TABIA NJEMA NA ATHARI ZAKE KLATIKA UISLAMU
  • Kichwa: TABIA NJEMA NA ATHARI ZAKE KLATIKA UISLAMU
  • mwandishi: Salim Said Mwaegah
  • Chanzo:
  • Tarehe ya Kutolewa: 0:38:43 7-10-1403

 

NAFASI YA TABIA KATIKA MWENENDO WA MTUME
Mambo matatu ambayo yanajulikana kuwa ndiyo sababu ya kuhuika na kuendelea kwa dini tukufu ya uislamu ni,

1.    Tabia ya bwana mtume(saww): jambo hili limechukuliwa kama ni muhimu katika kuendelea kwa uislamu. Mwenendo mzuri wa mtume(saww) na bashasha katika mazungumzo yake ,na hakuwaponda maadui zake na aliwaheshimu.

2.    Kujitolea imam Ali(as) katika kuulinda uislamu.

3.    Mali ya bibi khadija.

Hapa katika makala haya tutazungumzia kuhusu tabia ya bwana mtume(saww), ambayo ni nguzo muhimu sana katika kuendelea uislamu. Qur’an inatueleza jinsi tabia ya mtume(saww) ilivyosaidia kueneza  uislamu na kuzivuta nyoyo za watu katika kuukubali uislamu.

“Ewe mtume,kwa rehma ya mola ilokufikia umekuwa ni mpole kwa watu,na kama ungekuwa na moyo mgumu watu wangekukimbia,basi wasamehe na uwaombee msamaha na ushauriane nao katika mambo”

Kwa kuangalia aya hii tunaweza kusema kwamba ,tabia nzuri:

1.    Ni zawadi toka kwa mwenyezi Mungu.

2.    Wenye mioyo migumu hawawezi kuwavuta watu katika jambo.

3.    Kiongozi bora ni yule  mwenye mvuto kwa watu.

4.    Wote waliokimbia katika vita na wakaomba msamaha basi wasaidwe(kuhusu jambo hili ni ile aya inayowataja wale waliokimbia katika vita vya uhudi).

5.    Kushauriana na watu juu ya mambo yaliyo na umuhimu,ni jambo linalojenga umoja na ushikamano.

Pamoja na kuwa alikuwa akitangaza tabia yeye mwenyewe alikuwa ni msitari wa mbele katika kuhakikisha kuwa anatekeleza kwa vitendo mambo yote aliyokuwa akiwafahamisha watu na kutaka ayaige toka kwake. Katika mwaka wa tisa wa hijiria, wakati waislamu walipokabiliana na kabila la twei na waislamu kushinda;A’ad bin Hatham mkuu wa kabila hili alikimbia Sham, lakini dada yake ajulikanaye kwa jina la Safaana  alikamatwa mateka na waislamu, pamoja na mateka wengine alifikishwa Makka karibu na msikiti na kupewa sehemu ya kukaa. Siku moja mtume(saww) alipokwenda kuwatembelea mateka, safaana alitumia fursa hiyo kuongea na mtume na kumwambia;

“Ewe Muhammad,kama uko tayari niache huru  na minishutumu kama yanavyoshutumia makabila ya waarabu,mimi ni mtoto wa mtu mkubwa katika jamii,baba yangu aitwae Hatam alikuwa akiwaacha huru wakuu wa makabila, na akiwapa watu chakula, na akiwasaidia watu katika matatizo” kwa maneno hayo mtume akawaambia mwacheni huru binti huyu hakika baba yake alikuwa  akipenda tabia njema”

Mtume akamnunulia nguo nzuri na kumpa pesa za safari na kumuambatanisha na watu waaminifu kwenda Sham kuungana na kaka yake. Mtumw katika kila nyanja ya maisha yake kumejawa na tabia njema kama anavyosifiwa katika Qur’an:

“na bila shaka unatabia njema,tukufu”

Hapa tutaangalia baadhi ya mifano:

