MAMBO YASIYO FAA
  • Kichwa: MAMBO YASIYO FAA
  • mwandishi: Abu-Muslim
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 4:40:36 3-11-1403


BISMILLAHIR-RAHMAANIR-RAHIIM

MAMBO YASIYO FAA
Asalaam alaikum warahmatullahi wabarakatuh.
Shukran zote anastahiki Allah (S.W.T) na rehema na amani zimshukie bwana wetu Muhammad (S.A.W).

HUU NI UJUMBE, NA ANAESOMA UJUMBE HUU AMFIKISHIE MWENZIWE KWA NJIA YOYOTE ILE ILI TUSIWE NA DHIMA MBELE YA ALLAH.

Allah (S.W.T) anasema katika Qur-aan suratul Al Imran aya 31: 31. Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakufutieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta madhambi na Mwenye kurehemu. ***

32. Sema: Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na wakigeuka basi Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri. ***
Na hadithi ya Mtume wetu (S.A.W) inaeleza hivi:
Watu wote wataingia peponi ila asietaka,masahaba wakaumuuliza ewe mjumbe wa Allah, nani hao wasiotaka? Rasuul (S.A.W) akasema atakae nitii ataingia peponi na atakae niasi ataingia motoni. Hoja ninayoitaka kuieleza ina umuhimu katika maisha yetu na ambayo kila kukicha mambo yanazidi kugeuka na kubadilika sura.Na kama tukiachia hali hii iendelee tutafika mbali.

VIPI TUNAFUNGA NDOA???
Hili ni moja kati ya masuala muhimu ya kuulizwa wakati huu tulionao hivi sasa.Kwasababu NDOA ina muhimili mkubwa wa maisha ya jumla ya binadamu.Ikisimama ndoa sawa sawa basi nusu ya maisha ya binadamu yako sawa.Na ikiharibika ndoa basi na maisha ya binadamu yapo hatarini kuharibika. Suala ni vipi TUNAFUNGA NDOA na VIPI TUNASHEREHEKEA NDOA ZETU,Tunafuata Qur-aan, sunna, hadithi au Mayahudi na Manasara ?

Mtume wetu (S.A.W) alijaaliwa kuwa na watoto, na baadhi yao waliwahi kuwafikia balegh na kuolewa.Na aliwaozesha watoto wake kwa mahari madogo.Na kutoa sadaqa ya chakula kwa watu.Kama ilivyokuja katika hadithi. TUANGALIE JEE …MAMBO TUNAYOYAFANYA SISI HIVI LEO NI SAWAA???
1. KUSOMA DUA YA POSA - wanawake kualikana,kupikwa israfu ya vyakula yasio kuwa na idadi,kununuliwa maguo ya thamani ya ghali.
2. POSA - wanawake ndio wanaopeleka posa badala ya wanaume.Kualikana,shangwe na maguo ya thamani ya ghali kuandaliwa,israfu ya vyakula na muziki.
3. KUPELEKA SANDUKU LA HARUSI - Kualikana, kushona nguo za ghali, israfu ya vyakula na muziki.

4. KUPANGA HARUSI - Kualikana, kushona nguo za ghali, israfu ya vyakula na muziki
5. KUTIA HINA - Kualikana, kushona nguo za ghali, vyakula na muziki.
6. SHEREHE YA HARUSI - Kushona nguo za ghali,israfu ya vyakula na muziki.Sherehe kufanywa kwenye maholi ya mahoteli ya kifakhari kwenye usiku wa manane wake za watu na watoto wa kike wako nje.
7. MITINDO YA NGUO - Moja ya ishara ya kiama ni kwamba wanawake watajiona wamevaa nguo kumbe wako utupu.Haya ndio yaliopo hivi sasa.Nguo zivaliwazo na ndugu zetu,watoto wetu na mama zetu ni aibu na fedheha tupu kusema na waislamu.

8. KUVISHANA PETE - haya hayakuja katika sunna ya bwana wetu Mtume Muhammad (S.A.W).
9. KUKATA KEKI - Na haya pia hayakuja katika sunna ya mtume wetu.Na hizo keki ni kufuru tupu jinsi zinavyotengenezwa.Na mwisho wake ni kutupwa kwenye dust bin.
10. HONEY MOON - Huu ni uzushi mwengine kati ya uzushi tunaoiga bandu bandu wa mila za kiyahudi na kinasara kama hizo za kukata keki na kuvishana pete. Haya ni machache tu ambayo tunayujua na tunayasikia kwamba yanatendeka katika harusi zetu za KIISLAMU, pengine yako mengi mengine ambayo hatuyajui. Allah (S.W.T) ametwambia katika Qur-aan katika suratul Baqra aya 120:
120. Mayahudi hawawi radhi nawe,Mayahudi wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu. ***

Hapana budi tuzinduke ndugu zangu Waislamu kwani huu sio mwendo alokuja nao Mtume (S.A.W) ila ni mienendo ya Kiyahudi na KIkristo.Na Allah (S.W.T) anatutahadharisha kwamba tukiwacha uongofu wake na kufuata wa hao Mayahudi na Makristo hatutapata mlinzi wala msaidizi siku ya Kiama. Sheitani na wapambe wote waliotushawashi kufanya yalio kinyume na Dini yetu wataturuka siku hio.Kila mtu atakuwa na mzigo wake mwenyewe.Wacha watu watuseme na watukasirike lakini tusikubali kuingizwa ndani ya Jahannam kwa matamanio ya nafsi zetu au nafsi zao.

YAKUZINGATIA:
Mtume wetu kasema: Ficheni POSA zenu na dhihirisheni NDOA zenu.Na toeni sadaqa ya chakula. Haya ndio sunna ya Mtume wetu,sio hayo tunayoyafanya sisi,tangu posa inajulikana leo watu wanasoma dua ya posa,leo wanakwenda kuposa.Hivi sivooo!!!!!

Na si lazima harusi kufanywa kwenye maholi na kualika mamia ya watu na kuwatoa wanawake majumbani usiku kwenda kuzurura mahotelini.Ni bora kufanya nyumbani na kualika wanaostahiki kualikwa na hasa ukizingatia ni kutoa sadaqa ya chakula ni nani anaestahiki kupewa hio sadaqa.

Na la msingi jengine ni kupunguza bei ya kuwauza watoto wetu wa kike wanapokuja kuposwa kutoka maelfu ya mapesa na kufanya sunna ya Mahari ya kitu kidogo tu na sio biashara.Kufanya hivo ndio mwendo wa Rasuul.Mtume kasema mwanamke mwenye barka ni mwenye kuolewa kwa mahari madogo.Leo watoto wakike wamejaa majumbani wanasubiri kuolewa hamna mwenye uwezo wa kuwaoa kwani moja ya sababu ni kutozwa mahari makubwa..

Namuomba Allah (S.W.T) anisamehe popote nilipokosea kwani yeye ndiye mjuzi na mwenye kusamehe. Alhamdulillah nimefikisha ujumbe.
Wabillahi at tawfiq,
Akhuukum:
a ngozi zao wakati wanaposikia jambo. Wanasayansi wana matumaini kwamba ugunduzi wao huo utafungua njia ya kuimarishwa vifaa vya mawasiliano kwa ajili ya watu wasiosikia vyema.
MWISHO