, Kumsabihi(kumtukuza) na Kumwomba Maghufira MwenyeziMungu anasema:
"Enyi mlioamini! Mkumbukeni MwenyeziMungu kwa wingi na mtukuzeni asubuhi na jioni". (Al - Ahzab -41 -42) Na akasema:
"Na ili muombe msamaha kwa Mola wenu, kisha mtubie(mrejee) kwake. Atakustarehesheni kwa starehe nzuri mpaka mda maalum (mtapoondoka ulimwenguni). Na atampa (akhera) kila mwenye fadhila, fadhila yake, na kama mtakengeuka basi nakukhofieni adhabu ya (hiyo) siku kubwa." (Hud-3)
Na akasema:
"Basi (hapo) mtakase Mola wako pamoja na kumsifu na umuombe maghfira (msamaha) ; hakika Yeye ndiye Apokeaye toba ". (Nasr -3) 3- Dua Na Kuomba Msaada
Atakayeomba dua, au msaada, hatokuwa mwenye akili (iwapo atamwomba asiyemsikia) isipokuwa huyo anayemuomba awe ni mwenye kumsikia na kuwasikia wengine kila wakati, kila mahali na kwa kila lugha. Hatokuwa mwenye akili isipokuwa awe na yakini kwamba yule anayemuomba anao uwezo kwa njia za ghaibu wa kulijibu ombi lake na kumfariji dhiki zake, na awe na uwezo wa kimiujiza unaoweza kufanya jambo lolote katika ulimwengu huu. Mwenye uwezo huu hawezi kuwa mwingine isipokuwa MwenyeziMungu. Hawezi kuyafanya haya kiumbe chake chochote, aliye hai au aliyekwisha kufa.
Mwenye kuamini kwamba asiyekuwa MwenyeziMungu anao uwezo wa kufanya lolote katika hayo, kisha akamulekezea dua yake, basi atakuwa amefanya kiendo cha Shirki. MwenyeziMungu anasema:-
"Huyo ndiye MwenyeziMungu, Mola wenu, Mwenye ufalme, na wale mnaowaabudu kinyume chake, wao hawamiliki hata utando (ngozi) wa kokwa ya tende, kama mkiwaomba hawatakujibuni na siku ya kiyama watakataa ushirika wenu wala hatakuambia kama (akuambiavyo MwenyeziMungu) Mjuzi wa kweli kweli". (Fatir - 13 - 14)
Na anasema:-
"Na Mola wenu akasema "Niombeni nitakujibuni". Kwa hakika wale wajivunao kufanya ibada yangu bila shaka wataingia Jahannam, wadhalilike". (Al - Muumin - Ghafir- 60). Na akasema:-
"Na waja wangu watakapokuuliza hakika yangu Mimi niko karibu nao. Naitikia maombi ya muombaji anaponiomba. Basi waniitikie na waniamini ili wapate kuongoka". Al - Baqarah - 186
Iwapo mjinga yeyote ataelekeza dua yake kwa mwengine asiyekuwa MwenyeziMungu, basi ni wajibu wa anayeelewa kumbainishia, na anapaswa huyo asiyeelewa kufuata na kuiokoa nafsi yake isiingie katika Shirki.
4- Kuapa Kwa Jina La MwenyeziMungu
Mwislamu hali kiapo isipokuwa kwa jina la MwenyeziMungu, kwa sababu ya kumtukuza na kumheshimu. Mtume wa MwenyeziMungu (SAW) amesema:
Bukhari, Muslim, Ahmad na Annasai
Atakaekula kiapo kwa asiyekuwa MwenyeziMungu, akamtukuza kama anavyotukuzwa MwenyeziMungu na akamwogopa kama anavyomuogopa MweyeziMungu basi atakuwa amefanya kitendo cha Shirki. Mtume (SAW) amesema:-
Attirmdhiy, Ibn Majah, Ahmad, Annasai, na Addarimy Pia haijuzu mtu kuapa kwa 'Amana'. Mtume (SAW) amesema:
Ahmad na Abu Daud.
5- Kulingania watu
Kulingania Watu Katika Njia Ya MwenyeziMungu, Kuamrisha Mema Na Kukataza Mabaya MwenyeziMungu anasema:- "Ni nani asemaye kauli bora zaidi kuliko aitaye viumbe (viumbe) kwa MwenyeziMungu na (mwenyewe) akafanya vitendo vizuri na kusema: "Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu". Haa - Miym - Sajdah (Fussilat -33 )
Na anasema:-
"Sema": Hii ndio njia yangu; ninaita (ninalingania) kwa MwenyeziMungu kwa ujuzi wa kweli; mimi (nafanya hivi) na (kila) wanaonifuata. Na MwenyeziMungu ametakasika na kila upungufu, wala mimi simo miongoni mwa wanaomshirikisha (MwenyeziMungu)". (Yusuf - 108). Na anasema;
"Na wawepo katika nyinyi watu wanaolingania kheri (Uislamu) na wanaoamrisha mema na wakakataza maovu na hao ndio watakaotengenekewa". (Aal - Imran -104)
MWISHO