1.    Uday bin Hatam anasema baada ya kukimbilia Madina na dada yake Safaana kuwa mateka katika mikono ya waislamu ulipita mudam mrefu na mara siku moja dada yake akiingia Sham na alimlaumu kwa kumwacha akiwa mateka,nikamuomba msamaha na baada ya siku kadhaa nilimuuliza umemuonaje mtu huyo anayeitwa Muhammad? Naapa kwa mola nimemuona ni mtu mwerevu,ni bora ukajiunga naye,nikaona hili ni jambo jema nikaanza safari kuelekea Madina kwa lengo la kuingi katika uislamu.

Mtume alikuwa msikitini pale nilipomsalimia akanijibu na kuniuliza ni nani wewe? Nikamwambia ni A’ad bin Hathim,akainuka na kunipeleka nyumbani kwake.njiani alikutana na bibi kizee aliyekuwa na shida,mtume akachukuwa muda mwingi kumuelekeza bibi yule jinsi ya kutatua haja zake,nikasema mwenyewe, naapa kwa Mungu huyu si mfalme. Kisha tukafika nyumbani kwake,akanikaribisha na kunikirimu na kunikalisha juu ya jani la mtende, naye mwenyewe kukaa chini,nikajisemea mwenyewe hii ni alama nyengine ya huyu mtu si mfalme. Kisha akazungumzia juu ya swala kuhusu dini yangu ambalo lilikuwa ni siri kwangu,nikafahamu kuwa alikuwa ni mjuzi wa siri,hapo hapo nikasilimu.

Katika vita vya khaibar katika mwaka wa saba wahijiria,baada ya waislamu kushinda, mayahudi wengi walikuwa mateka katika mikono ya waislamu,mmoja kati yao alikuwa ni Swafiyya mtoto wa Huyyi bin Akhtwab(msomi mkuu wa kiyahudi),Bilal aliwachukuwa nawanawake wengine nakuwapeleka kwamtume. Njiani akawapitisha katikasehemu ilipowekwa miili ya mayahudi walio uwawa katika vita,Swafiyya baada ya kuona hivyo alilia sana kwa uchungu. Walipofika kwa mtume akamuuliza Swafiya sababu ya kumkosesha raha,akaelezea jinsi alivyopitishwa katika maiti za mayahudi, mtume akamwambia Bilal:

“Ewe Bilal je!Huruma imeondoka katika moyo wako? Pale kuwapitisha kwako wanawake wawili katika maiti za watu wao”

Ajabu ni kwamba katika kulipa haya aliyofanyiwa Swafiya, mtume alimuacha huruna kisha baadaye alimuowa.

Katika vita vyahunaynimnamomwakawananehijiria,Shiimaamototowa Halima (dada wakunyonyanamtume)alikamatwamatekanawaislamu,mtumeakamwambia,ukitakakubakinasisiunawezakubakinakamahutakinitakurudishakwawatuwako. Shiimaakakhiyarikurudikatikawatu wake.MtumeakawaachahurukijakazimmojanamtumishinawakaowanakishawotewawiliwakawawatumishikatikanyumbayaShiima(5).

Imam Swadiq(as) anasemakatikakuhusinanaakhlaqya bwana mtume(saw) kuwasikummojamtumealikuwaanasalisalayaadhuhurinawatuwengiwalijiunganasalayake,ghaflawalimuonamtumeakisalirakaambilizamwishokwaharakasana,wakatakakujuwakunajamboganilililotokea? Baadayasalawakamuuizamtumesababuyakuswalikwaharaka,akawauizamtume je hamkusikiasautiya motto analiainaonekanahakukuwanamtuwakumbembelezakwahiyomtumealiswaliharakaawahikumchukuwa motto iliambembeleze.(6)

Abdilahi bin Salaam mmojakatikamakureishiwamadinakatikazamazamtume,anazungumzajinsiambavyoakhlaqyamtumeilimfanyaaingiekatikauislamu. BaadayakuingiauislamumarakwamaraakawaanamnasihirafikiyakewakiyahudiaitwayeZaydi bin Shaabeiliaingiekatikauislamu, naakawaakimuelezajuuyautukufuwauislamupamojanaakhalaqnjemaya bwana mtume(saw). AnasemasikumojaalipoingiamsikitinialimkutarafikiZeydiyakeamesimamakatikaswafuyawaislamutayariameshasilimu,akamwendeakumuulizasababuzakusilimukwake,Zeydiakasema:nilikuwapekeyangundaniyanyumba,nanikisomakitabu cha tauratinilipofikakipengelekinachozungumziasifazaMuhamad,nikasomakwamakininakukaririsifamojamojailiyotajwakatikatauratijuuyamtume,nikaona bora nimuendee Muhammad nakumtahini.sikukadhaanimemuendeanakilakituchakenakuangaliakwamaikninikazionasifazotezilizotajwa,ikabakisifamojaambayolazimaniikamilishe,inasemakuwauvumilivuwa Muhammad unaonekanamachonimwakekilamajahiliwakimuendeahawaonikwakeilauvumilivu. Nilikwendamsikitinisikumojailikuangaliasifahiyo,nikamuonabeduiamekujakapandafarasi,alipomuona Muhammad alishukanakumwambia;nimekujanatokakatikakabilaFulani,naukameumetufanyakuwamakafiri. watuwakabilahiliniwaislamunahawanakitu,wanatarajikuwautawafanyiaihsan. Muhammad(saw) akamwambia imam Ali,jekunachochotekwako? Imam Ali akasemahapana,hapohaponikamuendeananikamuombanimpekiasi cha pesakwashartiwakatiwaanipekiasi cha tende. Mtume (saw)akakubalinakuchukuwazilepesanakumpa Yule bedui.

Nikakaakusubiriwakatiwakuvuna,nikamuona Muhammad akishughulikanamazaziyamtummoja,maraakakaachiniyakivulinamasahaba wake piawakakaasehemumbalimbali. Nikamuendeanakumwambia “Ewe mtumeunarudishamalizawatuna kasha hurudishi? Unajuwaumebakiwanamudamchachesanakutimizaahadiyako? Mara nilisikiasautiyaukaliya Omar bin Khatwabaliyetoaupanga wake nakuelekeakwangunakuniambiaondokahapambwawewe! Muhammad akamkatazaasinishambulienakusemahainahajayakufanyahasira ,huyuanatakiwaaelimishwekwaupolenauvumilivu. AkamwambiaOmar,nendasehemu Fulani nachukuakiasi Fulani cha tendeumleteeZeydi. WakaongozanaZeydina Omar nabaadayakumpatendealimzidishiavibabaishirini. Zeydialipouliza Omar akamwambiahiyondiyosubirayaMuhammad,kwakuwaMuhammadiameniamurunikuzidishieilikukufurahishabaadayakuwaulichukizwa”

Hiyoikanithibitishiaupolenauvumilivuwa Muhammad nahaponikaamuakusilimu.

Katika kumzungumzia mtume na akhlaq zake,imam Ali anasema: daima mtume alikuwa na uso wafuraha, tabasamu, upole, hakasiriki,hanamaneno mabaya, wala hakuwa mwenye kutoa aibu za watu,kila aliyekuja nyumbani kwake hakurudimtupu. alijitenga na mambo matatu:

1.   Kujadiliana sana katika mazungumzo.

2.   Kuzungumza sana.

3.   Kuchunguza mambo yawatu yaliyojificha, ila katika yale ambayo yaliwajibika kufanyiwa hivyo nayaliyo kuwa yameridhiwa na Mungu.


Rejeo:

1.      3:159

2.      Mustadrak al-wasail,juz.11,uk.194

3.      68:4

4.      Bihar al Anuar,juz,2,uk.172:Lam alwara,uk.120

5.      Wasail al-shi’a,juz.21,uk.480